Upatikanaji Dawa Muhimbili Wafikia Asilimia 97

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Hospitali ya Taifa Muhimbili na Amana zimesema upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa sasa ni asilimia 97.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam Mfamasia wa Hospitali ya Muhimbili, Nelson Faustine amesema, hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika taasisi hiyo imeimarika na wameshuhudia mabadiliko makubwa yaliyofanyiwa na Rais DK 'Samia Suluhu Hassan.

"Tumetoka asilimia 30 hadi zaidi ya asilimia 97 upatikanaji wa dawa katika hospitali yetu ya Muhimbili-Upanga na- Mloganzila ni hatua kubwa idadi ya wagonjwa imeongezeka kulingana na bajeti, kwa sasa manunuzi yetu ya dawa kwa MSD ni zaidi ya Shilingi bilioni sita kwa mwezi na kwa mwaka ni zaidi ya Sh. bilioni 24," alisema.

Alitoa wito kwa serikali "Kuongezeä mtaji " MSD* Kama ilivyoahidi na kufuta madeni ya nyuma ili kuwezesha taasisi hiyo kujiendesha. Nelson alitaka taasisi hiyo ikiwa ni kati ya wateja wakubwa kwa MSD wanapata huduma kwa kipaumbele cha pekee. Kadhalika, wameitaka MSD kuboresha huduma Muhimbili hususani huduma za kibobezi kuendana na mahitaji ya dawa na vifaa tiba vyake kama vya kupandikiza figo, uboho na uroto ambapo chupa moja ndogo ya dawa hizo ni hadi Shilingi milioni tatu.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Amana, Dk. Brayson Kiwelu, alisema mafanikio makubwa yaliyopo yamechagizwa na Rais Dk. Samia kutokana na maboresho aliyoyafanya sekta ya afya.

"Amana imeweza kupata zaidi ya Shilingi bilioni tano ambazo zimewekezwa katika jengo la kisasa la Ct Scan, X-ray, jengo la dharura, ukarabati wa jengo la wagonjwa mahututi na maboresho kitengo cha usafishaji damu kwa wagonjwa wa figo.

"Ukarabati huu umeendana na uwekezaji wa vifaa ambapo asilimia 70 ni kutoka MSD, tunajivunia hali ya utoaji huduma na upatikanaji wa dawa ni zaidi ya asilimia 97 changamoto ni dawa za wagonjwa wa saratani, hata hivyo tuna kifungu cha bajeti ya dharura tunazonunua dawa ambazo hazipo," alisema.
 
Mh nyie kijan sio wa kuwaamini ngoja raia wafike on point itajulikana kama dawa zinapatikana kwa wingi bila usumbuf.
 
Back
Top Bottom