Muhimbili yasaini mkataba kuboresha upatikanaji dawa Muhimbili

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), leo imesaini mkataba wa makubaliano na kiwanda cha Kairuki KPTL kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa dawa Muhimbili upanga na Mloganzila.

Mkataba huo umeanisha maeneo mawili,Kuboresha upatikanaji wa dawa ambazo hazipatikani kwa urahisi kwenye soko ikiwemo zinazotumika katika upandikizaji wa viungo mbalimbali mwilini kama Figo,Kongosho pamoja na dawa zenye ujazo mdogo zinazotumika kwa watoto na wagonjwa wa saratani.

Eneo la pili la makubaliano ni kuwajengea uwezo wataalamu wa Muhimbili katika uzalishaji wa dawa na namna ya kuongeza kuzitumia dawa zinazozalishwa na kiwanda hicho.

Mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amesema hiyo ni hatua nzuri kuwepo kwa kiwanda cha dawa ambacho kinamilikiwa na wazawa na kukidhi viwango vinavyohitajika.

Pia, amefafanua kuwa Muhimbili ni hospitali ya Rufaa ya kitaifa ni kubwa kuliko zote nchini ina vitanda 2,150 ambapo upanga kuna vitanda 1,550 na Mloganzila kuna vitanda takribani 600 hivyo inawahudumia wengi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha dawa cha Kairuki Dk.Muganyizi Kairuki amesema kiwanda hiko kimedhamiria kuzalisha bidhaa kulingana na mahitaji yaliyopo na kuhakikisha mkataba uliopo unakuwa na tija kwa hospitali.
 
Back
Top Bottom