Uozo wa nssf arusha room #8

MZEE SERENGETI

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
214
10
Nasikitishwa sana na wafanyakazi wa NSSF Arusha kwani mteja akiingia wanakuona kama msumbufu na
wao wamebaki wanatafuna maandazi na kuzungumza kwenye simu zao. Hivi kweli ndiyo Ofisi ya kibiashara ilivyo? Mbona wanafanya kazi kama wafanyakazi wa Serikali Kuu.

Ingawa Mkurugenzi Mkuu, Dr. Ramadhani Dau wakati wa Mkutano wa Wadau uliofanyika Arusha, alidai kwamba Ofisi ya Arusha imefanyiwa marekebisho katika utendaji wake. Kumbe ndio hamna kitu.

Njoo kesho zimezidi kwa wanaofuatilia madai yao.
 
kama ile nssf ya TMK yaani wanapokaa walipakodi kuna joto, pananuka majasho. ukiingia kwenye vyumba vyao kuna viyoyo vinapuliza. nssf ni full dharau.
 
It works like this, NSSF wanakuona wa maana pale ambapo bado unachangia, ila ikifika wakati unahitaji mafao yako hawakutaki kabisa.
 
Hakuna watu wazembe kama Nssf Arusha Br.
mWAKA JANA NILIFUATILIA HAKI ZA JAMAA YANGU kwa mara zaidi ya 20, ikabidi ni niwapigie maafisa fulani Dar ndipo wakalifanyia kazi faili langu!
Kuna mtu nilikuwa nahudhuria naye hapo, akaambiwa live kwamba aahidi atakata percent ngapi akisaidiwa fasta!...Na kwa vile jamaa alikuwa jobless na maisha yanmemfinya, akaahidi ten percent, akachangamkiwa, mimi nikaja kushugulikiwa 3weeks later!

Muda wote wanazunguka tu kule ndani, huku wakionyesha macho ya kuuliza kwamba "una hela?"...
Milangoni unapoingia kwenye vyumba unakutana na vyeo vizuri sana kama.."SENIOR BENEFITS OFFICER"...sijui "PRINCIPAL-NANINIINO"..kumbe wote wapuuzi sana!
 
hapo ni ktk kutoa huduma za kijamii na wanajamii ndio watu wenye hela zao pale nssf je wakianza kuzalisha umeme c kiburi kitongezeka. kuna shm nilikua nafanya kazi nikaacha kazi ili nikasome kimbembe ni kupata hayo mafao yng mpk naandika hapa hakuna kitu na hela ni zangu mimi naletewa jeuri wanataka nitoe psa ila nipate pesa yang mi nimegoma wakaijickia watanipa
 
Nyie mnakosea, ukienda pale akakwambia anataka kitu kidogo, mkubalie bila shida, nenda kachukue hela za moto mpe acheze nazo basi.
 
Kila ofisi ina kero zake.
Hawajui kama bila sisi hawana kazi pale.
Peleka malalamiko kwa wakubwa wao.
 
Back
Top Bottom