NSSF ifanyiwe ukaguzi wa uhakika kimaadili na kiutendaji

NEWSINKP

Member
Sep 26, 2016
77
92
Habari wana JF!

Ndugu zangu ninawaomba kila mmoja kwa wakati wake akiweza apite kwenye tawi lolote la NSSF nchini atake kupatiwa huduma yeyote ajionee jinsi pesa za walipa kodi zinavyotumika kulipa wapiga stori wanaojiita wafanyakazi.

Nimewahi kufika tawi la Arusha mjini kwenye kitengo cha benefits nikashuhudia kuna foleni ya watu wanasubiri huduma halafu wafanyakazi tunawaona kabisa wanapiga stori tena personal kabisa wako watatu hadi mzee mmoja akapaza sauti kuwaita kwa ukali ndio wakaja. Hapo hapo Arusha nilipeleka form yangu ili waitume tawi la Moshi wakaipokea ila hawakuituma hadi nilipofuatilia makao makuu Dar na ikabidi nisubmit copy na ile original niliacha Arusha gorofa ya pili ofisi namba 4 hawakufanya lolote.

Niliwahi pekeka form yangu ya marekebisho toka kwa mwajiri wangu 2021 September kituo cha Moshi mjini ambapo ndipo mwajiri wangu alikua akipeleka michango yangu ila mpaka mwaka 2023 June michango ilikua haionekani ikabidi nianze kufuatilia branch ya Kibaha nilipokua naishi ndipo NSSF Moshi wakai update kwenye system yao ndio nikawa naiona michango yangu.

Yaan kuna negligence na majibu ya ajabu mno toka kwa wafanyakazi asilimia kubwa wa nssf. Ila NSSF ya Kibaha ina wamama flan wana spiriti sana ya kazi, siku za j3 kunakuwaga na foleni kubwa mno lakini hawa wamama nilishuhudia waliita wateja wakasikiliza shida za kila mmoja na kuzitatua ndani ya muda mfupi sana. Kiukweli sehemu zingine mtu ameenda NSSF kuangalia statement tuu anakalishwa masaa 5

Hivi hakuna team inayoweza kuzunguka nchi nzima watu watolewe waajiriwe wengine, wapo vijana wengi mtaani wachapa kazi hawana ajira, ikifanyika safisha safisha hata kwa mwaka mara moja nidhamu itakuepo.
 
Nyie watoto punguzeni hizi tuhuma za kipuuzi..

Unafahamu wangapi wananufaika na NSSF?

STUPID
 
Moderators hizi tabia za kulea Uzi zinazodharirisha taasisi za UMMA sio haki..try to be fair
 
Sasa mbn unanitisha nilitaka nikajiunge nao maana wamepita mtaani kutoa elimu kwa wajasiria Mali ila sikupata elimu yakutosha sasa nimepata nakutana na hili swala lako Sasa apa unanishaurije🤣🤣
 
Hili ni tatizo sehemu yeyote ambayo Watanzania wameachwa wenyewe wafanye kazi.

Mtanzania anahitaji unyapara muda wote ili afanye kazi.

Haya ni madhara ya siasa za CCM za ujamaa na kujitegemea, tumezalisha kizazi cha wavivu, wapiga soga, malaya, wezi, wanafiki, wabishi wabishi bila logic.
 
Moderators nakazia huu Uzi ni ukweli mtupu, wahuni watakuja kupinga acha inyeshe
 
Tuache unafki vijana kutwa kulalamika hamna ajira lakini wakipata ajira hawafanyi kazi. Kutwa kulaumu wazee wameshikilia nafasi maofisini, lakini hao wazee ndio wachapa kazi.
 
Nyie watoto punguzeni hizi tuhuma za kipuuzi..

Unafahamu wangapi wananufaika na

Sasa mbn unanitisha nilitaka nikajiunge nao maana wamepita mtaani kutoa elimu kwa wajasiria Mali ila sikupata elimu yakutosha sasa nimepata nakutana na hili swala lako Sasa apa unanishaurije🤣🤣
Kajiunge tuu mkuu ila lazima tuseme ukweli NSSF kuna branch zina watu wazuri ila nyingi zina shida kubwa mnoo, mi nina zaidi ya miaka kumi huko
 
Nyie watoto punguzeni hizi tuhuma za kipuuzi..

Unafahamu wangapi wananufaika na NSSF?

STUPID
Mkuu soma tena mada uielewe hakuna sehemu imeongelea kua hainufaishi, issue ni huduma. Please read between the lines
 
Kajiunge tuu mkuu ila lazima tuseme ukweli NSSF kuna branch zina watu wazuri ila nyingi zina shida kubwa mnoo, mi nina zaidi ya miaka kumi huko
Kuzungushwa utazungushwa lkn mafao yako utapewa tu sindio na inaweza chukua mda gani
 
Hili ni tatizo sehemu yeyote ambayo Watanzania wameachwa wenyewe wafanye kazi.

Mtanzania anahitaji unyapara muda wote ili afanye kazi.

Haya ni madhara ya siasa za CCM za ujamaa na kujitegemea, tumezalisha kizazi cha wavivu, wapiga soga, malaya, wezi, wanafiki, wabishi wabishi bila logic.
😄😄😄😄😆Htari hii
 
Kuzungushwa utazungushwa lkn mafao yako utapewa tu sindio na inaweza chukua mda gani
Unawezaje kumzungusha mtu kwa delays zinazohusisha wafanyakazi wa ndani(wa nssf) na wakati mtu ametimiza kila taratibu za kisheria. Tuweni serious tuache kutetea uzembe. Mfano kuna waajiri hawapeleki michango ya wafanyakazi wao mpaka miaka 2 halafu hapo utasema kuna utendaji lazi? Ukizingatia sheria ipo wazi kua mfanyakazi kila mwezi akatwe 10% na muajiri 10% sasa kwa nini mpaka inafika miaka 2 nssf wako wapi wasifanye ukaguzi wanakula tuu hela za walipa kodi
 
Inategemea kama michango yako iko vizuri ni ndani ya mwezi tuu unalipwa mafao yako.
 
Back
Top Bottom