Uozo TTCL Broadband | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uozo TTCL Broadband

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by gnasha, Oct 15, 2008.

 1. g

  gnasha Member

  #1
  Oct 15, 2008
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani TTCL broadband mnatufilisi wateja wenu. Sisi ni wateja wenu wa miaka mingi sana. Sasa hii tabia mlioianzisha hivi karibuni sio nzuri kabisa. Tukiweka pesa kwa ajili ya internet ya Broadband baada ya wiki 2 mnafunga hata kama kuna hela imebaki. Halafu tukiwafuata mnasema tulipie shilingi elfu 25,000/- hivi mnafikiri pesa zinaokotwa? Mwezi uliopita nimelipia sh. 25,000/- mwezi huu mmenikatia tena mnaniambia nilipie tena sh. 25,000/- bado sijaweka hiyo vocha ya sh 10,000/-. Huo ni wizi wa kimachomacho. Mimi ni mwananchi wa kawaida wa kipato cha chini nimebahatika kuwa na line na simu nikabahatika kuwa na computer yangu ya Pentium lll na nikaamua kuweka na internet sasa kwa mtaji huo mnaotupeleka wa kulipa pesa nyingi hatutaweza. Tulitegea TTCL ni ya serikali ipo kwa manufaa ya wananchi wote kumbe tumekosea inawalenga wenye nazo. Tunaomba mjirekebishe. Mnatuumiza kwa mwendo huo.
   
 2. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hiyo 25,000/- wanasema ni kwa ajili ya malipo ya nini?


  Zantel wameanza kutoa huduma mikoani. Sifahamu bado idadi kamili ya sehemu inapopatikana huduma ya wireless Internet ya Zantel.
  Wakati TTCL wanatoza 260 per MB, Zantel ni 55/MB  .
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Oct 15, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  nenda pale extelecom watakufa report ya matumizi yako ya mtandao na jinsi unavyonunua hizo vocha ukipata hiyo sasa utaweza kulalamika au kunyamaza au kuamua kuchukuwa hatua zaidi au piga 104
   
 4. Tanzania 1

  Tanzania 1 Senior Member

  #4
  Oct 15, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 197
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nadhani 25,000/- za mwanzo ni kwa ajili ya kupewa modem.

  Mimi TTCL ilishanishinda siku nyingi! Mafundi wa TTCL waliniambia kuwa tatizo ni modem (disc-shaped) walizozitoa mwanzo. Wakanishauri ninunue modem mpya (wkt huo) ambazo walikuwa wakija nazo "ku-boost" modem yangu. Niliwaambia: "ikiwa ninyi mafundi wenyewe mnanishauri kubadili modem, nami hiyo modem nimeinunua kwenu, k/nini ninyi msiushauri utawala utubadilishie hizi modems?" Walinishauri niandike barua ambayo itahusisha ushauri wao huo (wa kubadilishiwa modem). Nilandika barua, na kweli nikabadilishiwa. Modem mpya haikuwa na matatizo, kasheshe ikawa matumizi! TTCL ilinishinda!!

  Zantel nao walianza vizuri, lkn nadhani walikuwa ktk promotion kwani charges zao ziko juu hivi sasa! Nadhani nayo itanishinda.

  Sijui tukimbilie wapi?!
   
 5. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  Nilitizama matumizi ya Zantel hata miezi miwili haijaisha kwa mtu anayetumia huduma yao. Nimethibitisha kwamba wana-charge sio zaidi ya 60Tsh per 1MB. Kama kuna mabadiliko basi yatakuwa ya hivi karibuni.

  Have you disabled Automatic Windows Updates? Antivirus update pia ni ya kubadili schedule yake isiwe ina-download kila siku. Update ya once per week or twice per month should be OK.  .
   
 6. g

  gnasha Member

  #6
  Oct 16, 2008
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni malipo ya kuunganishiwa tena sababu wamekata mawasiliano.
   
 7. g

  gnasha Member

  #7
  Oct 16, 2008
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mimi sina matatizo na matumizi yangu, nina tatizo na wao kubadili system yao bila kututaarifu wateja atleast wangetutangazia maana wengine tuna safiri mara kwa mara. Nikisafiri more than 2 weeks nikirudi ninakuta mtandao umeshakatwa tena nitakuwa nafanya kazi ya kulipia kuunganishwa upya kila nikirudi safari? I will try to find another way lakini sio sahihi kufanyia hivyo wananchi.
   
 8. g

  gnasha Member

  #8
  Oct 16, 2008
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nitacheck hao zantel huduma zao vipi. Nashukuru kwa ushauri
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Mkuu pole sana.
  Mimi mwenyewe nilikuwa nakumbwa na msuko suko kama huu lakini nilihama siku nyingi sana hao TTCL wababaishaji hama mkuu nenda ZANTEL wana bei chee kuliko hao wanao jiita wazarendo kumbe ndo wakabaji wakubwa.
  Ususe huo mtandao hama utafilisika kila mwezi watakuwa wanakukamua bado charges zao kubwa sana.
   
 10. g

  gnasha Member

  #10
  Oct 16, 2008
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante. Wamejisahau kuwa biashara ni ushindani.
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ndo tatizo letu sisi wa TAnzania eti kwa vile ni shirika la umma basi wao wanajali matumbo yao kujaa kazi wanasahau.
  Angalia mfano zile cmu za mkononi za kwao TTCL leo hii katika soko zimeporomoka sana utamwona mmoja mmoja anayo wameshindwa kabisa utendaji....Hivi huu uozo nani anaweza kuifumua TTCL pale rais au nani?Afanye timua timua na kuweka management mpya..
   
 12. g

  gnasha Member

  #12
  Oct 16, 2008
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inatia hasira sana.
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Chanzo ni serikali haramu hii ya sisiemu ambayo inaihujumu kampuni yake binafsi kwa kubadilisha management kila kukicha na kuweka management ya kitapeli.
  Ni aibu kusema lakini ndio ukweli kwamba serikali hii imetaka kuhakikisha kuwa TTCL inakufa.
  Wana lao jambo.
   
 14. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nashukuru mkuu kwa kutujuza haya,,,, mimi binafsi natumia TTCLBB na TTCL Mobile. Sikuwahi kufuatilia zaidi,,,,kuanzia sasa nitafuatilia hii issue nione iko vipi. Asante Mkuu
   
 15. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2008
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145


  MF, umesema kweli. Hii sio kampuni ya wazalendo tena kama wachangiaji wengi humu wanavyodhani. Hii kampuni sasa haijulikana hata iko chini ya nani. kila mtu anakuja anajichukulia na kuondoka zake. Saskatel waliopo sasa hata kutangaza biashara ya TTCL hawatangazi tena maana wanaona ni upotevutu wa hela ambazo wanaweza kuzipeleka kwao. Jiulize mara ya mwisho ni lini umeona tangazo la ukurasa mzima la TTCL kama wanavyofanya wenzao wa Zain, Vodacom na Tigo???? Tusiwalaumu sana waswahili wenzetu waliopo pale, bali tuwashikie bango watawala wetu na kuwauliza kulikoni???
   
Loading...