hp4510
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 8,916
- 9,727
Mimi Nilikuwa ni system adm wa kampun moja ya wazungu hapo Masaki, sasa jana bosi wangu alikuwa na mkutano wa online na mkurugenzi mkuu ambae yupo Marekani.
Kutokana na umuhimu wa hayo maongezi yao ikabidi bosi wangu aniombe ushauri kuhusu ni mtandao gani ambao una strong internet connection.
Kutokana na matangazo ya TTCL ya siku hizi, nikaona hawa jamaa watakuwa wamebadilika sana, kumbe Dah Nilikuwa naingia choo cha kike, nikamshauri bosi wangu kwa mbwembwe nyingi kuwa TTCL ni best kampany.. mmh nikapewa pesa za kwenda kununua line ya TTCL, nikaenda moja kwa moja makao makuu pale Samora, kufika pale nikanunua line kwa sh 2000 na muda wa maongezi....
Huwezi kuamini ishu ya kusajili line tu ilinichukua masaa 3 mpaka bosi akawa ananipigia simu kwamba vipi tena mbona unachelewa?
Ikabidi niondoke kurudi ofisini na yule mhudumu akaniambia niweke line kwenye simu na itafunguka tu yenyewe, nikafika ofisini nikampatia bosi wangu ile line na nikampa maelezo kuwa aweke kwenye simu na itafunguka tu yenyewe....
Dah mpaka saa 12 jioni hakuna kitu, bahati nzuri nilichukua namba ya yule dada alienihudumia nikampigia simu, jibu lake ndio niliishiwa pozi zote...
Akasema kesho asubuhi niende na hiyo line oh my god bosi akaanza kubadilika rangi akaanza kupiga simu kwa wazungu wenzake na kila mzungu akawa anatoa lawama kwangu kuwa why nilichagua TTCL ikiwa wenyewe tu wafanyakazi wa TTCL hawatumii huo mtandao....
So kwa hasira bosi kanifukuza kazi coz nimempa ushauri wa kampuni ambayo Nilikuwa najua fika kuwa huduma zake ni mbovu.
Ushauri wangu kwa TTCL ni kwamba fungeni hiyo kampuni yenu mpaka hapo ambapo mtakuwa tayari kuingia kwenye soko la ushindani.
=======
MAJIBU TOKA TTCL:

Ndugu hp4510
Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) inaomba radhi kwa matatizo na usumbufu uliotokea.
Maoni yako ni muhimu kwetu na yametupa changamoto ya kuendelea kuboresha zaidi huduma zetu na kuchukua hatua stahiki kwa wafanyakazi wetu.
Tafadhali kwa mawasiliano zaidi, wasiliana nasi kupitia customercare@ttcl.co.tz au unaweza kupiga namba 100 (Kwa kutumia laini ya TTCL) au 0222 100 100 (kwa kutumia mitandao mingine) ili tuweze kushauriana zaidi.
Pia unaweza kutembelea Kituo chetu cha huduma kwa wateja kilichopo Posta, Mtaa wa Samora ili uweze kuonana na Meneja wa TTCL mkoa wa DSM kati, Ndugu Diwani Mwamengo kwa kushauriana zaidi, Ndugu Diwani anapatikana kwa simu namba 0732 100 008.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
18/08/2016