TTCL wakosa ubunifu, Serikali wanyanganyeni mkonga wa Taifa

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,143
3,222
TTCL
Inaonekana wazi kabisa kwamba TTCL wamekosa ubunifu na ujunzi wa kutatua matatizo sugu yanayotukumba wananchi na Taifa kwa ujumla. Hii ni kwa sababu, japo tuna mkonga wa taifa-Fibre backbone Network, lakini, speed ya internet ipo chini sana na bei iko juu mno. Kutokana na hii speed ndogo ya internet na bei kuwa juu hali hii inavuruga uchumi wa mtu mmoja mmoja na wa Taifa. Kwa sababu mkwamo huu una discourge new starters ktk utumiaji wa ICT hasa na ktk kupata leverage yake ili kujinasua na umasikini.

1. Mfano, hakuna chochote kinachoelezeka kwanini mtandao una speed ya kinyonga. Hill lina maelezo mafupi tu kwamba TTCL wameshindwa kutumia teknolojia sahihi itakayowezesha kuli leverage hiyo Fibre backobone waliyo nayo.

2. Mfano, hakuna maelezo sahihi kwanini bei ya TTCL ni bei kubwa na unaffordable kwa mwananchi wa kawaida. Kwa mfano bandwidth ya 1Mbps TTCL na Tanzania kwa ujumla bei yake ni zaidi ya milioni moja. Inamaana 360Mbps kwa Tanzania utanunua karibu nusu bilion, nani mwenye hela hizo? Wakati wenzetu huko ulaya kwa 360 Mbps wananunua kwa sh elfu 70 yani euro 30 tu, nitakuwekea picha hapo chini na link.
Hii ya bei kubwa wasisingizie eti kwa sababu eti networks yetu imekaa vibaya, hapana ni kwa sababu wamekosa ubunifu na wamegota. Sasa ili ku compasate huu mugoto basi wanakuja na rocket price, na hii price haiwasaidii zaidi inawadidimiza zaidi.

3. Kutokana na shagalabagala huku, ndio maana local traffic sio local tena. Specifically speaking, mfano upo Manzese unaongea na server iliyopo buguruni, basi mara nyingi kama sio mara zote traffic hiyo itatoka manzese ianze, Manzese->London- New York->Buguruni. Hii si tu inakuwa na high vulnerability yakuwa sniffed kwa sababu inapita kwa mabepari, bali pia inaongeza slowness ambayo haikuhitajika kabisa.

serikali
Wanyanganyeni TTCL huo mkonga wa Taifa-The National Fibre Backbone Networks.
Mkishawanyanganya, serikali anzisha kampuni nyingine ambayo itasimamia huu mkonga wa Taifa. Hii kampuni iwe wholesaler tu, iwauzie bandwidth ISPs, Operators na TTCL included. Hii kampuni ije na solution sahihi ya teknolojia sahihi ya kutumia huu mkonga wa Taifa.

serikali, punguza bei ya kutumia mkonga yani 100Mbp atmost iwe sh laki moja.
Hii ita encourange watumiaji na waanzishaji wa biashara. Na hii itaweza kuwezesha kuongeza local traffic kuwa nyingi zaidi.
Kwanini local traffic zitaongozeka? makampuni ya nje yatakuja kwa wingi kufungua Datacenters na kuziweka hapo Tanzania kwa sababu uplink za datacenters zao bandwidth ipo na affordable.

Tatizo la bei Kubwa.
Hili tatizo limesababisha hata wenye vijiwebsite na vijiserver kuviweka nje ya nchi, na hivyo kuongeza gharama na umbali wa traffic kusafiri kwa sababu tu ya TTCL kukosa ubunifu.

Mwisho serikali
Mie nipo kuwafanyia consultancy kama mkihitaji, tubadili hii hali ya mkwamo iliyopo, nitawatengenezeeni network ya kisasa ambayo ita turn hii tide na adha inayomkumba mtanzania. If any, please give me shout.

Best Broadband- 360Mb Unlimited | Virgin Media Ireland
Ref, find it attached and enjoy.
 
Attachments

  • internet-pic.png
    internet-pic.png
    58.2 KB · Views: 102
Kiufupi maadamu wanasiasa ndiyo wamiliki au wana share tigo,vodacom na airtel suala la ttcl kufanikiwa sahau
Ni kweli
Ndiyo maana naonelea serikali iwanyanganye huo mkonga wa Taifa, iunde kampuni nyingine ambayo itasimamia huo mkonga. Ikumbukwe TTCL ni wasimamizi tu wa mkonga sio wa kwao.
 
Bila kuwanyanganya TTCL huo mkonga wa Taifa, hakutakuwa na na maendeleo sawia ya ICT. Serikali yapaswa kuliangalia hili jambo kiundani zaidi.
 
MkamaP, hiyo kampuni nyingine itakuwa na tofauti gani na TTCL?
Utendaji wa Watanzania ni huo huo. Labda useme wauuze kabisa kwa kampuni binafsi.

Muhimu ni TTCL kupata management mpya na kupewa Uhuru wa kuibadili kampuni bila kuingilia sana na wanasiasa.

Ni kweli TTCL kwasasa ni mzigo na hawana uwezo wa kushindana kwenye dunia ya Leo. Ni kama kwenye miti kukosa wajenzi. Wana kila kitu lakini hawana uwezo wa kuchomoka toka hapo walipo.
 
mkuu labda ungepigia debe suala la ndoa kati ya TTCL na AIRTEL iishe kwanza maana sizani kama hawa jamaa wameondoka na TTCL imerudi serikalini 100 percent, ndo tuje tupiganie hayo mengine kama bado itashindwa simamia
 
Dawa si kupigania ndoa, mpaka lini? Hii ninayowapa serikali ndo moja ya njia ya kuachana na airtel.
Wanyanganywe mkonga wa Taifa na wasipokuwa wabaunifu wafe natural death, wakati huo huo wanakabidhi kampuni mpya ya serikali yenye hisa 100% kusimamia tuseme waiite Tanzania Broandband ama Tanzania Open Access Networks. Mkuu wewe huoni napigania kuiondoa TTCL kwa airtel?
 
Mbona kama Airtel tayari wameondoka TTCL?

Pia mkongo unamilikiwa na serikali na TTCL wanausimamia tu. Baada ya Airtel kuondoka ndio watakabidhiwa TTCL kuumiliki.
 
Mbona kama Airtel tayari wameondoka TTCL?

Pia mkongo unamilikiwa na serikali na TTCL wanausimamia tu. Baada ya Airtel kuondoka ndio watakabidhiwa TTCL kuumiliki.

Tatizo mkuu sio kuumiliki, tatizo wameshindwa kuutumia kupunguza bei ya internet na speed ni ndogo. Haiingii akilini ununue 100Mbps kwa milioni mia moja. Wakati kwingine wananunua hiyo hiyo 100Mbps kwa laki moja. TTCL inabidi wanyanganywe huo mkonga na waunde kampuni nyingine litakalokuja na adds-on na mwelekeo mpya. Nisawa sawa na ATCL uwakabidhi ndege mpya

TTCL wana mindset ilele, mentality ile ile na mwelekeo ule ule, hawa niwagumu inabidi wasituliwe.
 
we jamaa umetumwa lazma maana naona unang'ang'ania tu wanyang'anywe watakusikia na watakupa kazi iyo kama ulivyosema
 
Mbona kama Airtel tayari wameondoka TTCL?

Pia mkongo unamilikiwa na serikali na TTCL wanausimamia tu. Baada ya Airtel kuondoka ndio watakabidhiwa TTCL kuumiliki.
umetumwa na nani mbona povu jingi? wasalimie airtel wambie sasa TTCL ni mwendo mdundo.
 
  • Thanks
Reactions: aye
we jamaa umetumwa lazma maana naona unang'ang'ania tu wanyang'anywe watakusikia na watakupa kazi iyo kama ulivyosema

Ha ha ha
Sio lazima, angalia tangu mkonga wa Taifa umekamilika ni lini? angalia na bei na speed ya mtandao.
Na kitu kingine
OPERATORS, TIGO,VODACOM, AIRTEL na wote unaowafahamu wanatumia mkonga wa TTCL, sasa cha kujiuliza kwanini VODACOM,TIGO nk wana make profit na TTCL wana struggle kwa market wakati hao wanao make profit wanatumia mkonga wa TTCL?
TTCL inapaswa wanyanganywe pretext zao za airtel hazima mashiko. Hata ATCL wangikuwa wana joint venture na precision air lazima wangesema sababu ni precision air ndo maana wana struggle kwa market.
 
Hao wenye maamuzi ndo wana share zao huko kwengine unategemea nn hapo
 
Hili la TTCL mbona kuna mdau alilieleza vya kutosha humu ndani katika mada yenye kichwa cha habari: Why TTCL is not the leading Cellular and internet Operator? Na wajuzi walichangia mada vizuri tu.
 
Hili la TTCL mbona kuna mdau alilieleza vya kutosha humu ndani katika mada yenye kichwa cha habari: Why TTCL is not the leading Cellular and internet Operator? Na wajuzi walichangia mada vizuri tu.

mkuu kweli nafikiri mtoa mada akaitafte iyo topic atapata majibu
 
Hili la TTCL mbona kuna mdau alilieleza vya kutosha humu ndani katika mada yenye kichwa cha habari: Why TTCL is not the leading Cellular and internet Operator? Na wajuzi walichangia mada vizuri tu.

Msichanganye vitu.
TTCL kwa sasa wana act kama wholeseller na operator. Ninachosema hapa nikuwa, wananyanganywe hiyo whole sell wabaki kuwa operator ama retailer kwa end end users. Jinsi wanavyoachiwa huo mkonga wa Taifa, wanakuwa wana act kama retailer na wholesale kwa wakati mmoja. Hii kitu wamefail.

Ni nyema TTCL wanyanganywe huu mkonga, serikali iunde kampuni nyingine ya kusimamia huu mkonga. TTCL wao wabaki kama operator na ISP.
Kazi ya ISP mara nyingi ni kukuunganisha kwenye internet ambayo wamekuwa wamenunua ile internet ama voice Gateway. Lakini Fibre optics backbone network kazi yake ni hasa ina deal na traffic between MANs, yani Matropolitan Access Network. Hii sio Cellular and internet Operator, japo ina kitu kimoja tu common. Ni kitu kimoja tu ambacho kiko common.

Kazi hasa ya Backborne Networks-mkonga wa Taifa ni kubeba traffic kama za cable Television, nk. TTCL wameufelisha mkonga wa Taifa. Nyie angalieni bei mnayonunua hamtakiwi kununua bei hiyo mara 1000 chini.
 
Na kitu kingine
OPERATORS, TIGO,VODACOM, AIRTEL na wote unaowafahamu wanatumia mkonga wa TTCL, sasa cha kujiuliza kwanini VODACOM,TIGO nk wana make profit na TTCL wana struggle kwa market wakati hao wanao make profit wanatumia mkonga wa TTCL?
.

TTCL inahitaji mabadiliko makubwa kwenye management yao. Timu yao ya masoko nadiriki kusema imekosa mbinu na uwezo wa kuuza bidhaa zao.
 
Back
Top Bottom