Rais Magufuli apokea gawio la TTCL la Tsh. Bilioni 2.1! Ashangazwa na Ofisi yake kutotumia TTCL, ataka ndani ya mwezi Viongozi wawe wanatumia TTCL

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Rais John Magufuli asubuhi ya leo Mei 21, 2019 atatembelea Makao Makuu ya TTCL na kupokea gawio kwa mara ya pili mfululizo.

Gawio hili linatajwa kuwa ni kubwa zaidi ikilinganishwa na mwaka jana.
IMG_20190521_094412.jpeg



UPDATES:
>>> Rais amefika katika Ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Simu Tanzania, TTCL. Akiwa hapo ameanza kwa kuzindua 'Video Conference' iliyofanyiwa marekebisho ambapo ameweza kuongea na Wakuu wa mikoa kadhaa kwa pamoja

>>> Sasa anaendelea kukagua mambo sehemu na vifaa mbalimbali ndani ya ofisi hiyo

Mkurugenzi Mkuu TTCL, Waziri Kindamba.
> Kwa mwaka huu TTCL inakabidhi gawio la jumla ya shilingi Bil.2.1 lililopatikana kutokana na ongezeko la mapato ya mwaka jana kutoka shilingi Bil.119 hadi Bil.167 kwa mwaka huu

> Tunaahidi kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kutimiza wajibu wa kisheria wa kuchangia Pato la taifa kulingana na huduma zetu zitakavyozidi kuimarika na kuongezeka

> Miongoni mwa mambo yaliyofanyika ndani ya mwaka huu ni pamoja na kuboresha huduma kwa wateja,kuongeza uwezo wa teknolojia na miundombinu pamoja na kuendelea kuwa msimamizi mahiri wa mkongo wa taifa na kituo mahiri cha utunzaji data

> Tumeanza kutekeleza agizo lako la mwaka jana la kujielekeza kutoa suluhu kwenye sekta ya kilimo ambapo tumeanzisha huduma ya TTCL - HAKIKI itakayoanza mwezi wa Julai,2019 itakayomsaidia mkulima kukagua ubora wa mbegu kupitia simu ya mkononi

> Hivi karibuni tumeanzisha utaratibu kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, kuwatengenezea uwezo wa kuajirika vijana ‘fresh from school’ na vijana hawa takribani 200 wengine wameajiriwa TTCL na wengine wameenda kuajiriwa kwingine


Rais Magufuli
> Tangu Shirikia la TTCL lianze kuendeshwa na wabia wetu, halikuwahi kutoa gawio hata la shilingi tano kwa miaka 15 na lilikuwa likipata hasara ya Tsh bil.15 kwa mwaka, lakini tangu tulirudishe kwenye mikono ya Serikali, shirika hili sasa limeanza kutengeneza faida kubwa

> Tangu kuanza kutoa gawio kwa Serikali mwaka 2016, Shirika hili la TTCL hapa mmetangaza faida ya Bilioni 8

> Naomba niwaambie tu ukweli, TTCL mnapigwa vita kweli kweli, vingine ni vita vya chini ka chini, hata leo kulikuwa na mbinu za kunifanya nisije hapa kuzungumza na nyinyi, kuzindua mfumo nenu na kupokea gawio, lakini nikasema hapana

> Nilikuwa nanong'ona na Waziri, huu Mfuko wa Mawasiliano ni wa nani?, akasema ni wa Serikali, TTCL ni ya nani?, akajibu ni ya Serikali, nikamwambia TTCL hawana minara ya kutosha, kwa nini huo Mfuko usijenge minara na kuikabidhi TTCL ambayo inatoa gawio kwa Serikali

Waziri amesema Mfuko wa Mawasiliano upo chini ya wizara yake, pesa zinachangwa na Watanzania na TTCL ni ya Watanzania, kwa nini inakodi minara ya mashirika mengine na kulipia Sh mil. 700 hadi mil. 800. Kwa nini usitumie pesa hizo kujenga minara ukawapa TTCL moja kwa moja?

> Baada ya mwenzi mmoja nomba niletewe orodha ya viongozi, kuanzia Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi na wengine ambao wanatumia laini za TTCL na sio ziwepo tu bila kutumika, ziwe zimetumika huwezi lipwa mshahara wa Serikali na hutumii mtandao huo, sijamaanisha msitumie mitandao mingine. Kuna wale viongozi wanaolipwa wanaowekewa hela kwenye simu, kwani kuna ubaya gani mkiwaambia kuwa ukitaka kuwekewa hela basi ni TTCL. Ukitaka laini nyingine jiwekee mwenye hela. Lakini pia na wewe Kindamba fanya hivyo kwa Wafanyakazi wako. Ofisi na Mashirika ya Serikali natoa wito kwenu, muanze kutumia line za TTCL, lazima tuthamini vya kwetu

Taasisi zilizojiunga kutumia TTCL, ofisi yangu ya Rais haikutajwa, chama changu CCM hakikutajwa, inaonekana hawa wanaopinga hata kwenye ofisi yangu wamo. Kama wananisikia ninataka ndani ya mwezi mmoja tuanze kutumia simu za TTCL na wizara nyingine

> Mwaka 2016 Serikali iliamua kununua 39% ya hisa zilizokuwa zikimilikiwa na Bharti Airtel kwa Bil.14 ili kuirudisha TTCL Serikalini, hii inaonyesha Serikali haikufanya makosa kwani kabla ya kuirejesha Serikalini hatukuwahi kupata gawio lolote

> Ombi kubwa kwa Watanzania, ni lazima tujali vitu vyetu, nitoe ombi kwa Viongozi wa dini, licha ya kazi kubwa ya kuliombea Taifa na kutuombea kuzishika amri za Mungu basi mtuombee pia kuthamini vitu vya kwetu

> Naamini mwaka huu tutakuwa na ongezeko la Mashirika yanayotoa gawio, Mashirika yasiotoa gawio lazima tutumie sheria kuhakikisha yanatoa au yanaondoka, Msajili wa Hazina simamia hili. Taasisi zote zinazotakiwa kutoa gawio, zifanye hivyo kabla ya mwezi wa saba, haiwezekani hadi Jeshi limetoa gawio wao wasitoe, tena nikiona hata Polisi na Magereza wanatoa gawio, nitafurahi sana

> Msajili wa Hazina hakikisha ifikapo mwezi Julai, Mashirika yote 253 nchini ambayo yamekuwa hayatoi gawio kwa Serikali, yawe yametoa gawio, la sivyo yafungwe. Kama Shirika halitoi gawio kwa sababu linajiendesha kwa hasara basi lifungwe, hakuna maana kuwa na Mashirika yanayofanya kazi kwa hasara, la sivyo watafute namna ya kutoa magawio yao Serikalini

> Idadi ya watu wanatumia simu ni Milioni 42.961 na wanatumia vifurushi ni Milioni 22, jumla ya miamala ya Trilioni 12.9 kwa mwezi hufanyika, kukua kwa sekta ya mawasiliano kunachangia kukua kwa sekta nyingine kama kilimo, ufugaji

> Napenda kuwahimiza Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kufanya bidii kusajili watu vitambulisho vya Taifa ambavyo sasa vinasaidia katika Sekta ya Mawasiliano, jana nilimuona IGP akisajili line yake ya simu huu ni mfano wa kuigwa
 
Ndo maana makampuni ya umma yanakufa..huwezi kufanya kazi kwa ajili ya kuwafurahisha wanasiasa. I very much doubt kwamba TTCL wanatengeneza faida kiasi wanachotaka tuamini. Not to that extent!

Ni kwamba Mkurugenzi na wetandaji wanataka kulinda vibarua vyao.
 
Hilo haliwakilishwi serikalini, linapigwa chinichini kama ile 1.5T.
Tunahitaji CAG akague
 
hahahaah..ndo maana makampuni ya umma yanakufa..huwezi kufanya kazi kwa ajili ya kuwafurahisha wanasiasa. I very much doubt kwamba TTCL wanatengeneza faida kiasi wanachotaka tuamini. Not to that extent!

Ni kwamba Mkurugenzi na wetandaji wanataka kulinda vibarua vyao.
siku nyingine usitumie kiingereza
 
Back
Top Bottom