TTCL na Posta Tanzania jifanyieni tathmini upya

TTCL na Posta Tanzania jifanyieni tathmini upya

whitehorse

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2009
Posts
2,570
Reaction score
4,455
Nimekumbuka zamani. Zamani za kale haya mashirika mawili yalikuwa moja POSTA na SIMU. Ndio jina lake miaka ikaenda ndugu hawa wakatengana. Shirika la SIMU likaendelea vema kabisa ila ndugu yake POSTA alianza kuzeeka upesi. Ujio wa technology ya simu za mikononi ukamfanya na SIMU nae atishie kuzeeka kama ndugu yake lakini akawa mjanja . Ila kwa sasa anazeeka. Japo shirika la POSTA na shirika la SIMU wanaongozwa na vijana ila vijana wenyewe kama siyo competent wao na team zao basi huenda mfumo wa uendeshaji waliokuta hapo Ni mfumo mgando , mitindo ya kale, na mbinu za kizee kabisa.


IMG_4836.JPG


SHIRIKA LA POSTA jiulizeni swali Nani wanatumia sanduku la barua miaka hii? Je ni watanzania wote? Je ni matajiri wote? Je ni wakulima wote? JIULIZENI MTEJA WENU NI NANI NA ANAINGIZA SHILINGI NGAPI KWENYE SHIRIKA HILI JAPO KWA MWAKA MMOJA.

Kwa nini WATEJA wanatuma parcels kwenye mabus ya abiria mfano , JM LUXURY, NDEMBELA, ABOOD na kadhalika? Nyie mlijikwaa wapi ? Huduma mbovu za kuibiwa mizigo ya wateja na kutoshughulikia matatizo wateja waliyoreport mmefikia mahali hamuaminiki mmedharaulika kabisa.

Mizigo imepotea sana mimi nikiwa muhamga wa kupotelewa mzigo mara mbili without any tress kuwa ulipotelea wapi huo mzigo. Mara kadhaa mizigo inachanwa na kupunguzwa lakini no refund wala apology zaidi ya kuzunguushwa na process za kizee hadi mtu una give up. Nikituma mzigo kwenye bus au fuso unafika salama tena ontime labda gari ipate ajali lakini njia tunazotumia tunaziamini kuliko nyie shirika la POSTA.

What are you doing there? Mnataka mzike kabisa hili shirika ama? Kwa nini tajiri mwenye kumiliki bus moja la abiria na dereva wake na kondakta wake ambao hata mikataba yao haieleweki lakini wanafikisha parcel yangu kutoka SONGEA hadi MTWARA bila figisu wala wizi wala upotevu. Lakini nyie shirika la posta lenye watumishi walioajiriwa kwa mikatana na wanaketi kwenye ofisi nzuri za serikali mnashindwa kusimama kama shirika la Umma mkafikisha kifurushi changu salama. Mnalo la kusema.
Masanduku ya barua yako mitaani kwenye majumba ya watu mnawalipa kodi nyie majengo yenu nchi nzima yamejaa masanduku? Mnapewa RUZUKU au hampewi? Hamuoni kama nyie ni wezi tu wa kodi zetu . Kwanini mnashindwa kujiongeza.

Mlianzisha kitu kinaitwa E commerce sijui nini ati mteja anaweza kutrace parcel zake kwenye mtandao nani anaweza sema alishafanya hilo na likawa kweli? Kwanini hamjibandui ngozi kama nyoka anavyofanya? Mnaganda na wizi, huduma chakavu zilizozubaa, wahudumu wazee wako mbele wakali utadhani wako mahakamani whats going on? SHIRIKA LA POSTA amkeni mfanye mabadiliko muanze kuleta faida ya uwepo wenu sio kufanya wizi wa miaka nenda miaka rudi mnaua mashirika mnasababisha vijana wakose ajira wanamiminika toka vyuoni mashirika yamekaa kama ng'omong'omo hayaeleweki. Mmenifika hapa nimeshindwa kuvumilia.

Its about time tujue mnaendesha SHIRIKA LA POSTA kwa faida ama hasara. Nimechoshwa na ulaghai, wizi na uzubavu wa hili shirika ninaamini sehemu ya kodi yangu ninayotozwa huku mtaani inaenda kulisha huu MSUKULE.



IMG_4834.JPG


TTCL nyie mna pesa mnapata kutoka vyanzo kibao ikiwemo minara ya simu pamoja na mkongo (seacom) ila na nyie uwepo wenu kwenye soko ni sawa na kama vile hampo kabisa.

TTCL mnashindwa nini kutumia fursa zilizopo mbele ya macho yenu? TTCL mpo kama hampo wakati wenzenu wanakula chakula nyie mnanawa mikono wakati wanamaliza chakula nyie ndio mnasogea mezani kula mnakuta sahani tupu kabisa.
TTCL nyie ni watoto wa Serikali na mna minara tanzania nzima hii na mmeingia kwenye technology ya digital , how comes bado mnayo mawaya waya ya kazi gani? Je hayana gharama? Je mawaya waya haya yakikatika mnajuaje kwanza , nini kinawasibu hata msibadili hii style?
Mmeganda na nyie kama wazee na makopo ya zamani. Waya karne hii. Watu wamejenga mabondeni wanahitaji kuwa na simu zisiofungamana na miundo mbinu. Kwa mfano muanza kutawanya wirelss extension majumbani muuze bei rahisi mtapata wateja na watu watafurahi kuwa na uhakika wa mawasiliano na majumbani kwao. Mmeacha soko na huu mwanya wazi .

Mkurugenzi kijana sijui hata umetokea wapi maana ghafla tu umekuwa mkurugenzi wa TTCL but akili yako imeishia hapo huna idadi ya wateja wenye furaha ya kurecommend kwa wenzao TTCL ni matatizo sana. Nilikuwa natumia ROUTER yenu kwa internet ofisini kwangu ni pale mwenge tu lakini ikileta shida hadi fundi aje ni zaidi ya siku nne are you serious in business.

Nikawaambia njooni mtoe wire sitaki simu ya wire mimi maana zina matatizo mara unapiga inaita kumbe haiiti wateja wangu wakaanza kunikosa mkaringa kabisa kunihamisha.

Nilijiongeza nikanunua extension mahali nilipochagua mwenyewe na line za mitandao inayojitambua na router yenu nikaipiga teke nilipo sasa nasikilizwa na kusaidiwa on time. Nyie kinawashinda paper work , fundi hadi aje kwa mteja process kama ya kuwekea dhamana mhalifu woooiiii mnadhani mtafika lini mahali tulipo sisi wateja wenu?

TTCL mlikuwa mtandao pekee wa mawasiliano tanzania leo hii hampo huko vijijini wala hamna mpango wowote nani awaonee huruma mwisho mtapobakia na Seacom tu ? Nayo hatuna hakika sana kama itakuwa mikono salama kwa mwenendo huu.


IMG_4837.JPG



RUDI NYUMBANI KUMENOGA really?


Nyie wakurugenzi wa TTCL na POSTA mjifanyie utafiti muache kukaa bure bila kufikirisha vichwa vyenu vema . Mnakuwa mnaua pato la taifa kimya kimya siyo tabia nzuri kabisa
 
Wanipe ukurugenzi wa posta na simu ya zamani waone ntakachokifanya.
 
Posta na hasira nao sana.Parcel ya mwanagu toka Nje imepotelea posta,waizi
 
TTCL hawatumii GSM, sijui nani aliwashauri wasitumie 2G network wakati watumiaji wengi huko vijijini wanatumia simu ndogo ambazo zina GSM network tu na EDGE Kwa ajili ya mtandao.

Sijui nani aliwashauri katika hili, hata hiyo T-Pesa unamtumia vipi mtu wa kijijini ambae anamiliki Nokia tochi? Au hawataki watu wa vijijini watumie line za TTCL?

It's lame and stupid...
 
Posta wanatakiwa wabadili mode of operation na kufocus upya market segment
CEO na Management lazma wawe vibrant

TTCL inatakiwa kuamshwa na kupewa target

Rais Magufuli anahitajka kuamua CEO wote wa Public Enterprises wawe kwa mikataba

Hii ya permanent positions haifai kabisa
Watu wanajisahau na kukalia kusubr posho na salary

Inasikitisha sana
 
Watumishi wengi wa hayo mashirika ni wazee,hata hao unaosema vijana nao ni wazeee tu ndo mana yanaendeshwa kizee


yes! hta hao vijana ni wazee kifikra, unakuta toka wamalize chuo hawajawahi kusoma vitabu vya logistic hta kimoja au kufuatilia wenzao ktk nchi zilizoendelea wanafanyeje!
 
Watumishi wengi wa hayo mashirika ni wazee,hata hao unaosema vijana nao ni wazeee tu ndo mana yanaendeshwa kizee

Wa TTCL ni kijana kabisa huyu hapa

IMG_4848.JPG



Wa Shirika la Posta pia ni huyu kijana pia

IMG_4849.JPG



Ila wafanyakazi wenzao wa chini yao ni 90% wazee. Wanaamkiana SHIKAMOO tupu kuanzia getini watapata wapi ujasiri wa kuwa nyoosha wanapokosea [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Posta wanatakiwa wabadili mode of operation na kufocus upya market segment
CEO na Management lazma wawe vibrant

TTCL inatakiwa kuamshwa na kupewa target

Rais Magufuli anahitajka kuamua CEO wote wa Public Enterprises wawe kwa mikataba

Hii ya permanent positions haifai kabisa
Watu wanajisahau na kukalia kusubr posho na salary

Inasikitisha sana

Ovyo sana mambo ya kufanya kazi bila target kwenye dunia hii ya ushindani [emoji29][emoji29][emoji29][emoji29]
 
Wa TTCL ni kijana kabisa huyu hapa

View attachment 791717


Wa Shirika la Posta pia ni huyu kijana pia

View attachment 791718


Ila wafanyakazi wenzao wa chini yao ni 90% wazee. Wanaamkiana SHIKAMOO tupu kuanzia getini wataajibishana vipi wanapokosea [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

kwa upande wa shirika la posta now kuna potential kubwa mno ya usafirishaji wa vifurushi,...hii km itapata muongozo mzuri inaweza kuwa na turn over ya hatari

lakini ndyo ivo wahusika wamelala usingizi wa pono wanasubiri sekta binafsi zianze wakishatawala soko wao ndyo waje na figisu kibao kuwakwamisha
 
Posta wanatakiwa wabadili mode of operation na kufocus upya market segment
CEO na Management lazma wawe vibrant

TTCL inatakiwa kuamshwa na kupewa target

Rais Magufuli anahitajka kuamua CEO wote wa Public Enterprises wawe kwa mikataba

Hii ya permanent positions haifai kabisa
Watu wanajisahau na kukalia kusubr posho na salary

Inasikitisha sana

Zaidi ya hayo, haya mashirika yanahitaji damu mpya kuanzia bodi ya wakurugenzi mpaka manejimenti ya shirika.
 
Back
Top Bottom