Uongozi wa UKAWA 2015 utakuwa hivi

Uongozi wa UKAWA 2015 utakuwa hivi

Mkuu itabidi hata hapa jf,ipangwe timu ya cdm inayopambana dhidi propaganda chafu dhidi ya chama chetu toka kwa maadui zetu na vibaraka wao.

Ni kweli mkuu tena kila mchezaji atajwe na alikotoka ili kuondoa dhana chafu kuwa chama pendwa na cha kikabila
 
maprofesa ,madokta na wachungaji wote tia maji tia maji tu sijaona timu apo
 
Paulina gekul

Hili ni jembe la ukweli. Mwakani vichwa vipya vinaingia bungeni. Kaeni mkao wa kula. Kuna jamaa anagombea morogoro mjini, mchambuzi wa star tv jina limenitoka, ni noma.. Hata tundu lissu hatii maguu pale.
 
Kuna kifaa kimeingia jimbo la ludewa kinaitwa Prof.Batromeo mkinga ukipenda muite Msambichaka hatareeeee
 
List naona imejaa wana kwaya watupu.
 
Ndugu wanajamii,
UKAWA wakiingia Magogoni mwaka 2015, uongozi wa juu wa Serikali utakuwa kama ifuatavyo:

Rais: Dr Wilbrod Peter Slaa.

Makamu wa Rais: Profesa Ibrahim Haruna Lipumba.

Waziri Mkuu: Hon James Francis Mbatia.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG): Hon Tundu Antipas Mugway Lissu.

Naibu AG: Profesa Abdallah Safari.

Mkuu wa Usalama wa Taifa: Hon Mabere Nyaucho Marando.

Naibu: Hon Wilfred Muganyizi Lwakatare.

Waziri wa Mambo ya Ndani: Godbless Jonathan Lema.

Gavana wa Benki kuu: Juma Duni Haji.

Waziri wa Michezo na Utamaduni: Hon Joseph Michael Mbilinyi (Sugu).

Hii baadhi ya safu ya kikosi cha MAENDELEO cha UKAWA baada ya kuingia magogoni mwaka ujao. Mnakaribishwa kutoa maoni yenu ili kukiboresha (pale itakapobidi). Kikosi hiki ndio tiba ya maendeleo ya watanzania yaliyokwamishwa na CCM kwa zaidi ya nusu karne sasa.

WanaUKAWA toeni maoni yenu yatakayosaidia kuboresha jeshi hili la ukombozi. WanaCCM naweza kuchangia ila msitumie jazba, kama kawaida yenu.

Nawasilisha.

:israel:

Umedhihirisha kwa kiasi gani huijui katiba ya nchi. Kwa mujibu wa katiba rais akitoka bara basi makamu hutoka visiwani (and vice versa). Kama kitu hujui usiandike tu kufurahisha watu
 
khaaaa,lipumba amekuwa mpemba!embu ipeni thamani elimu yenu japo kwa kutumia vizuri vichwa vyenu kufikiri.
 
Mkuu umechemka sana. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hairuhusu Rais na Makamo wa Urais kutoka upande mmoja wa Muunganio kama Rais atatoka Bara basi makamo wa Urais atatoka Zanzibar na Rais akitoka Zanzibar basi makamo atoke Bara. Tujaribu kufuatilia katiba kwa makini ili tusifanane na akili za maccm
 
Rais Dr Slaa
VIP Prof Safari

Hii ndiyo ipo toka siku nyingi!Lipumba ni Mtanganyika katiba itamkataa tpaul
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom