Guus
JF-Expert Member
- Jul 16, 2013
- 1,167
- 907
Kitu pekee ninachokipata kutoka katika bandiko lako ni kuwa mfumo mzima wa elimu yetu ni hohehahe, uko taabani na haujielewi. Umekitaja UDSM lakini tatizo lipo vyuo vyote vya umma (nataja umma maana sina uzoefu na vyuo binafsi).
Wanafunzi wanaomaliza katika vyuo vyetu (kadiri miaka inavyozidi kwenda) wanazidi kuwa watupu vichwani.
Wacha niweke mambo machache ya kuonesha tulipo sasa (kwa uzoefu wa vyuo vinne; UDSM, UDOM, SUA na Mzumbe).
1. Mhadhiri asipoingia darasani wanafunzi hufurahi
2. Mhadhiri akikazia wanafunzi waelewe (mfano mhadhiri akitumia seminar classes vilivyo huwa anachukiwa na wanafunzi. Na inaweza kwenda mbali kwa wanafunzi wa sasa wakakutengenezea zengwe. Ikumbukwe lecture classes mhadhiri huzitumia kutoa mhadhara wa somo, na seminars kama kupata mrejesho kutoka kwa mwanafunzi).
3. Mhadhiri anayerahisisha mambo "laissez-faire", yaani hatoi kazi kwa wanafunzi, anagawa marks hata pasipo usahihi, ndiye hupendwa na wanafunzi.
4. Ni kosa mwanafunzi kupata marks kidogo hata kama mhadhiri katumia vipindi vyote kwa usahihi. Wanafunzi wa sasa "usiingie darasani lakini toa marks"
Kiufupi elimu ya sasa ni ya marks zaidi kuliko uelewa/maarifa. Nina mifano mingi ya wahadhiri katika vyuo tofauti kuingizwa vikaangoni kutokana na zengwe zinazotengenezwa na wanafunzi.
Nimalizie kwa kusema, elimu ya dunia ya sasa ni maarifa. Inatakiwa hadi mwanafunzi anafika chuoni awe amekwishajua anachotaka kufanya maishani, ajue ni nini anadhani anakikosa (atakapoenda kuanza kukifanya hicho anachotaka) na anadhani kwenda chuo kitasaidia yeye kukipata.
Elimu ya msingi na sekondari inatakiwa iwaandae wanafunzi kwenye hili (tubadili mitaala, na sio kuikumbatia mitaala ya zamani wakati Dunia inazunguuka). Inatia ukakasi sana, hata humu JF huwa naona, mtu kamaliza sekondari anaomba ushauri akasome nini chuoni.