sumbai
JF-Expert Member
- Jun 16, 2014
- 18,517
- 41,756
Well said brother.
English medium sio mkombozi wa tatizo kabisaa ila ni mtaala wetu ndio tatizo.
Sent using Jamii Forums mobile app
English medium sio mkombozi wa tatizo kabisaa ila ni mtaala wetu ndio tatizo.
Mimi napenda kuchangia kidogo mtoa uzi.Mimi ni mwlm tena wa shule ya msingi.Nilianza na ngazi ya chert ila Leo natafuta shahada ya pili.Nimeingia kazini 2010.
Vyuo vikuu tusivilaumu sana kwakuwa vinapata product ambayo imetoka hapa chini.Msingi ambao ndoo elimu ya msingi ni mbovu kupitiliza .Siku hizi wanafunzi wakishafika darasa la saba wanafundishwa past pepers tu mpaka wanafanya mtihani lengo afaulu la saba.
Leo hii mwlm anaingia darasani na kitabu anafundisha kwa kuongea yeye mwanzo mwisho.Akimaliza natoa maswali mwanafunzi anafanya ,atakae kosa atamfnyia masahihisho na kuendelea na mada nyingne.Hakuna kumtengenezea mwanafunzi udadisi,uchunguzi wala ubunifu wowote.
Siku hizi waalimu ndoo wamechoka kabisaa wanawavanyia hadi mtihani wanafunzi ili mradi limtoke asije sumhuliwa kwann hawajafaulu ,mara uandike barua.Ndivyo wakubwa wa ngazi za juu wanavyo taka ,ufaulishe asilimia mia haijalishi umepatikanaje.
Hivyo hivyo shule za English midium,nao wanawakaririsha watoto.Hawana mbinu za kuwafanya watoto wadadisi,wawe wabunifu wala wawe wavumbuzi.Kinacho wasaidia hapo ni lugha na kukrishwa kwa wingi.
Wakitoka hapo wanaenda sekondary huko lugha kingereza na kwakuwa wanamsingi wa ligha wataweza kukariirishwa na kufaulu na jatimae watafika chuo kikuu na hizo one au two.
Tanzania mwanafunzi anae faulu vizuri kidato cha nne na sita akaenda UDSM anacho mzidi mwenzake aliepata 3 au 2 ni kuwa yeye ana uwezo mzuri wa kukariri na kukumbuka kuviandika kwenye karatasi tu ,hana kingine chochote zaidi ya hapo.
Tutazidi kupiga kelele na kuongea sana but mkombozi hayupo.Serikali lazima ikubali ije na mfumo mzima wa utoaji wa elimu utakao tusogeza miaka angalau thelathini mbele sio huu mfumo tulio nao.
Wanachosema serikali wanasema hawana pesa lakini najiuliza si bora wasigharamikie hiyo miradi mikibwa baadala yake wagharamikie elimu iwe bora?
Nisamehe nimeandika marefu sana ila natamani watanzania wajue na waungane kwa pamoja kuishinikiza serikali ibadili huufumo ili watoto wao wapate elimu bora.
Mimi na babaangu mdogo watoto wake wote watatu wamesoma kuanzia nasury mpaka kidato cha sita Tusiime. Chuo kikuu UDSM wote wapo kwake ,alifikiria gharama alioitumia ni kubwa sana na pesa ya kuwa pa mitaji hana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app