Uongozi Chuo Kikuu Dar Es Salaam una matatizo

Mtyela Kasanda

JF-Expert Member
Oct 13, 2018
554
818
- Miaka inaenda tu na kila mwaka wanachukua vijana wetu wanaojiweza sekondari lakini wanaturudishia uozo. Unakuta mtoto alikua ana akili kweli lakini akimaliza chuo anaanza kuongea pumba, ooh mara " nataka nianzishe kampuni yangu ya software" " nataka nitoe semina ya madini", " nataka niandae semina ya ujasiriamali", ushenzi na uzuzu tu.

- Wakati sisi tunawapeleka watoto pale tunasema mtoto anaenda mlimani, atatoka na kitu pale, kumbe anaenda kutoka na maongezi. Ndio maana hata watu wa taaluma kubwa za sayansi kutoka UDSM wanaishia kuwa wanasiasa. Chuo kimejaa porojo mno.

- Hivi unajua Mwijaku alikua mwanafunzi wa UDSM? that fat fuk should've been the one helping our film industry but he is dying with it. Yani chuo kinachoaminiwa na watanzania wote kinashindwa kuzalisha hata waigizaji wazuri. UDSM ndipo walipotakiwa kutoka first grade Creative writers lakini asilimia 98 ya vitabu vyote vipya Tanzania vinahusu ujasiriamali au ni catalogue za bidhaa mbalimbali. Upumbavu juu ya upumbavu.

- Wazazi hatupendi vijana wetu wawe wanasiasa, tunapenda vijana wetu wawe na taaluma zinazoeleweka.

- UDSM imejaa misifa tu na hamna la maana linalofanyika.

- Chuo kikuu kikubwa kama kile hamna independent course ya Robotics, huwezi kutengeneza lolote miaka hii ya sasa hivi bila kuwa na elimu ya Robotics. Lakini UDSM hamna.

- Kwanini tusichukue waalimu wa nchi za nje walioendelea kielimu kuja kutusaidia kufundisha? ( nchi kama Ujerumani, Uingereza, Norway na Marekani). Tumejaza wasakatonge kama wakufunzi pale badala ya wataalamu. Mtoto anatoka CoICT hata basic commands za Linux hajui.

- Muda umefika wa serikali ya wanafunzi kukomalia taaluma inayotolewa pale, sio kila siku wanafunzi wanagombana na serikali kuu, tafuteni elimu inayoeleweka. Ukiwa na Cheti cha Geology kutoka UDSM halafu huna ajira wewe maisha yako ndio yameisha hivyo lakini haitakiwi kuwa hivyo. Wanafunzi lilieni elimu, mnatoka pale na uwezo mdogo tofauti na matarajio.

Mpaka leo hatuna kampuni binafsi ya mtandao wa simu ya kitanzania, zote zilizopo ni subsidiary ya kampuni za nje, na UDSM ipo tu miaka inaenda. Amkeni serikali ya wanafunzi, chuo kutafute waalimu competent na mazingira yawe wezeshi kusaidia kua na utaalamu wa hali ya juu kabisa kwa kozi husika.
 
Tatizo linaanzia kwa hao wakufunzi wenyewe. Mwanafunzi unatoka unakokaa unajua una lecture ya course fulani, unafika darasani saa nzima lecturer hajafika, kumbe anapiga deal zake huko. Wakufunzi wengi wamejikita katika kupambana na maisha yao na kusahau lengo la uwepo wao katika eneo la kazi. Tena na hivi wanavyopewaga videal vingi vingi eti kisa wanaonekana wataalamu. Nakumbuka Kuna course

Nakumbuka kuna course moja alikuwa anafundisha prof mmoja hivi. Tangu semister inaanza mpaka inaisha kaja Mara 2 tu, the rest anamuachia msaidizi wake ambaye anaishia tu kuwasomea notes. Hapo unategemea mwanafunzi anatoka na nini ?
 
Jiwe limerushwa gizani. Wenye maamuzi wanafanya kama vile hawaoni ukweli.!!

Mfumo kuanzia elimu ya msingi ni shida tupu,wao wanawapeleka watoto wao katika za 'english medium',huku wakifahamu kuwa kila mwananchi anataka elimu bora kwa mtoto wake.

Tujiulize,ni gharama kiasi gani inahitajika ili kubadilisha mfumo wa elimu ya msingi kuwa 'english medium' .
Tena,tujiulize kwanini shule za 'english medium' zinazidi kuongezeka.

Majibu ya maswali hapo juu,ni kwamba bado wenye maamuzi hawajawa tayari kutatua 'KIU YA MWANANCHI' katika kuwapatia watoto elimu yenye usawa katika jamii.
Ngazi ya vyuo,bado tumeendelea kukariri mifùmo iliyopitwa na wakati,na hivyo kuathiri ubora na umahiri wa mwanafunzi anaporudi kuishi na jamii.

Jamii inamuona mwanafunzi hana msaada kwa jamii
 
Nilisoma udsm na ulo ongea ni kweli kabisa. Ila naona sio udsm pekeee ila ni ugonjwa wa vyuo vyote vya Tanzania sema umelenga Udsm kwani ndo tulipoweka imani ni chuo bora kwa Tz.

Katika vitu nilivyo laumu ni kusoma hadi na maliza hakuna mahali tulipo hitajika kusoma ujasiriamali au kompyuta japo ni Mwalimu wa Sayansi.

Laiti sio kujiongeza kwangu ningetoka mtupu kwenye hayo maswala. Yaaani Elimu yetu imeshindwa kufikiria mbele miaka kumi ijao kuwa dunia itakuwa wapi. Kama umesoma shule za serikali hadi unaingia chuo Kikuu niseme tuu ukweli una hasara sehemu flani katika Maisha hasa kwenye zama hizi. Maana utaambulia kuwa na hiyo Elimu ya makaratasi na vyeti.

Na ujinga mwingine ni wanafunzi wengi kujiskia hasa kipindi wako chuo ,Wanaona kama ndo maisha yameisha hata hii ni kwa wanachuo wote tuu wakishafika chuo duuuh kuna ka kiburi flani hivi kwa wale hawajasoma au kufika na wakiamini maisha ni simple wakishamaliza.

Nilikataa huoo ujinga hasa nilipo kosaga mkopo nikajiongeza ili niweze kujisomesha.. Utamkuta mwanafunzi kavaa likamba la Udsm Student hadi kariakoo ilimradi mumjue anasoma wapi.
 
Jiwe limerushwa gizani.Wenye maamuzi wanafanya kama vile hawaoni ukweli.!!

Mfumo kuanzia elimu ya msingi ni shida tupu,wao wanawapeleka watoto wao katika za 'english medium',huku wakifahamu kuwa kila mwananchi anataka elimu bora kwa mtoto wake.

Tujiulize,ni gharama kiasi gani inahitajika ili kubadilisha mfumo wa elimu ya msingi kuwa 'english medium' .
Tena,tujiulize kwanini shule za 'english medium' zinazidi kuongezeka.

Majibu ya maswali hapo juu,ni kwamba bado wenye maamuzi hawajawa tayari kutatua 'KIU YA MWANANCHI' katika kuwapatia watoto elimu yenye usawa katika jamii.
Ngazi ya vyuo,bado tumeendelea kukariri mifùmo iliyopitwa na wakati,na hivyo kuathiri ubora na umahiri wa mwanafunzi anaporudi kuishi na jamii.
Jamii inamuona mwanafunzi hana msaada kwa jamii
Mkuu tapishana nawewe kidogo. Shule za english medium sio kwamba zinatengeneza products za kjja kujiajri ila wao huwa wanafocus zaidi katika kupata good examination results good caring of pupils basi.

Tatizo lipo kwenye mtaala wetu.

Tatizo lipo pale pale. Hata hao wa english medium mtaan wana hangaika tuu kujiajiri awawez

Sent using Jamii Forums mobile app
 
54 Reactions
Reply
Back
Top Bottom