Uongozi Chuo Kikuu Dar Es Salaam una matatizo

Uongozi Chuo Kikuu Dar Es Salaam una matatizo

Jiwe limerushwa gizani. Wenye maamuzi wanafanya kama vile hawaoni ukweli.!!

Mfumo kuanzia elimu ya msingi ni shida tupu,wao wanawapeleka watoto wao katika za 'english medium',huku wakifahamu kuwa kila mwananchi anataka elimu bora kwa mtoto wake.

Tujiulize,ni gharama kiasi gani inahitajika ili kubadilisha mfumo wa elimu ya msingi kuwa 'english medium' .
Tena,tujiulize kwanini shule za 'english medium' zinazidi kuongezeka.

Majibu ya maswali hapo juu,ni kwamba bado wenye maamuzi hawajawa tayari kutatua 'KIU YA MWANANCHI' katika kuwapatia watoto elimu yenye usawa katika jamii.
Ngazi ya vyuo,bado tumeendelea kukariri mifùmo iliyopitwa na wakati,na hivyo kuathiri ubora na umahiri wa mwanafunzi anaporudi kuishi na jamii.

Jamii inamuona mwanafunzi hana msaada kwa jamii
Zinaongezeka kwakuwa huku kwa wadanganyika wanaamini kuongea kiingereza ndiyo Elimu Mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la wahitimu wa vyuo vikuu vyote nchini.

Ukitaka kujua hawana kitu kichwani,ni pale wanapojisifia na sifa ya degrii tu.

Wengine wasiosoma watasifiwa hadi na Rais wamefua Umeme wa maji elimu yao ikiwa darasa la sana tu.Wengine wameamzisha kampuni ya uchapaji wa magazeti wakiwa hawana elimu.
Wengine wamejinadi kutengeneza sabuni maarufu za dawa, formula ya kutibu vidonda vya tumbo na dawa nyingine nyingi.

Wahitimu wa vyuo vikuu kazi yao ni kujitengenezea mazingira ya kujilipa pesa ya makusanyo ya kodi kupitia vyeo mbali mbali bila kuwa na masuluhisho ya matatizo ya watanzania.

Ukiona mleta mada ni sawa na nyani anacheka kun.du la nyani wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unaonekana huelewi tatizo ni nini hasa unaishia kulaumu Chuo ambacho sidhani hata kama unakielewa na unauelewa mchango wake siyo tu kwa Tanzania ila katika ukanda wa Africa.
Unaonekana kabisa huna uwezo wa kuchuja hisia na hoja unajiandikiaandikia tu.Punguza povu njoo tena.
 
Nilisoma udsm na ulo ongea ni kweli kabisa. Ila naona sio udsm pekeee ila ni ugonjwa wa vyuo vyote vya Tanzania sema umelenga Udsm kwani ndo tulipoweka imani ni chuo bora kwa Tz.

Katika vitu nilivyo laumu ni kusoma hadi na maliza hakuna mahali tulipo hitajika kusoma ujasiriamali au kompyuta japo ni Mwalimu wa Sayansi.

Laiti sio kujiongeza kwangu ningetoka mtupu kwenye hayo maswala. Yaaani Elimu yetu imeshindwa kufikiria mbele miaka kumi ijao kuwa dunia itakuwa wapi. Kama umesoma shule za serikali hadi unaingia chuo Kikuu niseme tuu ukweli una hasara sehemu flani katika Maisha hasa kwenye zama hizi. Maana utaambulia kuwa na hiyo Elimu ya makaratasi na vyeti.

Na ujinga mwingine ni wanafunzi wengi kujiskia hasa kipindi wako chuo ,Wanaona kama ndo maisha yameisha hata hii ni kwa wanachuo wote tuu wakishafika chuo duuuh kuna ka kiburi flani hivi kwa wale hawajasoma au kufika na wakiamini maisha ni simple wakishamaliza.

Nilikataa huoo ujinga hasa nilipo kosaga mkopo nikajiongeza ili niweze kujisomesha.. Utamkuta mwanafunzi kavaa likamba la Udsm Student hadi kariakoo ilimradi mumjue anasoma wapi.
aisee nilikutana na muhitimu wa Hapo hajui hata Basics za Microsoft word..

nikabaki tu kujiuliza aliandaaje kazi zake!
 
Umeongea ukweli mtupu hali ya vyuo ipo hoi.
Lakini utailaumu UDSM bure tu, tatizo linaanzia elimu ya msingi. Watoto wakiwa wadogo hawawekewi msingi mzuri wa kudadisi na kuwa wabunifu mwanzoni kabisa wa safari yao ya elimu. Hata hao mnaowasifia wamesoma English Medium hakuna jipya kule wanameza tu notes na kukaririshwa vitu kibao ilimradi wafaulu mitihani na sio iliwajifunze namna ya kujifunza.
Kama kuna mtu amewahi kusoma mtaala tofauti na huu wa Kitanzania hasa hasa level ya msingi utanielewa ninacho ongelea. Kule mtoto akiwa mdogo anafundishwa namna ya kujifunza, anafundishwa namna ya kufanya brainstorming tangia akiwa standard 3 ili ajifunze mapema namna ya kujiongeza na kuweza kupata mawazo mapya.
Ukikosea kwenye msingi hata aende wapi hata afaulu vipi mtarudi tu kulalamika kuwa watu hawana ubunifu.
Mfano wa haraka ni baadhi ya mawaziri na viongozi waliosoma vyuo vikuu vya nje vikubwa tu lakini bado tunawalalamikia kwamba upeo wao ni mdogo. Sababu ni kwamba msingi wao ni mbovu.
Kurekebisha elimu ya Tanzania ni kufumua kabisa elimu ya msingi ili iwe ya msingi kweli na siyo kuwamezesha watoto wadogo notes na concepts za kutosha nambazo kimsingi hazimsaidai chochote kwa huo umri sana sana zinamdumaza fikra mpaka kaburini.
Ni kweli vyuo vyetu vinashida kubwa sana lakini wanaokwenda pale wangekuwa tayari wana msingi mzuri wangeweza kuzikabili hizi changamoto na kuzishinda.

UDSM inalalamikiwa kwasababu ndio chuo Mama, msingi ulitakiwa ujengwe na wahitimu wa mwanzo kabisa ambao wengi wao wametoka UDSM.

Angalia hata wenye kufanya maamuzi katika sehemu mbalimbali nchi hii ni wahitimu wa UDSM, Asilimia kubwa ya walimu wa vyuo vingine ni wahitimu wa UDSM.
 
Hapa nitashauri kama mpita njia
1. Elimu ya chuo kikuu ni pana sana, mwanachuo hapaswi kutegemea madesa ya darasani pekee. Mkufunzi akishadodosa kidogo ni jukumu lako kwenda deep kupitia vitabu vya maktaba na tutorials nyingine mitandaoni.
WANACHUO MSIPOTEZE MUDA KWENYE KUTAZAMA SERIES NA PORNO.

2. Si ajabu kumkuta mwanachuo wa mwaka wa mwisho anaesomea ualimu hana notes za kufundishia, kila alipokuwa akienda field anabeba daftari lake la O'level alilosomea miaka mitano iliyopita anaenda kuwafundishia vijana, yaani hana muda wa kuboresha kile cha zamani kwa kuzingatia kuwa sasa ameelimika. Hili haliitaji mkufunzi akwambie, linahitaji utashi wa mtu mmoja mmoja, kama huna, huna.

3. Si ajabu kumkuta mwanachuo anaesomea engineering, IT, electronics n.k katika laptop yake ana software nyingi za games kuliko za fani yake. Unamuuliza mwanachuo wa mwaka wa pili anaengia watatu wa fani ya IT kama anajua kutumia framework yoyote katika kutengeneza tovuti, anakuuliza framework ndio nn?
Huyu ni mwanachuo ambae akishafundishwa kile cha darasani ndio kamaliza hatoki nje ya box. Hajihangaishi kujua duniani wataalamu wa fani yake wanatatua changamoto kwa mtindo upi wa kisasa.

4. Maisha magumu ya wanachuo nayo pia yanachangia kupunguza umakini. Si ajabu kumkuta mwanachuo hana laptop, hana smartphone yupo yupo tu na madesa yake, unategemea nini hapo, mkopo wenye asilimia 30, ndugu wanamtegemea, bata hapohapo, aishi kichuochuo, halafu unategemea awe mbunifu, aaa wapi.

5. Chuo kuna katabia kakuaanda project mwaka wa mwisho, project ziwe kila semester, japo ndogondogo, ili mwaka wa mwisho atutengenezee kilicho bora kabisa. Hii system ya sasa inawafanya wazubae zubae sana.

Mpita njia nipo kwenye kimbweta saa hii, nitashuka cafteria ya yombo muda si mrefu niende zangu changanyikeni.
Ciao.
Kuna la kujifunza kupitia hoja zako hizi,
Binafsi nikupongeze kwa mchango mzuri usiojikita kwenye kurusha tuu lawama na kusemasema Bali umetoa nini kifanyike[emoji122][emoji122][emoji122]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Welcome to Open Discussion Forums -- The Home of Critical Thinkers!, a completely free knowledge & information exchange platform! Register or Log in, choose your favorite forum and start posting or replying to topics. Help others to learn by sharing with them what you have!

For more details, see Welcome To Open Discussion Forums

Open Discussion Forums is steadily gaining its due attention, in 2018, Open Discussion Forums was ranked number 32 in the 2018 list of Africa’s Movers and Shakers in Corporate Online Learning, see also Africa’s Movers and Shakers in Corporate Online Learning 2018
 
Binafsi namna nzuri yakukabiliana na changamoto zote hizi Kuna majukumu yakufanya upande wa serikali pia vyuo Kama taasisi;-
-Serikali inabidi itoe dira kamili inayojipambanua kwanini waliochaguliwa wafanye bidii nawahakikishe wanarudi na utaalamu isiache tuu watu wajiendeee Kuna course za miaka mingi yamkini ata kwa Sasa si kipaumbele Tena lakni hawasemi

Mfano Kama jinsi wanavyo 'highlight" priority course wakati wakuwapatia vijana mkopo ndivyo inavyopaswa kufanyika hata wakati wakuruhusu kwenda kusomea taaluma hizo. Hii itatoa nguvu kwa wasomi wetu wajione Kama ni watoto walipewa chakula Cha familia wale wakatafute waje wasaidie familia

-Kwa upande wa Vyou Kama taasisi iko haja yakutafuta namna nzuri zaidi yakupata wakufunzi nakuondoa nadharia ya kujikita kutizama G.P.A

Wengi tunaona/kusikia namna ambavyo GPA inatafutwa huko vyuoni pasipo kuzingatia ata uhalali wake

Hili linachangia kiasi kikubwa kuwa na wakufunzi hao waliopo

Ata hao maPROFESA tunaofikiri yamkini ni msaada waliowengi ni waandishi tuu nawala si ni wabobezi waliogundua vitu hivyo kimsingi tukitupia kwa hawa Bado hatujapata namna yakuzuia hili lakutopata matokeo tuliyoyatarajia


Kimsingi natambua tume za ukaguzi zipo nazinafanya kazi zake,lakini iko haja yakupata watu waadilifu kwelkwel katika TUME hizi ......vyuo tunavyovizungumzia vitupe WANASAYANSI maabara zao zinaupungufu wa hali ya juu saanaa

Ili kufanikisha adhima yakupata wataalamu bora tume zilizoundwa ziwe na watu waadilifu si watu wakuhongwahongwa .....chuo inatoa course ambayo kimsingi mahtaj yake hajakamilika si kusimamisha udahili tuu Bali nikukifungia kabisa kutokana na kukosa uaminifu


-Kwa msaada wa serikali iko haja yakuanda MIND SET ya hawa vijana wanaoenda kuanza chuo watambua kule wanaenda kusoma taaluma walizochagua na kuchaguliwa nasiivinginevyo

" Waziri wa Elimu Mh Joyce Ndalichako alisikika akisema pesa tunazowapa wanafunzi nikama jinsi zilivyo ainishwa nasiivinginevyo ...Cha ajabu wengi wenu wanatumia pesa hizo kurembea maghetto na kufanya matumizi ya tofauti kabisa''


Zaidi sana Sanaa ni Serikali kuweka mfumo mzuri zaidi yakuwawezesha watahiniwa kunufanika na taaluma zao

Kama nikuwatafutia ajira Kama wanavyofanya sasa kupitia Taasisi yake chini ya waziri mkuu

Ama kuwawezesha kujiajiri kupitia taaluma zao kwa kuwapa mawazo au msaada mbalimbali Kama mtaji
Na hii serikali imefanya hasa kwa kada za kilimo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
- Miaka inaenda tu na kila mwaka wanachukua vijana wetu wanaojiweza sekondari lakini wanaturudishia uozo. Unakuta mtoto alikua ana akili kweli lakini akimaliza chuo anaanza kuongea pumba, ooh mara " nataka nianzishe kampuni yangu ya software" " nataka nitoe semina ya madini", " nataka niandae semina ya ujasiriamali", ushenzi na uzuzu tu.

- Wakati sisi tunawapeleka watoto pale tunasema mtoto anaenda mlimani, atatoka na kitu pale, kumbe anaenda kutoka na maongezi. Ndio maana hata watu wa taaluma kubwa za sayansi kutoka UDSM wanaishia kuwa wanasiasa. Chuo kimejaa porojo mno.

- Hivi unajua Mwijaku alikua mwanafunzi wa UDSM? that fat fuk should've been the one helping our film industry but he is dying with it. Yani chuo kinachoaminiwa na watanzania wote kinashindwa kuzalisha hata waigizaji wazuri. UDSM ndipo walipotakiwa kutoka first grade Creative writers lakini asilimia 98 ya vitabu vyote vipya Tanzania vinahusu ujasiriamali au ni catalogue za bidhaa mbalimbali. Upumbavu juu ya upumbavu.

- Wazazi hatupendi vijana wetu wawe wanasiasa, tunapenda vijana wetu wawe na taaluma zinazoeleweka.

- UDSM imejaa misifa tu na hamna la maana linalofanyika.

- Chuo kikuu kikubwa kama kile hamna independent course ya Robotics, huwezi kutengeneza lolote miaka hii ya sasa hivi bila kuwa na elimu ya Robotics. Lakini UDSM hamna.

- Kwanini tusichukue waalimu wa nchi za nje walioendelea kielimu kuja kutusaidia kufundisha? ( nchi kama Ujerumani, Uingereza, Norway na Marekani). Tumejaza wasakatonge kama wakufunzi pale badala ya wataalamu. Mtoto anatoka CoICT hata basic commands za Linux hajui.

- Muda umefika wa serikali ya wanafunzi kukomalia taaluma inayotolewa pale, sio kila siku wanafunzi wanagombana na serikali kuu, tafuteni elimu inayoeleweka. Ukiwa na Cheti cha Geology kutoka UDSM halafu huna ajira wewe maisha yako ndio yameisha hivyo lakini haitakiwi kuwa hivyo. Wanafunzi lilieni elimu, mnatoka pale na uwezo mdogo tofauti na matarajio.

Mpaka leo hatuna kampuni binafsi ya mtandao wa simu ya kitanzania, zote zilizopo ni subsidiary ya kampuni za nje, na UDSM ipo tu miaka inaenda. Amkeni serikali ya wanafunzi, chuo kutafute waalimu competent na mazingira yawe wezeshi kusaidia kua na utaalamu wa hali ya juu kabisa kwa kozi husika.
Looks like you love Linux OSses: Linux and Unix Based Operating Systems
 
Kuna la kujifunza kupitia hoja zako hizi,
Binafsi nikupongeze kwa mchango mzuri usiojikita kwenye kurusha tuu lawama na kusemasema Bali umetoa nini kifanyike[emoji122][emoji122][emoji122]

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana. nami nikushukuru kwa kupitia mchango wangu na kunijulisha hili.
 
Back
Top Bottom