Commander In Chief
JF-Expert Member
- May 12, 2019
- 315
- 718
Certified commentNilisoma udsm na ulo ongea ni kweli kabisa. Ila naona sio udsm pekeee ila ni ugonjwa wa vyuo vyote vya Tanzania sema umelenga Udsm kwani ndo tulipoweka imani ni chuo bora kwa Tz.
Katika vitu nilivyo laumu ni kusoma hadi na maliza hakuna mahali tulipo hitajika kusoma ujasiriamali au kompyuta japo ni Mwalimu wa Sayansi.
Laiti sio kujiongeza kwangu ningetoka mtupu kwenye hayo maswala. Yaaani Elimu yetu imeshindwa kufikiria mbele miaka kumi ijao kuwa dunia itakuwa wapi. Kama umesoma shule za serikali hadi unaingia chuo Kikuu niseme tuu ukweli una hasara sehemu flani katika Maisha hasa kwenye zama hizi. Maana utaambulia kuwa na hiyo Elimu ya makaratasi na vyeti.
Na ujinga mwingine ni wanafunzi wengi kujiskia hasa kipindi wako chuo ,Wanaona kama ndo maisha yameisha hata hii ni kwa wanachuo wote tuu wakishafika chuo duuuh kuna ka kiburi flani hivi kwa wale hawajasoma au kufika na wakiamini maisha ni simple wakishamaliza.
Nilikataa huoo ujinga hasa nilipo kosaga mkopo nikajiongeza ili niweze kujisomesha.. Utamkuta mwanafunzi kavaa likamba la Udsm Student hadi kariakoo ilimradi mumjue anasoma wapi.