Jagina
JF-Expert Member
- Jan 29, 2019
- 11,549
- 5,386
- Thread starter
- #81
Kwani kuna mahali nilikuambia kuwa Luka alikuwa miongoni mwa mitume 12 wa Yesu? Sijasema hivyo popote.
Luka na Marko ni wainjili, hawakuwa miongoni mwa mitume 12 wa Yesu. Nadhani unafahamu kuwa baada ya mitume wale 12 wa mwanzo, waliongezwa wengine 70 kipindi Yesu bado yupo Duniani, hawa hawakuitwa mitume, bali waliitwa mashemasi. Na katika kundi hilo unampata pia Stafano, shahidi wa kwanza kufia imani ya Kikristo. Lakini hawa 70 walimwona na kumsikia Kristo wao wenyewe. Wapo wanaosema kuwa Luka alikuwa miongoni mwa hawa, lakini Luka mwenyewe kwenye injili yake anasema aliyoyaandika ni kufuatana na maelezo ya wale walioshuhudia wenyewe juu ya yale aliyonena Kristo, na matendo waliyoyaona. Hivyo Luka akiwa na uelewa mzuri wa kuandika, aliongea na mitume wa Kristo, na kuweka kwenye maandishi.
Lakini ufahamu pia, hata hao mashemasi 70 au 72 wa mwanzo, wapo walioandika injili, wanatajwa 13, lakini injili zao, japo hazikukataliwa, hazikuingizwa kwenye biblia kwa sababu tofauti tofauti. Mojawapo:
1. Kuwa na maelezo ya matukio machache sana, sababu mojawapo ni kutokuwe na Yesu toka mwanzoni, kulenga tu matukio fulani ambayo wao waliyaona ni muhimu na kuacha mengine mengi. Hivyo injili hizo zinatambulika na Kanisa, na zimetunzwa, ingawa siyo sehemu ya biblia. Kwa hiyo hizi injili 4, ndizo zilizoonekana kubeba matukio karibia yote I muhimu, zikiwa na contents zinazofanana sana. Ufahamu kuwa hata injili ya Petro na Thomaso hasikujumuishwa kwenye biblia, kwa sababu z0ilikuwa na matukio machache. Hivyo huwezi kuipuuza injili ya Luka eti tu kwa vile hakuwa miongoni mwa wale mitume 12, wakati kuna injili kama ya mtume Petro na Mtume Thomaso haikuingizwa kwenye biblia kwa sababu ya kuwa na matukio machache. Inaweza kutokea mtu ambaye hakushuhudia tukio akawa na moyo na hamu sana ya kupata taarifa na kudocument kila alichoambiwa kwa uhakika na wale walioshuhudia, kuliko yule ambaye aliyashuhudia yote, yeye akayachagua tu aliyoyaona ni muhimu zaidi.
Na Yohana kwenye injili yake analisema hili, kuwa Yesu alitenda mengi ambayo hayajawekwa kwenye biblia, bali yaliyoandikwa yameandikwa ili mpate kuamini na kusaidiki.
Ughushi mkubwa katika Luka 24:44–48 kuhusu “ufufuo wa Yesu siku ya tatu,” ukidai kuwa ulitabiriwa katika Agano la Kale ilhali haukutabiriwa!
Hebu tuangalie Luka 24:44–48 kutoka Biblia ya NIV:
Luka 24
44 Akawaambia, “Haya ndiyo niliyowaambia nilipokuwa bado pamoja nanyi: kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu katika Torati ya Musa, na katika Manabii, na katika Zaburi, hayana budi kutimizwa.”
45 Kisha akawafungua akili zao wapate kuelewa Maandiko.
46 Akawaambia, “Ndivyo ilivyoandikwa: Kristo atateswa na atafufuka kutoka kwa wafu siku ya tatu,
47 na kwamba toba na ondoleo la dhambi vitahubiriwa kwa jina lake kwa mataifa yote, kuanzia Yerusalemu.
48 Ninyi ni mashahidi wa mambo haya.”
Kuna ughushi mkubwa katika Luka 24:44–48! Inasema kwamba imeandikwa kuwa Yesu atakufa na kufufuka siku ya tatu.
Hilo liko wapi katika Agano la Kale?!
Nionyeshe aya moja tu ya Agano la Kale inayotabiri ufufuo wa Yesu siku ya tatu?