Uonevu wa Trafic Police Tanzania

Uonevu wa Trafic Police Tanzania

Si ndio zinaingia kwenye trilioni za mwezi jamani. Mnazani number itawezaje kutangazwa. Tutaisoma number tu...
 
Leo nikiwa natoka Arusha kwenda moshi dereva aliyekuwa akiendesha gari letu alipigwa faini kwa kuendesha spidi 56 mahala pa Spidi 50. Nilimuonea huruma kwa sababu hamna gari inayoonyesha spidi hamsini aidha 40 na 60 hivyo inabidi dreva aangalie mshale ukae kati.

Sasa swali, dereva ataangalia mbele au mshale ubalance? Abiria pia tulivyosikia dreva akibishana na trafiki tuliona ni kweli gari lake haina mahala panapoonyesha spidi 50 ila 40 na 60.

Uonevu kama huu ndiyo inafanya watu wachukie Jeshi la Polisi.

View attachment 398063
Mimi naomba nikusahihishe kidogo tu hapo uliposema hakuna gari inayoonesha speed 50. Zipo sema wewe hujaziona, kuna gari zina digital speedometer mfano toyota cresta,mark2,vitz za zamani. Ningesema modern cars ungesema tz gari nyingi za zamani. Pia zipo speedometer analog,za mshale zina 10/20/30.

Tukirudi kwenye hio gari isioonesha 50 naamini inaonesha 20/40/60. 50 ni katikati ya 40/60 kama ni dereva umepata leseni kihalali huwezi kushindwa ku balance 50kph.

Tusiwape hawa polisi sababu wote tunawajua lengo lao.
 
Hiyo 50 unaionaje kwenye speed meter?meter inasoma 40 halafu 60 unabalance katikati ambapo hamna namba kwenye speed meter.
Katika ya 40 na 60 kuna mstari mkubwa bold hapo 50. Nyuma na mbele ya huo mstari wa 50 kuna vimistari vidogo vya 45 na 55 respectively.
 
Sina hamu nao kabisa hao njaa kari.wana njaa sana hao watu yani ninavyoandika hivi hasira zinanipanda kila siku wananionea mimi siku hizi nasafiri usiku sababu yao tumekuwa tunaishi kama sio nchi yetu na ninamtafuta Mpinga siku moja nimueleze tunaishi km tupo jehanam wachukue magari yetu yawe yao km tunafaidi
 
Leo nikiwa natoka Arusha kwenda moshi dereva aliyekuwa akiendesha gari letu alipigwa faini kwa kuendesha spidi 56 mahala pa Spidi 50. .
Uonevu kama huu ndiyo inafanya watu wachukie Jeshi la Polisi.
View attachment 398063
Mkuu upo sahihi kabisa hili Jeshi sasa halitendi haki
mm nilipouona uzi huu nilimtafuta dreva niliyekuwa naye majuzi 07/09/2016
tukitokea Moshi mjini kwenda Arusha tulipofika Moshi Technical kuna kilima ambapo kuna matengenezo ta barabara wamemwaga changarawe mistari haionekani.
Dreva akalipita Lorry la container lililokuwa likienda taratibu kumbe mbele dreva anapiga tochi
hakuupata huo mwendokasi kwani ilikuwa kabla ya kibao cha 50
lakini akapigwa mkono na kuambiwa ame WRONG OVERTAKING
ibishi ukatokea kuwa mbona mistari ya barabarani imefukiwa na matengenezo?
bado wakadai ni Mlimani hairuhusiwi ni lazima ukae kwenye mstari
dreva akadai alipolipita alirudi kwenye mstari
jibu likaja km ni mbishi utalala kituoni hadi asubuhi upelekwe Mahkamani
au Changia 30,000/= upewe risiti yako uende
ulibidi tumuongezee akalipe yaishe km ni TRA au GOVT sawa
lakini ukusanyaji mbaya huo jamani mnaacha maajali mnatafuta vikosa km wring overtaking
kwa maana ya kiswahili sanifu ni kuwa drewa wetu alipitia magari KUSHOTO kwao
hela ikaenda hiyo, mafuta hatukuwa nayo
ile 5,000 ya JPM wakaikataa
 
Tifauti ipo ni kuwa 56>50
Amekuambia tofauti ya maana "significant difference" elimu
Poleni saana aisee, tatizo sio traffic tatizo ni hao wakubwa zao wanawawekea dau kubwa sana la kupeleka kwao, kuna mtu alinipa hio distribution nikashangaa, kwa Dar lazima upeleke si chini ya mabo matano (sikubuki vyema), the same to Mwanza na baadhi ya maeneo mengine. Aliyeyasema haya ni askari polisi sio kwamba nimetunga, sasa imagine kila leo mambo yanavyokuwa magumu, huyu askari atapata wapi hio idadi na unakuta wako zaidi ya watatu. Ndio maana kuna wakati wakikuona wanafaa kukushangilia na kukukimbilia hadi unajiuliza, hawa watu wana nini??

Yaani unakuata wanakanyagana wakigombea kukukamata.... kama vile ule mchezo wa kukamata kuku.
 
Kwani angeendesha chini ya 50 pia angepigwa fine. Kuna kamsemo kanasema heli nusu shari kuliko shari kamili
 
Hakuna risiti za kimagumashi kweli?,kinacholipwa watu wanatia mfukoni..
 
Huo msimamo na hizo adhabu walau zimesaidia kupunguza ajali, madereva wengine uspowakazia katika speed ya 56 siku ingine watazidisha mwishowe ajali bhaa!!
 
Next time akikaribia sehemu za spidi 50kph ashushe mpaka 40kph kabla hajaingia kwenye kibao cha spidi. 56kph > 50kph kwa vile rushwa inaendelea kupigwa vita ni vyema ameweza kulipa faini.
 
Kwa utafiti mdogo niliofanya nimegundua kwamba Idara ya Polisi inazidi kuchukiwa kutokana na vitendo vya kinyama na kidhalimu vinavyofanywa na trafic police.. sasa hivi wanalazimisha kukusanya faini kwa mabavu..ila naona muda si tusubiri maafa
 
Hawa jamaa ni waonevu hawana huruma hadi kwa walemav wanaotafuta rizik zao mf..madereva Bajaj fain km hizo huwa wanapigwa
 
Hawa polisi ndiyyo maana wanakosa ushirikiano toka kwa wananchi, wamekuwa wapinzani wa jadi.
 
Iko waz traffic hawana fear wao wanchojua ni kukupiga Notification tuu hawana Warning
Elimu pia muhim Kwa Jeshi letu sio kila kitu na faini tuu
 
Notification ina ukosefu wa risiti ya malipo ya serikalini (risiti ya njano). Hapo 30000 imeishia mfukoni mwa traffic, mimi nimewahi kufanyiwa hivyo inauma sana alafu jamaa ni wapenda shari kana kwamba umevunja sheria ya nyumbani kwao. Baadhi ya traffic hawana uwezo wa kutafsiri sheria za usalama barabarani badala yake wanatanguliza ukali ili tu dereva upate hofu na kukubali upuuz wanaotaka kukufanyia...
 
EFD ipo kwa majaribio dsm pekee.

Ukikatiwa hiyo notification paper/receipt pesa lzm itafika hazina.

Hakuna GRR ila kuna ERV ambayo kuipata ni kwa mhasibu baada ya aliyekukamata kuwasilisha pesa hiyo. Hapa kuna mapungufu, vitabu vya notification ni vingi lkn vya ERV ni vichache. Kuna imbalance.

Wanatakiwa kiyatatua lkn ikiingizwa kwenye electronic payment itatatua malalamiko ya muda mrefu.

Mwisho pesa hizo ni maduhuri ya serikali hazina. Ambacho sijajua, makusanyo ya mwezi sijui kama yanajumuishwa kwenye ripot mwezi ya TRA
Umeeleweka. Ila hapo kwenye ERV ni tatizo ambalo huwa linaleta mtafaruku mkubwa sana kati ya nyie askari na dereva. Serikali inahimiza kudai na kutoa risiti, hili somo linazidi kueleweka kwa wananchi wengi. Ajabu nyie mnaoiwakilisha serikali yenyewe moja kwa moja hamtoi risiti!! Aibu sana.
 
Next time akikaribia sehemu za spidi 50kph ashushe mpaka 40kph kabla hajaingia kwenye kibao cha spidi. 56kph > 50kph kwa vile rushwa inaendelea kupigwa vita ni vyema ameweza kulipa faini.
kuna kipenge pia kipo kinachokataza kuendesha gari kwa mwendo wa polepole bila sababu (yaani kufanya jam kwa speed ndogo)
unakuta sehemu ni over 50kph ww uanaenda 40 ni kosa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom