Uoga wa Serikali/CCM

Uoga wa Serikali/CCM

Ni mara kadhaa sasa nimeona na kusikia watu wakisema kuwa eti serikali inaogopa.

Kwamba inaogopa maandamano yanayopangwa kufanyika tarehe 26 mwezi Aprili.

Watu wasemao hivyo wanasema hivyo kwa sababu wamejiaminisha kuwa kama serikali ingekuwa haiyaogopi hayo maandamano basi baadhi ya viongozi wasingeyazungumzia hata kidogo.

Si ajabu hata hapa atajitokeza mtu atayesema kuwa hata mimi nayaogopa hayo maandamano na ndo maana nimeanzisha tena uzi unaoyahusu.

Sasa jana rais Magufuli naye kazungumzia watu kuandamana. Na si mara yake ya kwanza kufanya hivyo. Keshafanya hivyo mara kadhaa huko nyuma.

Magufuli kutaja neno ‘maandamano’ hiyo jana imekuwa nongwa. Watu wanataka kutuaminisha kwamba hayo maneno ya mitandaoni huko kuhusu hayo maandamano yanamnyima raha na usingizi rais kwa sababu mpaka yeye kayazungumzia hiyo jana.

Mimi sidhani kama serikali inaogopa. Ninachokiona ni serikali yenye watu wanaojua na kutambua kinachozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii. Kujua na kutambua huko si uoga. Si kuogopa.

Kuogopa ni pale ambapo wale waliokuwa wanapiga sana kelele za maandamano kutokujitokeza na kuandamana siku ambayo walikuwa wamepanga kuandamana. Huo ndo uoga na huko ndo kuogopa.

Maana tayari wameshaambiwa ole wao waandamane. Wataenda kusimulia yatayowapata. Sasa siku ya siku ikifika na hakuna anayeingia barabarani, huko ndo kuogopa.

Lakini mtu kusema kuwa kasikia kuna watu wamepanga kuandamana au Ngabu kuja kuanzisha nyuzi hapa kuhusu hayo maandamano, sioni uoga hapo.

Kwa hiyo, mimi nadhani na naamini kuwa wote wasemao kuwa serikali inaogopa wanasema hivyo kujipa faraja tu.

Wanajiaminisha kuwa serikali inaogopa ili wajisikie vizuri tu. Wajione na wao kelele zao dhidi ya serikali zina athari ingawa kiuhalisia sivyo hivyo.
Rais Magufuli zaidi ya kauli za kibabe ana nini kingine?
 
Mange Kimambi ni Mwanachama wa CCM

Tangu Mange Kimambi agombee ubunge CCM hajawahi kujitoa CCM

Mange Kimambi hakuwahi kufukuzwa uanachama CCM

Nyerere Alisema upinzani imara utatoka ndani ya CCM na huyo ni Mange

Maandamano ni ya Wanaccm, watanzania (Mgambo, Jeshi, Polisi etc)

Kwani waliotaka kumpindua Nyerere ni akina nani? Ni Wana CCM (TANU)

Someni historia nyie vilaza wa Lumumba/UVCCM aka Buku 7
 
Kinga ni bora.
Ndugu yangu, hii Kinga inawafanya mpaka wasio tumia mitandao ya kijamii huko vijijini kufahamu kuwa kuna maandamano. Kabla Mh raisi hajatoa tamko hakuna gazeti lilikuwa limeandika, sasa kaongea kila gazeti limeandika maandamano, maandamano. Mpaka magazeti ya nje. Hii ishu inatakiwa ibaki huko huko instergram na idhibitiwe huko huko na vijana wa mitandao. Ukikubali kuileta physical unaongeza ugumu wa kuihandle. Na pia ukiwaita wapinzani ukaongea nao na wao wakakemea, halafu ukaongea na viongozi wa dini na wao wakakemea. Baaasi.
 
Mimi sielewi kwanini kuna promo sana ya haya maandamano kutoka kwa wasiyoyataka kuliko Ilivyo kwa wanayoyataka. Sijaona nyuzi zinaosema tutaandamana kwa wingi kama ninavyoona za kuzuia maandamano.
NDIO WOGA WENYEWE. ATA MLETA POST NI MWOGA. MM NAFIKIRI ANGEJADILI HOJA ZA WANAOATAKA KUANDAMANA BADALA YAKE ANAJADILI WOGA WAKE. njoo ndugu ujadili hoja za wataka maandamano uoneshe usupirior wako. jaribu kukua kiakili, punguza ushabiki kua mtu wa kujenga hoja kwa yale mamb ya msingi.
 
Hivi wakiwaacha waandamane na kuwapa ulinzi kuona wanaelekea wapi na wanamaliza maandamano kwa amani kuna tatizo? I think tunatumia nguvu nyingi kuwazuia kuliko kuwaacha
Hii serikali inaongozwa na watu waovu ndio maana wanafikiria maovu,katiba inaruhusu raia kuandamana sasa sioni sababu ya serikali kuanzia Raisi,mkuu wa Jeshi,,mkuu wa polisi,waziri wa mambo ya ndani kupanik,....serikali nzima imepanik kutokana na mwanaharakati wa mitandaoni ambae hayuko hata Tanzania,....

Hii serikali dhaifu sana,serikali inayomgozwa kwa woga haiwezi kuleta maendeleo kwa raia wake
 
Hivi wakiwaacha waandamane na kuwapa ulinzi kuona wanaelekea wapi na wanamaliza maandamano kwa amani kuna tatizo? I think tunatumia nguvu nyingi kuwazuia kuliko kuwaacha
I couldn't agree more with you!

Ninaona kama wanazidi kujiongezea mizigo kuliko kujitua. Wangeua ndege wengi kwa kukubali hayo maandamano; kuyapa ulinzi katika routes zote; viongozi wasisitize umuhimu wa amani, umoja na ushirikiano; na kupunguza usumbufu kwa watu wengine kwa kushirikiana na waandaaji wa maandamano kupanga njia, destination na muda wa maandamano. Yaani wangekuwa wameonyesha 'ukomavu' wa hali ya juu na kupunguza gharama za rasilimali watu, wasilimali muda na sintofahamu wanazozidi kulimbikiza.
 
Mange Kimambi ni Mwanachama wa CCM

Tangu Mange Kimambi agombee ubunge CCM hajawahi kujitoa CCM

Mange Kimambi hakuwahi kufukuzwa uanachama CCM

Nyerere Alisema upinzani imara utatoka ndani ya CCM na huyo ni Mange

Maandamano ni ya Wanaccm, watanzania (Mgambo, Jeshi, Polisi etc)

Kwani waliotaka kumpindua Nyerere ni akina nani? Ni Wana CCM (TANU)

Someni historia nyie vilaza wa Lumumba/UVCCM aka Buku 7
Mange alipiga moto kadi ya ccm kwenye jiko la gesi na akarekodi video kabisa.
 
Nimeweka Mada ya kuuliza juzi kimetokea nini hapo Lugalo na kueleta purukushani imeondolewa haraka Sana kama ilivyo ada siku hizi
Hii inaonyesha waliosema itolewe wanajua kuna tatizo , sio hali ya kawaida
Ndio maana wengi tunaojua kuchambua mambo tuliwaambia muwe Makini Sana haya maandamano ni diversion strategy tu ... na hayaratibiwi na watu wa kawaida ni watu well connected in the system

Waliondoa topic kama siku ilipowekwa topic ya Upanga ilipondolwa haraka

Najiuliza na Huo ufa humo Ndani mkiwaingiza Mitaaani wadhibiti hali ,hawatawajeuka???
Na hao Polisi discipline Yao na morali ndio iko chini kuliko wote !!!!
 
Mimi sielewi kwanini kuna promo sana ya haya maandamano kutoka kwa wasiyoyataka kuliko Ilivyo kwa wanayoyataka. Sijaona nyuzi zinaosema tutaandamana kwa wingi kama ninavyoona za kuzuia maandamano.[/QUOT]

Huo ndio uoga wenyewe ambao baadhi ya watu wameweka pamba masikioni kama nyani
 
Back
Top Bottom