SoC02 Unywaji holela wa dawa bila kupewa maelekezo ya Daktari

Stories of Change - 2022 Competition

PRISCAR MWAKA

New Member
Aug 22, 2022
2
0
UNYWAJI HOLELA WA DAWA BILA KUPEWA MAELEKEZO YA DAKTARI
Dawa mtu hupewa baada ya kugundulika kuwa ana ugonjwa fulani au ana dalili za ugonjwa fulani, baada ya kumuelezea daktari kwa undani na kufanyiwa vipimo kutokana na dalili alizozisema ila siku hizi kumekuwa na ongezeko kubwa sana la unywaji holela wa dawa, watu wananunua dawa bila kupata maelezo kutoka kwa daktari, Kawaida inatakiwa baada ya kuhisi dalili fulani ambazo zinakufanya usiwe sawa kimwili umuone Daktari na kumuelezea na baada ya hapo Daktari huwa anakuandikia vipimo ambavyo inatakiwa vifanywe ili kuhakikisha kama kweli mtu huyo anaugonjwa.

Katika Jamii yetu tunayoishi watu wamekalili kwamba ukiona dalili fulani fulani imekupata utakuwa una ugonjwa fulani ,wamekalili hivyo bila kufahamu kuwa dalili moja inaweza ikasababishwa sio na huo ugonjwa tu bali magonjwa huwa yanaingiliana dalili mfano, mtu anaumwa kichwa anaenda duka la dawa na kuhitaji dawa za malaria wakati kuuamwa kichwa haina maana kwamba huna malaria peke ake.

Dawa maarufu kama dawa za kupunguza maumivu katika Jamii watu hutumiwa sana bila kuenda kupima hospitalini hili ugundulike kuwa wana ugonjwa gani ili uweze kupata matibabu ambayo ni sahihi dawa hizo ni nzuri kwakuwa kupunguza maumivu lakini tatizo hilo huwa haliishi inabaki palepale.


KWANINI KUNA ONGEZEKO KUBWA SANA LA UNYWAJI HOLELA WA DAWA
  1. Upotoshwaji uliopo katika Jamii mtu ana kuwa na elimu isio sahihi ambayo elimu hiyo ameipata kutoka kwa marafiki zake au ndugu wasio na elimu kuhusu mambo ya afya uelewa huo unapelekea Jamii kufahamu majina mengi sana ya dawa na matumizi yake
  2. Upatikanaji holela wa dawa katika maduka ya vyakula na sio maduka ya dawa hii hupelekea watu kujinunulia tu dawa bila kufuata maelekezo maalumu ya Daktari .
  3. kuhofia kukutwa na magonjwa ya ngono wakienda kupima hospitali kutokana na dalili wanazozosikia hali hii pia hupelekea unjwaji holela wa dawa bila maelekezo maalumu ya Daktari
  4. Sababu nyingine ni mtu kuona hali fulani ya utofauti katika mwili wake na kuona kuwa hiyo ndio hali yake hivyo dawa fulani ndio inayoweza kumsaidia kupima


MADHARA YA KUTUMIA DAWA BILA KUPEWA MAELEKEZO KUTOKA KWA DAKTARI
  1. Kuongeza sumu ndani ya mwili.
jinsi dawa ilivyotengeneza imetengenezwa kwa kutumia kemikali ambayo ni maalumu kwa ajili ya Kuua ugonjwa fulani sasa mtu anavokunjwa dawa ambayo sio ya huo ugonjwa husababisha mkusanyiko wa sumu ndani ya mwili wa mwanadamu baadae hupelekea hatali mbaya zaidi ndani ya mwili hatali hizo zinaweza kuwa za Mda mrefu au Mfupi kwa mtu Jamii zetu lazima ziwe na elimu kuwa dalili za ugonjwa mmoja zinaweza kuwa ni dalili za ugonjwa mwengine pia kwahiyo watu wasikalili maana madhara ya kunywa dawa isiyo sahihi ni hatari zaidi.
  1. Husababisha allergy
Kwasababu mtu huyu amekunywa dawa bila kufuata ushauri wa Daktari na bila kufahamu haswa tatizo ni nini basi huenda dawa alizotumia bila ushauri wa Daktari zikamsababishia kupata allergy fulani mfano kuwa na upele kwenye ngozi,kupata kifua na hii inatokana kwasababu kwenye hii dawa mtu aliokunywa huenda kuna chemikali ambayo mwili wake hauikubali chemikali hiyo.
  1. Husababisha tatizo kuwa sugu
Unavokwenda hospitali Daktari anakuandikia vipimo vipimo hivyo ukishaenda kupima maabara baada ya majibu kurudi daktari atakuandikia dawa kutokana na ugonjwa uliopatikana lakini pia na stage ambayo ugonjwa huo umefikia kwahiyo anakupa dozi ya mda fulani sasa kutumia dawa bila kujua ugonjwa kunasababisha kunjwa dozi Isio kamili sababu hiyo inapelekea vimelea vya ugonjwa vizoee dawa husika na husababisha ugonjwa huo usitibike hali hii inapelekea magonjwa sugu kuwepo mfano kuna watu kwenye Jamii zetu wana UTI Sugu ni kwasababu wamekunywa dawa za UTI bila kupewa maelekezo stahiki na dozi sahihi kutoka kwa Daktari.
  1. Husababisha Saratani(CANCER)
  • Unjwaji wa dawa kiholela bila ushauri na maelekezo ya daktari huwezi husababisha Saratani hii inatokana kwa sababu dawa hizo ambazo mtu amekunywa na sio sahihi kwa ajili ya kutibu ugonjwa fulani dawa hizo zinakusanyana mwilini na Kuua seli za mwili baadae seli hizo zinakuja kugeuka na kuwa seli za saratani ambayo ikisambaa katika mwili huenda ikapelekea madhara makubwa zaidi ndani ya mwili wa mwanadamu.
  1. Hupelekea kupungua kwa kinga ya mwili
Mwili kupunguza uwezo wake wa kujikinga dhidi ya Maradhi mbalimbali hii itapelekea mtu augue mara kwa mara sababu kinga yake ni hafifu na dhaifu.

  1. Unjwaji holela wa dawa hupelekea kifo
Hii inatokea sana sana kwa watu wenye magonjwa hatarishi zaidi kama watu wenye magonjwa ya moyo shinikizo la damu sababu dawa zingine huchochea tatizo na husababisha kifo kwao.

  1. Athali kwa mama mjamzito
Mama mjamzito inatakiwa awe makini sana kwenye kutumia dawa sababu dawa ambazo atatumia bila ushauri wa Daktari zinaweza kupelekea madhara kwa mtoto alioko tumboni mwake kwahiyo mama mjamzito asitumie dawa bila kupata maelekezo na ushauri kutoka kwa daktari.


NINI SERIKALI IFANYE ILI KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA UNYWAJI HOLELA WA DAWA BILA MAELEKEZO KUTOKA KWA DAKTARI

  • Kutoa Elimu
  • Serikali inatakiwa kutoa elimu kwa watu kupitia vyombo vya habari, magarazeti, radio ili watu waweze kupata ufahamu kwamba utumiaji holela wa dawa bila maelekezo ya daktari huwezi kupelekea athali mbalimbali katika mwili.
  1. Kukomesha uuzaji holela wa dawa kwenye maduka ya vyakula
Dawa inatakiwa ziwe zinapatikana kwenye maduka ya dawa pekee marufuku ni lazima itolewe kwenye maduka ambayo yanauza vyakula kwamba hayaruhusiwi kuuza dawa ,na dawa ambazo zinapatikana sana ni dawa maarufu kama dawa za kupunguza maumivu.


MAONI YANGU KUHUSU UNYWAJI HOLELA WA DAWA BILA KUPATA MAELEZO STAHIKI KUTOKA KWA DAKTARI

Watu inatakiwa waache kutumia dawa kiholela bila kupewa maelekezo ya daktari sababu madhara ambayo yanaenda kutokea ni makubwa sana kwahiyo ni vema mtu akijisikia vibaya asinunue dawa bila kwenda hospitali kupima ,unavoenda hospitali na kupima utagundulika ugonjwa unaoumwa na utatibiwa vizuri kuliko kunywa tu dawa bila kufahamu unachoumwa

Watu wasiogope kwenda kupima hospitali sababu gharama zingine za matibabu sio kubwa sana na mtu unakuwa na uwezo wa kuzimudu.
 

Attachments

  • inbound937494672.docx
    14.4 KB · Views: 4
Back
Top Bottom