PRISCAR MWAKA
New Member
- Aug 22, 2022
- 2
- 0
UNYWAJI HOLELA WA DAWA BILA KUPEWA MAELEKEZO YA DAKTARI
Dawa mtu hupewa baada ya kugundulika kuwa ana ugonjwa fulani au ana dalili za ugonjwa fulani, baada ya kumuelezea daktari kwa undani na kufanyiwa vipimo kutokana na dalili alizozisema ila siku hizi kumekuwa na ongezeko kubwa sana la unywaji holela wa dawa, watu wananunua dawa bila kupata maelezo kutoka kwa daktari, Kawaida inatakiwa baada ya kuhisi dalili fulani ambazo zinakufanya usiwe sawa kimwili umuone Daktari na kumuelezea na baada ya hapo Daktari huwa anakuandikia vipimo ambavyo inatakiwa vifanywe ili kuhakikisha kama kweli mtu huyo anaugonjwa.
Katika Jamii yetu tunayoishi watu wamekalili kwamba ukiona dalili fulani fulani imekupata utakuwa una ugonjwa fulani ,wamekalili hivyo bila kufahamu kuwa dalili moja inaweza ikasababishwa sio na huo ugonjwa tu bali magonjwa huwa yanaingiliana dalili mfano, mtu anaumwa kichwa anaenda duka la dawa na kuhitaji dawa za malaria wakati kuuamwa kichwa haina maana kwamba huna malaria peke ake.
Dawa maarufu kama dawa za kupunguza maumivu katika Jamii watu hutumiwa sana bila kuenda kupima hospitalini hili ugundulike kuwa wana ugonjwa gani ili uweze kupata matibabu ambayo ni sahihi dawa hizo ni nzuri kwakuwa kupunguza maumivu lakini tatizo hilo huwa haliishi inabaki palepale.
KWANINI KUNA ONGEZEKO KUBWA SANA LA UNYWAJI HOLELA WA DAWA
MADHARA YA KUTUMIA DAWA BILA KUPEWA MAELEKEZO KUTOKA KWA DAKTARI
NINI SERIKALI IFANYE ILI KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA UNYWAJI HOLELA WA DAWA BILA MAELEKEZO KUTOKA KWA DAKTARI
MAONI YANGU KUHUSU UNYWAJI HOLELA WA DAWA BILA KUPATA MAELEZO STAHIKI KUTOKA KWA DAKTARI
Watu inatakiwa waache kutumia dawa kiholela bila kupewa maelekezo ya daktari sababu madhara ambayo yanaenda kutokea ni makubwa sana kwahiyo ni vema mtu akijisikia vibaya asinunue dawa bila kwenda hospitali kupima ,unavoenda hospitali na kupima utagundulika ugonjwa unaoumwa na utatibiwa vizuri kuliko kunywa tu dawa bila kufahamu unachoumwa
Watu wasiogope kwenda kupima hospitali sababu gharama zingine za matibabu sio kubwa sana na mtu unakuwa na uwezo wa kuzimudu.

- Upotoshwaji uliopo katika Jamii mtu ana kuwa na elimu isio sahihi ambayo elimu hiyo ameipata kutoka kwa marafiki zake au ndugu wasio na elimu kuhusu mambo ya afya uelewa huo unapelekea Jamii kufahamu majina mengi sana ya dawa na matumizi yake
- Upatikanaji holela wa dawa katika maduka ya vyakula na sio maduka ya dawa hii hupelekea watu kujinunulia tu dawa bila kufuata maelekezo maalumu ya Daktari .
- kuhofia kukutwa na magonjwa ya ngono wakienda kupima hospitali kutokana na dalili wanazozosikia hali hii pia hupelekea unjwaji holela wa dawa bila maelekezo maalumu ya Daktari
- Sababu nyingine ni mtu kuona hali fulani ya utofauti katika mwili wake na kuona kuwa hiyo ndio hali yake hivyo dawa fulani ndio inayoweza kumsaidia kupima
MADHARA YA KUTUMIA DAWA BILA KUPEWA MAELEKEZO KUTOKA KWA DAKTARI
- Kuongeza sumu ndani ya mwili.
- Husababisha allergy
- Husababisha tatizo kuwa sugu
- Husababisha Saratani(CANCER)
- Unjwaji wa dawa kiholela bila ushauri na maelekezo ya daktari huwezi husababisha Saratani hii inatokana kwa sababu dawa hizo ambazo mtu amekunywa na sio sahihi kwa ajili ya kutibu ugonjwa fulani dawa hizo zinakusanyana mwilini na Kuua seli za mwili baadae seli hizo zinakuja kugeuka na kuwa seli za saratani ambayo ikisambaa katika mwili huenda ikapelekea madhara makubwa zaidi ndani ya mwili wa mwanadamu.
- Hupelekea kupungua kwa kinga ya mwili
- Unjwaji holela wa dawa hupelekea kifo
- Athali kwa mama mjamzito
NINI SERIKALI IFANYE ILI KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA UNYWAJI HOLELA WA DAWA BILA MAELEKEZO KUTOKA KWA DAKTARI
- Kutoa Elimu
- Serikali inatakiwa kutoa elimu kwa watu kupitia vyombo vya habari, magarazeti, radio ili watu waweze kupata ufahamu kwamba utumiaji holela wa dawa bila maelekezo ya daktari huwezi kupelekea athali mbalimbali katika mwili.
- Kukomesha uuzaji holela wa dawa kwenye maduka ya vyakula
MAONI YANGU KUHUSU UNYWAJI HOLELA WA DAWA BILA KUPATA MAELEZO STAHIKI KUTOKA KWA DAKTARI
Watu inatakiwa waache kutumia dawa kiholela bila kupewa maelekezo ya daktari sababu madhara ambayo yanaenda kutokea ni makubwa sana kwahiyo ni vema mtu akijisikia vibaya asinunue dawa bila kwenda hospitali kupima ,unavoenda hospitali na kupima utagundulika ugonjwa unaoumwa na utatibiwa vizuri kuliko kunywa tu dawa bila kufahamu unachoumwa
Watu wasiogope kwenda kupima hospitali sababu gharama zingine za matibabu sio kubwa sana na mtu unakuwa na uwezo wa kuzimudu.
Attachments
Upvote
0