Unpopular opinions kuhusu Samaki: Kutoka Dar es Salaam Kwenda Mwanza na Bukoba"

Akotia

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
455
1,069
Juzi kati nikipata fursa ya kutembelea Kanda ya ziwa Kwa wiki kadhaa. Nikapata uzoefu wa kipekee nilipotembelea Mwanza na Bukoba, maeneo ambayo mimi kama mkazi wa Dar es Salaam niliyozoea maisha yake ya pwani, nilifunzwa mambo mengi hasa kuhusu vyakula hasa hasa Samaki.

Nikiwa Dar es Salaam, nimekuwa nikila samaki wa baharini kama changu, kibua, jodari, na tuna fish. Hawa samaki wa baharini wana ladha nzuri sana, na unaweza kuwapika supu, katlesi, kuwachoma au kuwakaanga na bado watakuwa wazuri. Hii ilikuwa ndiyo taswira yangu ya "samaki" kwa miaka mingi.

Walakini, nilipofika Mwanza na Bukoba, nilishangazwa na tofauti katika aina ya samaki na ladha zao. Nilijaribu samaki wa maji baridi kama sato na sangara. Awali, nilijisikia kushangazwa kidogo na ladha yao, lakini baadaye nikagundua kwamba wanaweza kuwa watamu sana wanapopikwa na mchuzi wa nazi. Ingawa si sawa na samaki wa baharini niliyoizoea, nilianza kufurahia ladha yao tofauti.

Jambo lingine ambalo lilinivutia ni utofauti wa dagaa zao. Nimeshuhudia jinsi dagaa wa Mwanza wanavyokuwa na ladha tofauti na kufurahisha wakiwa fresh walivokaangwa kuliko wanavokuja Dar wakiwa wamekaushwa.

Uzoefu huu ulinifundisha kutathmini na kuthamini tofauti za kitamaduni na kuhusu vyakula. Ni wazi kwamba kila eneo lina rasilimali na utamaduni wake, na kujifunza kutoka kwa tofauti hizo ni sehemu ya uzuri wa kutembelea sehemu mpya.

Ningependa kusikia uzoefu wako au maoni yako kuhusu vyakula na utamaduni wa eneo unaloishi au ulilopitia.
 
Samaki wa ziwa victoria watamu sana,endelea kuenjoy,fika ziwa tanganyika uonje pia migebuka,kuhe na dagaa wa kigoma hakika utafurahi pia.
 
Back
Top Bottom