Unpopular Opinion: Liverpool hatotwaa taji lingine msimu huu

Baada ya tathmini yangu, nimegundua kuwa Liverpool hatotwaa taji lingine msimu huu na atabakia na kombe lake la Carabao.

Wote ni mashahidi, kwenye EPL tumeona moto wa Man City ambaye kwa mechi mbili zilizopita kafunga goli 10 na kuruhusu moja. Man City anapewa nafasi kubwa sana ya kutwaa EPL huku akiongoza ligi kwa point 3 na goal difference 7 dhidi ya Liverpool.

Liverpool kabakiza mechi na Southampton away na Wolves home wakati Man City kabakiza na West Ham away na Aston Villa home.

Hivyo naipa nafasi Man City ya kutwaa EPL nafukiri hii iko wazi kabisaaaa.

Kwenye F.A Cup weekend hii ni fainali ya Liverpool Vs Chelsea, hapa naona kabisa Chelsea wanavyoenda kubebea ndoo kutokana na Liverpool kumkosa kiungo wao Fabinho aliye majeruhi. Pia Chelsea ataitumia mechi hiyo kulipa kisasi cha Fainali ya Carabao.

Kwenye Uefa, ni Liverpool Vs Real Madrid. Hapa wanakutana waliopitia njia ngumu dhidi ya waliopitia njia nyepesi. Kwa historia ya miaka ya karibuni, jumlisha bahati, sijawahi kuona Real Madrid akifungwa fainali ya UCL. Kwa vyovyote vile nwapa nafasi Real Madrid kunyanyua makwapa.

Nihitimishe kuwa, Liverpool hawatobeba taji lingine msimu iwe unapenda au unachukia, na huo ni mtazamo wangu, tukutane mwisho wa mwezi huu kuthibitisha maono yangu.
Hapo kwa Madrid umechambua vizuri sana...irudiwe
 
Mimi siipendi madrid pia. Ila hoja ya jamaa hii ina ukweli ndani yake. Njia ya liverpool nyepesii sana. Plus hata swala la bahati wakikutana liverpool hana ya kumzidi madrid

Kwenye Uefa, ni Liverpool Vs Real Madrid. Hapa wanakutana waliopitia njia ngumu dhidi ya waliopitia njia nyepesi. Kwa historia ya miaka ya karibuni, jumlisha bahati, sijawahi kuona Real Madrid akifungwa fainali ya UCL. Kwa vyovyote vile nwapa nafasi Real Madrid kunyanyua makwapa.
Asante kwa appreciation
 
Wakati beki za liverpool zinawazuia washambuliaji wa benfica robo fainali.. beki za madrid zilikuwa zinamzuia mbape, neymar na wakali kibao wa psg wasipate goli

Nusu fainali pia wakati beki za liverpool zinazuia washambuliaji wa bei rahisi wa villareal wasipate goli.. beki za madrid zilikuwa zinazuia kevin da bruyne, riad mahrez, foden, na wakali kibao wa man city wasipate goli.

Hiyo tu inakupa picha.. njia ya liverpool kufika final nyepesi sana..

Huwezi kutwaa kombe kwa kumfunga inter milan hatua ya mtoano , then benfica robo na villareal nusu final.. huku mwenzako anamfunga psg na man city. Liverpool alikuwa kama anacheza europa league weak teams tupu

Liverpool hakuwa tested mpaka anafika fainali..

Angepitishwa njia aliyopita madrid asingetoboa
 
Mimi huko kistone: Oya wana ngoja ngoja niende kule JF baada ya haya matokeo nikasome comments za wadau maana kuna uto mmoja kasema eti vijogoo hawanyanyui tena kwapa msimu huu.
Vijogoo tunasubiri hiyo ndoo ya uefa kwa habari yako
Endelea kusubiri usichoke
 
Wakati beki za liverpool zinawazuia washambuliaji wa benfica robo fainali.. beki za madrid zilikuwa zinamzuia mbape, neymar na wakali kibao wa psg wasipate goli

Nusu fainali pia wakati beki za liverpool zinazuia washambuliaji wa bei rahisi wa villareal wasipate goli.. beki za madrid zilikuwa zinazuia kevin da bruyne, riad mahrez, foden, na wakali kibao wa man city wasipate goli.

Hiyo tu inakupa picha.. njia ya liverpool kufika final nyepesi sana..

Huwezi kutwaa kombe kwa kumfunga benfica robo na villareal nusu final.. huku mwenzako anamfunga psg na man city

Liverpool hakuwa tested mpaka anafika fainali..

Angepitishwa njia aliyopita madrid asingetoboa
Sahii kabisa
 
Back
Top Bottom