Unpopular Opinion: Liverpool hatotwaa taji lingine msimu huu

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
1,387
3,454
Baada ya tathmini yangu, nimegundua kuwa Liverpool hatotwaa taji lingine msimu huu na atabakia na kombe lake la Carabao.

Wote ni mashahidi, kwenye EPL tumeona moto wa Man City ambaye kwa mechi mbili zilizopita kafunga goli 10 na kuruhusu moja. Man City anapewa nafasi kubwa sana ya kutwaa EPL huku akiongoza ligi kwa point 3 na goal difference 7 dhidi ya Liverpool.

Liverpool kabakiza mechi na Southampton away na Wolves home wakati Man City kabakiza na West Ham away na Aston Villa home.

Hivyo naipa nafasi Man City ya kutwaa EPL nafukiri hii iko wazi kabisaaaa.

Kwenye F.A Cup weekend hii ni fainali ya Liverpool Vs Chelsea, hapa naona kabisa Chelsea wanavyoenda kubebea ndoo kutokana na Liverpool kumkosa kiungo wao Fabinho aliye majeruhi. Pia Chelsea ataitumia mechi hiyo kulipa kisasi cha Fainali ya Carabao.

Kwenye Uefa, ni Liverpool Vs Real Madrid. Hapa wanakutana waliopitia njia ngumu dhidi ya waliopitia njia nyepesi. Kwa historia ya miaka ya karibuni, jumlisha bahati, sijawahi kuona Real Madrid akifungwa fainali ya UCL. Kwa vyovyote vile nwapa nafasi Real Madrid kunyanyua makwapa.

Nihitimishe kuwa, Liverpool hawatobeba taji lingine msimu iwe unapenda au unachukia, na huo ni mtazamo wangu, tukutane mwisho wa mwezi huu kuthibitisha maono yangu.
 
Braza mm Nina uhakika 70% -90% Liver anabeba FA na UCL

Mimi siipendi madrid pia. Ila hoja ya jamaa hii ina ukweli ndani yake. Njia ya liverpool nyepesii sana. Plus hata swala la bahati wakikutana liverpool hana ya kumzidi madrid

Kwenye Uefa, ni Liverpool Vs Real Madrid. Hapa wanakutana waliopitia njia ngumu dhidi ya waliopitia njia nyepesi. Kwa historia ya miaka ya karibuni, jumlisha bahati, sijawahi kuona Real Madrid akifungwa fainali ya UCL. Kwa vyovyote vile nwapa nafasi Real Madrid kunyanyua makwapa.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom