Unpopular Opinion: Liverpool hatotwaa taji lingine msimu huu

Namshangaa jurgen klop bado anahangaika na mechi za EPL kwanini? hizo mechi za EPL zilizosalia atumie under 23 squad....klop nae!
 
Baada ya tathmini yangu, nimegundua kuwa Liverpool hatotwaa taji lingine msimu huu na atabakia na kombe lake la Carabao.

Wote ni mashahidi, kwenye EPL tumeona moto wa Man City ambaye kwa mechi mbili zilizopita kafunga goli 10 na kuruhusu moja. Man City anapewa nafasi kubwa sana ya kutwaa EPL huku akiongoza ligi kwa point 3 na goal difference 7 dhidi ya Liverpool.

Liverpool kabakiza mechi na Southampton away na Wolves home wakati Man City kabakiza na West Ham away na Aston Villa home.

Hivyo naipa nafasi Man City ya kutwaa EPL nafukiri hii iko wazi kabisaaaa.

Kwenye F.A Cup weekend hii ni fainali ya Liverpool Vs Chelsea, hapa naona kabisa Chelsea wanavyoenda kubebea ndoo kutokana na Liverpool kumkosa kiungo wao Fabinho aliye majeruhi. Pia Chelsea ataitumia mechi hiyo kulipa kisasi cha Fainali ya Carabao.

Kwenye Uefa, ni Liverpool Vs Real Madrid. Hapa wanakutana waliopitia njia ngumu dhidi ya waliopitia njia nyepesi. Kwa historia ya miaka ya karibuni, jumlisha bahati, sijawahi kuona Real Madrid akifungwa fainali ya UCL. Kwa vyovyote vile nwapa nafasi Real Madrid kunyanyua makwapa.

Nihitimishe kuwa, Liverpool hawatobeba taji lingine msimu iwe unapenda au unachukia, na huo ni mtazamo wangu, tukutane mwisho wa mwezi huu kuthibitisha maono yangu.
Mkuu Liverpool wameshakujibu huko,kombe la pili (fa cup) hilo kabatini. Ongea na moderators waufute huu upuuzi wako.
 
Mimi huko kistone: Oya wana ngoja ngoja niende kule JF baada ya haya matokeo nikasome comments za wadau maana kuna uto mmoja kasema eti vijogoo hawanyanyui tena kwapa msimu huu.
Vijogoo tunasubiri hiyo ndoo ya uefa kwa habari yako
 
Baada ya tathmini yangu, nimegundua kuwa Liverpool hatotwaa taji lingine msimu huu na atabakia na kombe lake la Carabao.

Wote ni mashahidi, kwenye EPL tumeona moto wa Man City ambaye kwa mechi mbili zilizopita kafunga goli 10 na kuruhusu moja. Man City anapewa nafasi kubwa sana ya kutwaa EPL huku akiongoza ligi kwa point 3 na goal difference 7 dhidi ya Liverpool.

Liverpool kabakiza mechi na Southampton away na Wolves home wakati Man City kabakiza na West Ham away na Aston Villa home.

Hivyo naipa nafasi Man City ya kutwaa EPL nafukiri hii iko wazi kabisaaaa.

Kwenye F.A Cup weekend hii ni fainali ya Liverpool Vs Chelsea, hapa naona kabisa Chelsea wanavyoenda kubebea ndoo kutokana na Liverpool kumkosa kiungo wao Fabinho aliye majeruhi. Pia Chelsea ataitumia mechi hiyo kulipa kisasi cha Fainali ya Carabao.

Kwenye Uefa, ni Liverpool Vs Real Madrid. Hapa wanakutana waliopitia njia ngumu dhidi ya waliopitia njia nyepesi. Kwa historia ya miaka ya karibuni, jumlisha bahati, sijawahi kuona Real Madrid akifungwa fainali ya UCL. Kwa vyovyote vile nwapa nafasi Real Madrid kunyanyua makwapa.

Nihitimishe kuwa, Liverpool hawatobeba taji lingine msimu iwe unapenda au unachukia, na huo ni mtazamo wangu, tukutane mwisho wa mwezi huu kuthibitisha maono yangu.
Unasemaje sasa?
 
Back
Top Bottom