Unpopular opinion: Huwenda Manchester City ikatoka kapa msimu huu

Ozone_

Member
Dec 30, 2023
88
107
Tangu kuanza kwa msimu wa soka 2023/24 moja ya timu ambayo ilitabiriwa kufanya makubwa kutokana na ubora wa wachezaji ilionao pamoja na usajili uliofanyika ukijumlisha na umahiri wa kocha pep guadiola, wengi walitazamia kuona timu hii ikifanya maajabu ya kurudia kile ilichokifanya msimu uliopita kwa kuchukua mataji matatu makubwa iliokuwa ikishiriki.

Sasa tofauti na msimu uliopita timu hii inaweza kumaliza msimu bila taii la ubingwa kwakuwa tayari mpaka sasa bingwa wa carabao cup ni Liverpool. Huku ikiwa katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu soka epl.

Hii itatokana na sababu nyingi ikiwemo zifuatazo;

Mosi, kukosekana kwa wachezaji muhimu katika mechi muhimu. Mchezaji kama rodri atakosa mechi dhidi ya Newcastle katika muendelezo wa fa cup na ukiangalia katika mechi zote alizokosekana msimu huu timu haikupata matokeo mazuri, pia mtu kama jack kukosekana kwako kumepunguza ubora wa kikosi kutokana na uwezo wake wa kucheza mpira pamoja na uwajibikaji wake tofauti na mtu kama doku.

Pili, uimara wa wapinzani wao. Msimu huu timu ponzani has ndani ya nchi ni Liverpool pamoja na arsenal ambao mpaka sasa wamekuwa na viwango bora hali inayotishia timu hii kuondoka patupo.

Tatu, kuongezeka kwa makosa binafsi hususani idara ya ulinzi. Kama umetazama vizuri utagundua kuwa magoli mengi waliofungwa man city msimu huu yametokana na makosa binafsi hususani kipa wap namba moja (enderso), huyu jamaa anaweza kuwa kafanya makosa mengi yalioigharim timu kuliko hata mtu mzima onana pale matofali ya kuchoma. Hii ni hatari zaidi hususani katika michuano mikubwa kama UCL.

Msimu bado haujaisha ila dalili za kutoka patupu zinaonekana.
 
Hujui mpira makosa yanasabishwa na upinzani kutokana na pressure ya mechi sema timu uwezo umepungua. Timu yoyote lazima ifanye makosa ndio ifungwe.
 
CITY msimu huu ndio kapoteza mechi nyingi sana. ila cha kushangaza timu zingine zimeshindwa kumuacha mbali.

ligi imebaki mechi 10. sizani kama hizo timu zinazoongoza ligi zina uwezo wa kushinda mechi zote 10 zitwae ubingwa.

sitashangaa kumuona City bingwa
 
Liver atashinda zote na kua bingwa
 
Vyovyote itakavyokuwa, Man City atabeba tena taji la EPL.

Arsenal ataanza kupoteza alama mechi ijayo pale Etihad.

Liverpool au Arsenal mmoja au wote wataangusha alama pale Old Trafford ni suala la muda.

Halafu usiwasahau Tottenham ya Big Ange inaweza ikabeba alama za Arsenal au Man City.

Bado naamini Man City atabeba ndoo tena ya EPL sijajua hizo nyingine.
 
Nimetunza hii komenti yako...
Ila nakuhakikishia kua Liverpool atakua bingwa sijaona timu ya kumzuia
 
CITY msimu huu ndio kapoteza mechi nyingi sana. ila cha kushangaza timu zingine zimeshindwa kumuacha mbali.

ligi imebaki mechi 10. sizani kama hizo timu zinazoongoza ligi zina uwezo wa kushinda mechi zote 10 zitwae ubingwa.

sitashangaa kumuona City bingwa
Pia ukiangalia msimu huu man city wamekuwa wakiruhusu magoli mengi jambo ambali linazipa confidence ya kupata matokeo timh pinzani
 
Back
Top Bottom