UNIVERSITY OF KILIMANJARO in Kenya

UNIVERSITY OF KILIMANJARO in Kenya

sisi hatukojolei kuran, aliyefanya hivyo ni mtoto mdogo. huna watoto kwenu wewe, hujazaa? utakapokuja kuzaa utajua kuwa mtoto wa mwenzio ni wako tu, na watoto huwa wanasumbua sana. kuweka liability ya alichokifanya mtoto kwa watu wazima au watz wote ni upungufu wa akili. zaidi ya yote, ikikojolewa moja, zingine si zimebaki? na pia, allah si ndo maandishi yake yale, atajipigania kwanini mmtetee kwasababu hananguvu? vitabu vyenyewe ivyo si vynachapwa apahapa duniani? kuna viwanda kabisa vinachapa si mtachapa vingine kile kilichokojolewa kitupwe mpate vile vizuri? akili ni kitu cha muhimu sana...dini zingine huficha akili za watu kabisa aisee. mbona jambo dogo sana mmeshupalia hadi leo?
mbona povu hivyo?? ni omo hiyo au puff?? i meant instead of pipo kukazania mambo ya kijinga, wangekomalia issues za maana na kuleta maendeleo nchini, kuna smthings ukizisikia u feel like change your blood and become a citizen of another country! hope sasa umenielewa, yaani hata kama ni kuandamana, tuandamane kwa mambo ya maana!
 
ni majuha yaliyoshika madaraka! period! inauma sana kwa kweli!
Sure cacico, kuna wakati ukifikiria unatamani ushike bunduki ukamtoe mtu madarakani. Yaani wapo wapo tu wanafikiria kuiba tu pesa ya nchi. Ndiyo maana Twiga wanapanda ndege wanaondoka, lakini Rais na mawaziri wa mambo ya nje na wa maliasili hawana habari. Inakera siyo siri.
 
Unajua kuwa kwenye utalii hospitality services ndio zinaingiza hela kuliko gate collection?
Mtalii atakuja Kenya, atakaa hotelini kwa dolari 250 per day, atatoka na malaya wa kikenya na kumpa dola 100, atahudhuria matamasha ya muziki na kula vyakula vyao, atakodi gari lililosajiliwa Kenya.
Atakuja huku atalipa kiingili na hela za potter ambazo hazifiki dola 200.
Nani mjanja hapo?

Fine, lakini hatuwezi ku-entertain watu walio jaa hila (hapa hakuna ujanja wowote ni hila/wizi tu) za ku-undermine Taifa letu, suala hili Mh.Membe anapaswa kulivalia njuga ili Wakenya wajuwe Tanzania means business, kwani hawajuhi hati miliki ina maana gani? Nafikili kwa mawazo yao wanafikili TANZANIA imelala usingizi, hatujuhi chochote kuhusu sheria za hati miliki; na ili ndilo tatizo kubwa la baadhi ya raia wa Kenya, wanafikili wanaweza kuvunja sheria za kimataifa wakapindisha vitu hapa na pale na kuachwa bila kukemewa au kuchukuliwa hatua KALI.

Wanarudia makosa ya Iddi Amini ya ku-underrate resolve ya Watanzania ya ku-deal summarily na watu wakorofi/arrogant.
 
mbona povu hivyo?? ni omo hiyo au puff?? i meant instead of pipo kukazania mambo ya kijinga, wangekomalia issues za maana na kuleta maendeleo nchini, kuna smthings ukizisikia u feel like change your blood and become a citizen of another country! hope sasa umenielewa, yaani hata kama ni kuandamana, tuandamane kwa mambo ya maana!
hili kwako ni povu, kwasababu umezoea mapovu, kwasababu labda hata wewe unatoa mapovu. i hope hutoi mapovu uko kunako kama wengine walivyo ndo maana unayajua mapovu. kama kuna mtu asiye na akili ni yule ambaye anaweza kuamini kuwa, unapoibiwa hakimiliki hauzulumiki....we ni mtu wa ajabu kidogo.hii ni issue ya kijinga? uelewa wako wote ndo umeishia hapo? or you have the ability to think more than that?
 
jamaa wanatuzidi kla idara, na hatuna jinsi ya kuwaulza, coz sisi waoga!
Wakenya wanavision sana, wakati nyie mwalalama wao wanajitangaza kimataifa,bravo!!
na sisi tunaendelea kulalama tu bila kubuni mawazo ya kuwabana wanaotudumaza au kujua jinsi ya kuzitumia the so called rasilimali zetu (rasilimali za dunia).
Embu angali huu mfano mmoja unaotokana na hawa jamaa kuwa visional:
Hizi picha leo zilikuwa kwenye home pages za vituo vya habari na mitandao mingi duniani. Vile vile mwaka jana kwenye final ya UEFA alikuwepo McDonald Malliga, hapo hujaongelea akina Rudisha, na wenzake au mjukuu wao Obama.

wnym.jpg
Barcelona's goalkeeper Victor Valdes (R) watches the ball hit the back of the net after Celtic's Kenyan forward Victor Wanyama (L) scored during their UEFA Champions League Group G football match at Celtic Park in Glasgow on November 7, 2012. AFP PHOTO/IAN MACNICOL
 
Haya ni majina tu hata kwetu yapo, unapomuita Mtoto Obama, Osama unaulizwa na nani? na Je Unapoiya Mtaa Samora unaulizwa na nani Kijini kwetu kuna kilima kinaitwa Kasenye wakati kasenye ipo uganda hapo vipi?
 
tofautisha mtaa na kilimanjaro. kuna kitu fulani hivi kwenye sheria ya hati miliki ya mwaka 1999, kinaitwa folklore rights, yaani kuna vitu fulani vinavyogusa Tanzania moja kwa moja na watz pekee ndo wenye haki hizo, vitu hivyo havitakiwi kuguswa ovyoovyo. mfano. huwezi leo hii kusikia mtu ameweka chuo kikuu kule marekani akaitwa university of serengeti, university of Dar es salaam (unless ni branch/campus tu), university of ruaha, university of mwalimu nyerere (unless sisi wabongo tumeruhusu kama kilivyo cha mandela kule arusha etc). hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kufaidika na kilimanjaro kwa namna yeyote ile ila watz, na sisi ndo wenye kazi ya kulinda hata jina la kilimanjaro lisichafuliwe kwani ukitaja tu kilimanjaro umetaja tz, serengeti, mikumi, ruaha, olduvai gauge, mt. meru etc. hii inatambulika dunia nzima...sasa watz huwa hatufuatilii vitu vyetu, ndo maana tunadharaulika.

Kama mambo ndiyo yako hivyo, kwanini tumezubaa kiasi hiki hadi tunaibiwa mali zetu huku tunaangalia tu? Kwa kweli tunahitaji Ukombozi mkubwa sana wa kiroho na kifikra ili tutoke katika laana hii. Inakuwaje nchi inakuwa na utajiri mkubwa wa raslimali lakini watu wake ni maskini?
 
sisi wenyewe tumeshindwa kujitangaza na kuitangaza mlima kilimanjaro sasa mnalalamika nini? waache wakenya watufanyie kazi ambayo tumeshindwa....JK kila siku yuko ulaya mmejiuliza akiwaga huko anaitangaza kilimanjaro? au kwa vile kilimanjaro haiko msoga hana time nayo?
 
ni jambo ambalo linakatazwa katika sheria za hakimiliki, naomba viongozi watoe majibu haraka hapa kwasababu tz ikionewa na kenya huwa naumia sana. yaani huw aniko tayari hata kurusha ngumi.

Ni lini TZ ilipata haki miliki ya jina 'Kilimanjaro'? Mbona hapa TZ tunatumia majina yao bila kuyalipia, mfano Kenyatta road? Kama wamefungua chuo kwa jina la Kilimanjaro, tatizo likn wapi? Mbona UDSM kuna Nkrumah Hall, pale Yanga kuna Kaunda Stadium, Dar kuna Mandela road, Sam Nujoma, A-town kuna Nelson Mandela Institute of Science and Technology: yote haya tunayalipia?
 
Wakenya wanavision sana, wakati nyie mwalalama wao wanajitangaza kimataifa,bravo!!

Kweli kabisa, wakati wao wanatafuta mbinu mbali mbali za kujenga uchumi wao - hata kuiba majina ya walio usingizini kama waTZ - viongozi wetu wanazunguka dunia mzima na bakuli wakiomba
 
Ok ok ok nimewaelewa! Kwahiyo tufanyeje? Tusiwe mahodari kwenye kuponda tu,tutoe na suluhisho,au sio wana jopo?
 
Ulichonacho ukishindwa kukitumia waliokaribu watakiusaidia kukitumia
 
Ni lini TZ ilipata haki miliki ya jina 'Kilimanjaro'? Mbona hapa TZ tunatumia majina yao bila kuyalipia, mfano Kenyatta road? Kama wamefungua chuo kwa jina la Kilimanjaro, tatizo likn wapi? Mbona UDSM kuna Nkrumah Hall, pale Yanga kuna Kaunda Stadium, Dar kuna Mandela road, Sam Nujoma, A-town kuna Nelson Mandela Institute of Science and Technology: yote haya tunayalipia?
tatizo ni kwamba watu hawajui intellectual law ya hapa tz, ndio maana unalinganisha mitaa na mlima kilimanjaro. kuna vitu fulani katika kila nchi ni urithi wa taifa na vinaitambulisha nchi hutakiwi kuvigusa, labda kwa ruhusa ya wenye nchi. kitu kama mlima kilimanjaro ambao hapa tz unatutambulisha, serengeti etc ni urithi wa taifa....huwezi kuvitumia katika mazingira ambayo yanaweza ku prejudice interest za nchi....mfano, leo hii watu wanaweza kuamini kuwa mlima kilimanjaro upo kenya na wakaenda kenya kutalii badala ya tz, au kenya wanaweza tumia jina hilo vibaya likachafua mlima wetu nasi tukapata hasara, hivyo ni sisi tunatakiwa kulinda vitu hivi ambavyo ni urithi pekee wa taifa letu. achilia hiyo mitaa etc....mlima kilimanjaro is beyond that...jaribu leo hii kujenga hotel halafu taja jina "israel hotel", au Jerusalem hotel, hapa dsm uone kitakachotokea....ukishindwa kuelewa hapa lete hela ya tuition nikufundishe kwa darasa kabisa...
 
je wakiweka jina la barabara mojawapo kuwa Nyerere road hapo vipi!!
nyerere road si urithi wa taifa....hata hivyo a road cannot be compared to kilimanjaro. sasa unataka pale Moshi wakijenga university wakitaka waite university of Kilimanjaro waache kwasababu mkenya ametuwahi?....jaribu leo kuweka chuo hapa ukiite University of Mt.EVEREST uone wenye mlima watakavyokuja juu.
 
Ni lini TZ ilipata haki miliki ya jina 'Kilimanjaro'? Mbona hapa TZ tunatumia majina yao bila kuyalipia, mfano Kenyatta road? Kama wamefungua chuo kwa jina la Kilimanjaro, tatizo likn wapi? Mbona UDSM kuna Nkrumah Hall, pale Yanga kuna Kaunda Stadium, Dar kuna Mandela road, Sam Nujoma, A-town kuna Nelson Mandela Institute of Science and Technology: yote haya tunayalipia?
akili yako ni sawa na unavyoonekana kwenye picha, ndo maana hujui kama mlima kilimanjaro ni hakimiliki ya watz na si mtu mwingine yeyote yule. tukusaidiaje aisee....hata kile ambacho Mungu amekuletea hadi sebuleni nyumbani kwako unataka explanation?
 
Haya ni majina tu hata kwetu yapo, unapomuita Mtoto Obama, Osama unaulizwa na nani? na Je Unapoiya Mtaa Samora unaulizwa na nani Kijini kwetu kuna kilima kinaitwa Kasenye wakati kasenye ipo uganda hapo vipi?
mzee, uzito wa mlima kilimanjaro na uzito wa majina ya hao watu binafsi si sawa. leo hii nakuambia ukiweka chuo pale arusha ukakiiita University of Mt. kenya, utaona watakavyofanya...mbona ni kitu kirahisi sana kuelewa jamani na watu hawaelewi? unapoita mtaa wa samora, samora ni kitu ambacho ni urithi wa taifa? ndo maana watu wakitoka nje wanasema watz tuna uwezo mdogo sana kufikiri.kama hali yenyewe ndo hii.
 
Back
Top Bottom