Baba Tunde
JF-Expert Member
- Apr 5, 2012
- 369
- 115
Hii inaumiza kwa sababu hatuko na maono ya mbele. Tanzania ni shamba la bibi!! Kuna siku nilikuwa natoka Dubai na shirika la ndege la Kenya. Katika foleni ya kuingia kwenye ndege kutokea board room, nyuma yangu alikuwa Mmarekani na Mkenya mmoja. Yule mmarekani alikuwa anakwenda Kenya na pamoja na mambo mengine alikuwa anataka kupanda mlima Kilimanjaro na kwenda Zanzibar. Nadhani alikuwa anakwenda Nairobi kwa Workshop. Aliuliza: "Nataka kupanda Mlima Kilimanjaro ila sijui ni masaa mangapi kutoka Nairobi?" Yule Mkenya alidakia haraka, ni karibu sana, one hour and a half. Yule bwana akauliza tena "Huo mlima si uko Kenya?" Jamaa akajibu tena, "ndiyo?". Nilipatwa na hasira ya ghafla na hamaki kwani yule Mkenya hakujua mie ni Mtanzania? Nilimpasha vilivyo na hatimaye aliishia kujiona mjinga kweli kweli, ingawaje ndio hivyo wanajitangaza. Kwa bahati mbaya nilikaa seat moja naye na mwisho wa safari aliishia kuniomba msamaha kwa aibu. Hapa ndugu zangu yatubidi kuwa aggressive kujitangaza, tena sana. Tunaonekana ni wajinga tu huko nje! Kwa mlima Kilimanjaro, ni kweli unatumiwa sana na jamaa kupata kipato. Tunachotakiwa kufanya ni kutoza kiingilio kikubwa kupanda mlima na njia ya kupanda zote ziwe protected. Mpandaji yeyote atakayethibitisha kutumia dola zaidi ya elfu moja nchini, tozo liwe dogo, say $100 na chini ya hapo, $500. Hii itapunguza fix za jamaa zetu na itafanya watalii wengi kuelekea Kilimanjaro kupitia Tanzania na si kushukia Kenya na kuja kupanda mlima. Pia kuwa na matangazo ya kutosha. Serikali itenge budget ya kutosha ili kuitangaza Tanzania Marekani, Ulaya, Japan, China, etc. Hii itasaidia sana. Pia watu wetu wapate mafunzo ya kutosha ya utalii. Ni lazima kutambua ya kuwa Wakenya katika Jumuiya ya Afrika Mashari hawako kwa maendeleo yetu, jamaa wako kibiashara, na udhaifu wetu ni faraja kwao. Just imagine zile Vurugu za Mbagala na Zanzibar, they went all over kutangaza kuwa Tanzania si salama kwa watalii kutembelea. Tukifunguka, wao wamekwisha!!! Tuache kulalama tuuuuu!!