Universe ni Ndogo: No light years between Planets or Galaxies

Universe ni Ndogo: No light years between Planets or Galaxies

Nini faida za moja kwa moja tunazozipata kutokana na kugundua mambo ya kwenye sayari nyingine?
Kwanini mataifa makubwa yana invest million dollars kwenye tafiti hizo?
Tuna assume sisi ni smart kuliko ng'ombe, mbuzi na fisi maana hao ndo hawana muda na uvumbuzi. Wanafurahia tu zawadi ya maisha. Hawana hata mikopo wale.
 
Tofauti siyo jina hujamwelewa mkuu... wanatuambia dunia pekee ndio ina mimea na wanyama (viumbe hai) sasa kwanini iendelee kuingia kundi moja na hizo nyingine
Maana ya sayaari siyo kuwa ni kuwa na viumbe hai. Rudi kasome ili heavenly body iitwe planet inakuwa na sifa gani. Kuwa na uhai siyo sifa moja wapo au kutokuwawa na uhai si sifa mojawapo. Ndiyo maana kuna mawe makubwa yanazunguka jua lakini hayaitwi sayari, ndiyo maana mwezi hautwi sayari. Imetofautishwa tayari kuwa ni syari lakini ni Earth, hakuna earth nyingine.
 
Kwa sababu kusema kuwa ulimwengu unatanuka manake unataka kuuwekea mipaka ulimwengu
Kutanuka haimaanishi kuwekea mipaka, kutanuka kuna maanisha hali ilivyooneka kwa mwanzo na inavyoonekana kwa sasa ni tofauti. Tofauti yake iko wapi? Tofauti yake ni kuwa hali yake imeongezeka ukubwa kutoka kwenye hali ya mwanzo ilivyokuwa. Lakini hapa dhana yake ipo juu zaidi ya hii tafsiri. Tutaona maelezo ya mbele yatafafanua zaidi.
Kama mambo yako hivyo suala la kutanuka unalipimaje wakati kinachotanuka ni nothing na kinatanukia kwenye nothing mkuu ?
Kinachotanuka ni ulimwengu. Ulimwengu siyo "nothing" ulimwengu ni "everything" ambavyo unavyovijua na unavyovisikia kwenye anga.

Hali ni kwamba, "Big Bang" ilivyotokea an entire universe (ulimwengu) full of energy ukazaliwa pia na "space". Aina yoyote ya energy inazalisha mazao ya nishati ambayo yatazaliwa. Mojawapo ya kani inayotokana na mazao ya nishati hizo ni "repulsive gravity" Hii inaitwa "Energy of nothing". Hii ni kani/nishati ambayo kinzani. Ni nguvu ambayo haileti nguvu pamoja, ni nguvu ambayo inayosukumiza vitu kuelekea kivyake. Hapa ndipo unapopatikana msingi wa kusema ulimwengu unatanuka. Ina maana galaxies uwepo wake uliyoonekana juzi ni tofauti na ulivyoonekana leo, zinazidi kukwepana kuwa mbalimbali. Hii tafsiri ndiyo tunasema ulimwengu unatanuka.
Sasa kinachotanuka ni empty kabisa,na hicho kinachotanukiwaa ni empty,sasa hapo unapimaje huo utanukaji,na umejulikana vipi wakatti hakuna mipaka baina ya ulimwengu na kule ambako ulimwengu unatanukia...
Ukisema empty maana yake ni kitu kilicho na hali ya kuhodhi kitu lakini hakina kitu. Bila shaka ulimaanisha nothing.

Ukisema nothing ina maanisha hakuna chochote. Na Ulimwengu si nothing ama ukiupa taswira ya empty kama ulivyoipa , bali ulimwengu ni everything kama mwanzo nilivyoandika. Tafsiri inayokuja hapa ni "Everything inatanukia kwenye Nothing". Ukiifikiri maana ya Nothing ni unafikiri kwa kufikiri kusipo na kufikiri. Kwa sababu hakuna kitu! Na kusipokuwa na kitu kukijiwa na kitu panakuwa kitu, na ndivyo universe inavyofanya! Inatanukia kwenye nothing then ina occupy ile hali inatengeneza mazingira yake na ndivyo mchezo unavyokuwa.
 
Kama ulimwengu hauna mwanzo wala mwisho vipi utanuke kama unatanuka basi unaukingo yani mpaka Wa ulimwengu
Ok labda niiweke hivi!

Maana ya hayo maneno ni hii: Sayansi na teknolojia ya sasa haifahamu mwanzo wa ulimwengu ni upi na mwisho wake ni upi! Bali wanafahamu pale nguvu na maarifa ya sayansi na teknolojia yalipoishia. Kwa sababu kuna zillion na zillion za galaxies. Yaani hazina idadi, hazihesabiki! Kwa hili wakasema universe ni infinite! Ni endless! Ni limitless.
 
Ikiwa mambo yako hivi manake universe ni kama lea flani ambayo inatanuka.

Nahapo tukifikiria vizuri tutaona kuwa kama ni hivyo manake hapo kuna vitu vitatu.

Kuna universe yenyewe ambayo ndo inatanuka.

Kuna space ambayo universe ndo hutanukia.

Na kuna mpaka baina ya universe na kitanukiwa.

Sasa jee kule ambako universe hutanukia,yaani kule kunakotanukiwa na universe,yani kabla ya universe haujatanuka,vipi kule ambako tunatarajia universe utanukie sio universe nako ?

Kama sio universe ni wapi huko ?

Kama ni universe dhana ya kutanuka inakufa hapo.
teh
 
Sayansi ya anga ni UZUSHI PERIOD.

Kumbe hata hujaelewa, zimeona hayo maeneo jinsi yalivyokuwa billions of years ago. Yani kile zilichokiona sasa ni cha hizo billion light years ago maana huo mwanga ulizofikia umetoka huko billions of
Hiyo Billions years wameijuaje ? Na hii siyo sayansi maana njia za kujua mbo ya kale zina taka chain.
According to physics universe had to be expanding or contracting at a speed of light.
Je kulifanyika jaribio la kisayansi kuipa nguvu hii kauli ?
Einstein aligundua hili lakini akawa mwenyewe anapingana nalo, na kufanya formula yake ikubariane na upingaji wake, alaweka kitu kinaitwa cosomological constant which was a mistake ambapo baadae ilikundulika kuwa ni kweli ulimwengu unapanuka kwa kasi ya spidi ya mwanga, so mawazo ya Einstein yalikuwa sawa tu ila akajishtukia tu.
Tuoe faida hapa kaka, walitumia nini kugundua hilo la ulimwengu kutanuka kwa mwendo kasi wa mwanga ?

Pili, naomba unifahamishe hii speed ya ligjt inapimwaje ?

Ahsante.
 
Hiyo Billions years wameijuaje ? Na hii siyo sayansi maana njia za kujua mbo ya kale zina taka chain.

Je kulifanyika jaribio la kisayansi kuipa nguvu hii kauli ?

Tuoe faida hapa kaka, walitumia nini kugundua hilo la ulimwengu kutanuka kwa mwendo kasi wa mwanga ?

Pili, naomba unifahamishe hii speed ya ligjt inapimwaje ?

Ahsante.
Mheshimiwa topic ya Physics inayofundishwa kuanzia O level mpaka Vyuo vikuu wewe unataka ueleweshwe na uelewe ndani ya dakika tano [emoji119][emoji119][emoji119] Kwa kifupi experiments zilizofanyika zimekuwa approved with concrete reasoning

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nini faida za moja kwa moja tunazozipata kutokana na kugundua mambo ya kwenye sayari nyingine?
Kwanini mataifa makubwa yana invest million dollars kwenye tafiti hizo?
Kwa kweli hata mimi siwaelewi hawa NASA wapo bize na vitu ambavyo havina faida kwa binaadam

Maana sijawahi kusikia NASA wameenda kuchimba dhahabu sayari ya Mars au Mwezini
 
At a point in life hizo sayar zilikua na viumbe hai.sayar za mwanzo zile

Ustake knowledge zaid..mambo ni meng..kumbuka jua lina tanuka.joto la sasa na mwanga wa sasa sio ulivyokua miaka bil kadhaa nyuma..kadir balance ya joto na mwanga inavyokua ndo support ya uhai inavyokua..higher joto na higher mwanga no life..less joto na less mwanga no life..life inataka moderate..dunia iko moderate...kumbuka light ni energy..mmea hauwez ishi wala kutoa hewa bila light..binadam hawez survive au kiumbe mwingne hawz survive bila light..BUt vyote hvyo lazima viwe kwenye balance sio high wala sio low..moderate ndio uhai unapotokea..so planet za kwanza zilikua na viumbe at a time.ila planet hzo zmekufa kwa sabab ya kimazingira kutokana na jua na tabia yake
Sayari yetu ya dunia ni tofauti sana na hizo sayari nyingine kwa zaidi ya 99%.
 
Mheshimiwa topic ya Physics inayofundishwa kuanzia O level mpaka Vyuo vikuu wewe unataka ueleweshwe na uelewe ndani ya dakika tano [emoji119][emoji119][emoji119] Kwa kifupi experiments zilizofanyika zimekuwa approved with concrete reasoning

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpaka nakuuliza hayo maswali ujue kwamba sijaona hizo concrete reasons, landa kama zipo nyingine au kama kuna majaribio ya kisayansi yali fanywa kuthibotisha hilo.

Kwa ufupi Fizikia nimeisoma mpaka kidato cha tano na sita, kwahiyo sihitaji kufundishwa nahitaji kuambiwa ukweli jui ya hayo maswali niliyo uliza.

Tuendelee ....
 
Sorry what is universe in its real meaning... What's the different between galaxy, world and earth

Jr[emoji769]
Galaksi (ing. galaxy) ni kundi la nyota nyingi zinazoshikamana pamoja katika anga ya ulimwengu kutokana na graviti yao. Nyota hupatikana angani katika makundi kama mawingu makubwa sana.
Kuna galaksi nyingi sana ulimwenguni. Kwa wastani kila galaksi imekadiriwa kuwa na nyota kama bilioni 100 lakini kuna galaksi kubwa na ndogo.
Galaksi yetu, ikiwemo mfumo wetu wa jua, imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya bilioni 300 (3·1011). Sehemu ya nyota hizi zinaonekana kama kanda la kung'aa kwenye anga la usiku linalojulikana kwa rangi yake kama njia nyeupe au "njia ya maziwa"[1]. Umbo lake linafanana na kisahani kikiwa na kipenyo cha miakanuru 100,000 na kikiwa na unene wa miakanuru 3,000.
Kwenye kitovu cha galaksi graviti ni kubwa sana kiasa cha kwamba galaksi nyingi huaminiwa kuwa na shimo jeusi kituvoni[2].
Galaksi zilizo karibu angani zinaitwa Mawingu ya Magellan ambayo ni galaksi mbili ndogo zilizopo kwenye umbali wa miakanuru 170,000 na 200,000. Galaksi kubwa ya jirani ni Andromeda na ina umbali wa miakanuru milioni 2.5.
Idadi kamili ya galaksi zote angani haijulikani. Kuna makadirio ya kwamba idadi ya galaksi zinazoweza kuangaliwa kwa vyombo vinavyopatikana ni mabilioni. Hadi sasa sehemu ndogo tu imehesabiwa lakini mara kwa mara galaksi mpya zinatambuliwa kwa njia ya darubini au vyombo vya angani.
Galaksi zinazojulikana zimepewa namba katika orodha ya kimataifa na wanasayansi wa astronomia.
Galaksi kati yao hujumuika pia zikiathiriana kwa njia ya graviti yao na kuzunguka kitovu cha graviti cha pamoja. Galaksi hadi 50 zinazoshikamana katika kipenyo cha miakanuru milioni 10 huitwa kundi la galaksi (ing. galaxy group). Kuna pia galaksi mamia hadi maelfu kadhaa zinazoshikamana na hii huitwa fundo la galaksi (ing. galaxy cluster) linaweza kuwa na kipenyo cha miakanuru milioni 10 - 20.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka nakuuliza hayo maswali ujue kwamba sijaona hizo concrete reasons, landa kama zipo nyingine au kama kuna majaribio ya kisayansi yali fanywa kuthibotisha hilo.

Kwa ufupi Fizikia nimeisoma mpaka kidato cha tano na sita, kwahiyo sihitaji kufundishwa nahitaji kuambiwa ukweli jui ya hayo maswali niliyo uliza.

Tuendelee ....
Unasema umesoma Physics na unauliza speed of light imepatikanaje? Are you serious? Mpaka conclusions zifikiwe inamaanisha experiments za kutosha zimefanyika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom