United State of America to Become Failed State ?

United State of America to Become Failed State ?

Chochote kinaweza kutokea hapa duniani mkuu.
Mataifa yanazaliwa, yanakuwa makubwa na mwisho wake yanapotea kabisa.
Alichokisema ndugu Bowie kipo lakini ni sababu chochoze tu/Sababu za ghafla (Immediate causes)
Mwaka 1976 kuna mwanasayansi wa siasa na historia kutoka Ufaransa anaitwa Emmanuel Todd alisema taifa la Urusi au U.S.S.R lingesambaratika ndani ya miaka 20 ijayo kutokana na sababu kama vifo vingi vya utotoni (High Mortality Rate), Rushwa ndani ya chama cha kikomunisti (CPSU), mgogoro baina ya Uchina na Urusi (Sino-Soviet Split) na sababu nyingi sana za msingi.

Alikuwa na miaka kama 27 kipindi hicho,
Na ikumbukwe miaka ya 60's na 70's Urusi alikuwa anaongoza kwa kuwa na nguvu kubwa kijeshi,
hasahasa alivyomfanya Marekani huko vietnam.
Alikuwa na Teknolojia kubwa sana ya anga, wao ndiyo walikuwa wakwanza kurusha Satelaiti ya kwanza na kupeleka mtu nje ya dunia.
Biashara yao ya mafuta na silaha imekaa vizuri sana na hadi wataalamu wakasema ndani ya miaka 30 tu wakimaanisha mwaka 1990-1995 Urusi itakuwa ndilo taifa pekee lenye uchumi mkubwa duniani na Marekani itasambaratika kwasababu mataifa ya Asia na Ulaya yatamfuata Mrusi.
Kwa kifupi uchumi wa China unavyokuwa kwa kasi kipindi hiki basi ndiyo U.S.S.R ya miaka ya 60 na 70.

Watu walimpinga Todd wakasema anaota ndoto za mchana, hata wasomi wa Ufaransa walikataa utabiri wake wa kisayansi wakisema hauna mashiko.
Lakini mwaka 1990 badala ya Urusi kuwa taifa kubwa kama walivyosema mwaka 1963 Urusi ikasambaratika vibaya na kwa aibu kubwa.
Bahati mbaya alichokisema huyu bwana Emmanuel Todd miaka ya 1976 kilitokea kwa zaidi ya asilimia 90%

Mwaka 2003 wakati Marekani imetoka kuvamia Kossovo, Afghanistan na yuko Irag.
Emmanuel Todd aliandika kitabu kingine k
inaitwa AFTER THE EMPIRE: THE BREAKDOWN OF AMERICAN ORDER. Humo ndani aliandika kwamba Marekani itaanguka vibaya na dunia nzima haitaamini. Alitabiri kutokea kwa deni kubwa la Marekani ambalo baada ya mtikisiko wa uchumi wa mwaka 2008 alilitengeneza baada ya kukopa sana hela kwa Uchina na Japan.
Akaseme kuanguka kwa maadili ya Kimarekani yaliyoifanya Marekani liwe taifa kubwa duniani; akasema Marekani imeruhusu nchi yake iongozwe na wawekezaji wa wakubwa wa Marekani hapo hapo na Ulaya. (Good Will of Investors) akasema wawekezaji wanaweza kuiacha Marekani peke yake na kweli hili linatoke sasa labda uwe kipofu.

Ford Motors wanataka kwenda Mexico,
Boeing wanatengeneza kinu chao huko Uchina,
CF Fertilizer Industries inahamia kabisa Uingereza,
Coca-Cola Enterprise nalo linahamia Uingereza.

Au yasipohama yanaungana na makampuni mengine kama BAYER na MONSANTO,
Kibaya zaidi hapa inabidi wachague makazi mapya maana Sheria ya Makampuni (Corpoate Law) itataka kampuni isajiliwe upya.
Kifupi tu tokea mwaka 1983 hadi mwaka 2014 zaidi ya kampuni 47 zimehama Marekani; hichi ziyo kitu kidogo wala cha kupuuzwa. Ukisoma gazeti la THE ECONOMIST la tarehe 16 Agosti mwaka 2015 wamezungumzia hili jambo kwa kifupi. Nakuwekea link hapo chini usome na uchambue mwenyewe.

Kingine kinachonishangaza cha Todd ni kinachotokea sasa.
Alisema Urusi na mataifa ya mashariki ya kati yatashikamana sana (unaona kinachoendelea Syria, Iran na Uturuki),
Urusi na bara la Ulaya watakuwa washirika wakubwa wa kibiashara wa Urusi, (Urusi leo ni soko kubwa la Jumuiya ya kibiashara ya Ulaya na hata vikwazo vyao vimeathiri baadhi ya nchi za Ulaya)
Yeye anaamini kwamba Marekani ilikuwa ya maana kwasababu dunia hasa mataifa ya Magharibi yaliwaogopa sana Warusi na Ukomunisti, sasa ili kupata ulinzi walienda kwa Marekani.
Leo Wasovieti na ukomunisti vimekufa na havirudi tena Marekani ni lazima angebadilisha mkakati wake.

Hiki kitabu mimi nimekisoma chuo japo Wazungu wengi hawakipendi kabisa na wanakikosoa sana,
Nakumbuka profesa moja alisema "GOD IS REAL AND HE IS AN AMERICAN"
Utabiri wa mwanasayansi huyu mtu makini huwezi kupinga kwasababu amefanya tafiti za kisayansi zinazoonekana .
Hata Profesa Stephen Cohen mtaalamu namba moja wa masuala ya Siasa za Urusi na Historia ameonya juu ya utabiri haya mambo.

Link:After the Empire | Books | Columbia University Press
Link: The Economist explains: What’s driving American firms overseas | The Economist
Link:After the Empire
Link:Bayer and Monsanto to merge in mega-deal that could reshape world’s food supply
Link:s://www.theguardian.com/theobserver/2004/feb/08/society.politics


CC: Apollo , Dotworld , Bukyanagandi , Koba , maalimu shewedy , Barbarosa, kui , MSEZA MKULU , MOTOCHINI
Duuuuh watu mmeshiba nondo siyo Mchezo!!!! Duuh ...international affairs...
 
Mtaniona mimi ni mwendawazimu but that is reality. Tatizo lenu mna lack of knowledge katika masuala ya dunia hii . Kuna taifa kubwa kama ilivyokuwa USSR leo hii iko wapi. I think majority ya nyie mlitoa maoni yenu you are from secondary ya Kata.
May be ungejaribu kutafuta ni nafasi gani anayo rais ktk kufanya maamuzi magumu yanayohusu taifa hilo.
 
Kama sio saud arabia kutumiwa na marekani kushusha bei ya mafuta mwishoni mwa miaka ya 80 soviet union haingeanguka,
urusi ilijikute mapato yamepungua wakati ina mzigo mkubwa wa kubeba ikabidi ivunjike,hata kutoka afaghnstan sio kuwa walishindwa kwa vita bali pesa ilikauka,solution ikawa ni kurudisha majeshi nyumbani,
putin aliirudisha juu Russia,lakini tena mmarekani wakazoza na hawa waarabu wa saud ili wapunguze tena bei ya mafuta,lakini sasa russia alikuwa pia anauza gesi huko ulaya,sasa ili wamarekani waibinye vizuri russia,walipanga na wasaudia lijengwe bomba la gesi toka qatar likipita syria mpaka ulaya ili wazungu wa ulaya waache kununua gesi ya mrusi ili tena waiporomoshe russia,
assad akiwa na uhusiano mzuri na russia aligoma kukubali bomba lipite syria kwahiyo ilibidi assad apigwe vita atoke,ndo kisa cha mrussia kukomaa pale syria.

Uchumi wa marekani hauko kamili sana hasa baada ya kupiganisha vita ambavyo vimeicost matrilion ya dola na nchi kujikuta na deni lisiloweza kulipika,lakini kinachoibeba marekani ni mfumo wa petroldollar,
asilimia kubwa ya viwanda vyake vilihamia china,vietnam,bangladeshi kwasababu gharama za kuendesha kiwanda marekani zilikuwa juu,kiasi wenye viwanda wakawa hawapati faida,
siku nchi kama saud ikiiamua kuuza mafuta kwa pesa yeyote tofauti na dollar ndo siku dollar ya marekani itaanguka,na hilo marekani hawatakubali na ndo maana kuna kambi za jeshi huko saudi arabia,qatar,bahran na pia kuwait.
Siku wanahama kutumia dollar ndo siku marekani atawageuka na kuwapindua na kisha kuweka kibaraka wao.
Suala la uchumi kwa wamarekani ni national security issue na wako tayari kwenda vitani kulinda nafasi yao kama superpower ndo maana hawaishi kuzifanyia chokochoko nchi kama Russia,china,brazil etc
 
If the nation is founded in God's principles and later her people do not adhere to that principles what will follow is the punishment from God. America is slowly falling apart from God's principles and expect punishment from God and one of the likely punishment is economic melt down. We are not praying for that because America is assisting many nations financially. This may take time to come because of the few American who pray day and night that God can have mercy and save the nation from going down. Remember also American has God's favour because of association with Israel. Those who bless Israel shall be blessed. Every nation dissociate with Israel will be cursed. Is what happened to our nation when we cut our tie with Israel. You may not believe this because is more on spiritual side but this is the truth.
 
If the nation is founded in God's principles and later her people do not adhere to that principles what will follow is the punishment from God. America is slowly falling apart from God's principles and expect punishment from God and one of the likely punishment is economic melt down. We are not praying for that because America is assisting many nations financially. This may take time to come because of the few American who pray day and night that God can have mercy and save the nation from going down. Remember also American has God's favour because of association with Israel. Those who bless Israel shall be blessed. Every nation dissociate with Israel will be cursed. Is what happened to our nation when we cut our tie with Israel. You may not believe this because is more on spiritual side but this is the truth.

Aren't the Israelites going against The Sacred rules of the Torah and The Bible which are the sole basis of their statehood and their religion? Which god are they serving nowadays?
Such are the cumbersome questions tormenting my head, please shed some light.
 
Law of diminishing marginal return soon camming in America
 
Back
Top Bottom