Happy Nyerere Day na kwako pia mkuu. Binafsi nilihitaji sana uelewa wa mtoa mada katika jambo hili la mkataba wa wa Marekani kwa lengo la kuongeza kitu. Ninafahamu fika kuwa Marekani kwa sasa imeshana kwenye nyavu zinazopelekea kuutisha umoja wao.
Tangu katikati na mwishoni mwa miaka ya 90, marekani ilijikita zaidi katika kuhakikisha inalidhoofisha na kulisambaratisha kanisa katoliki au kupunguza kabisa ushawishi wake ndani ya Marekani na Duniani kwa ujumla, kwa kuanza kuibua kashfa za wale maaskofu za kunyanyasa watoto wa kiume kimapenzi. Mtandao wa Kanisa katoliki uligundua njama hizo na ilionekana hata wale watumishi walipenyezwa kujiunga na kanisa kimkakati tangu ujana wao. Ni katika nyakati hizo ambapo utawala wa Bill Clinton ulikumbana na msimamo wa Kanisa kupinga projects za wamerekani za kufanya Human Cloning, ndipo utawala ule uliamua ku press the button na kutumia zile kshfa za wale maajent maaskofu na mapadri.
Baada ya kuibua kashfa zile ndipo yule Papa mzee ambaye pamoja na uzee wake lakini akili zake bado zilikua na makali ya wembe mpya, aliamua kuwaita maaskofa na mapadri wote waliohusishwa katika kashfa zile. Walipofika Vatcan, Pope John Paul The second aliongea nao kwa kirefu na kuwataka wachague 'upande' Viongozi wale wa dini waliamua kubaki kundini na kuendelea kulitumikia kanisa, ndipo Pope John Paul II aliamua kufanya nao mafungo na maombi kwa muda wa siku kumi (18) kama sikosei, baada ya mafungo hayo akawaongoza katika toba na kuwaruhusu warudi maeneo yao ya kazi. Hakuna ajuae kwa hakika nini kiliongelewa kati ya Pope wale mapadri na cardinals wengine, ila jambo la uhakika ni kwamba kashfa zile hazikuongelewa tena popote wala na chombo chochote ndani ya Marekani.
Utawala wa Bush ulifanya jitihada kubwa sana kurudisha mahusiano kati ya kanisa na marekani, na walifanikiwa sana. Lakini mwanzoni mwa miaka ya 2000, kuna chokochoko zilifanywa na waliberali wa Marekani, ambao walitaka Kanisa katoliki nchini humo lidhibitiwe na kuua ushawishi wa Vatican. Safari hii Pope hakuongea chochote, wala hatukusikia lolote likiongelewa kutoka Vatcan, badala yake wale maaskofu na Mapadri walijihusha na kashfa za wale watoto ndiyo waliosimama na kuionya marekani iangalie sana hatua wanazojaribu kuzichukua, na waliilaumu CIA kuwa either haipo makini au imeamua kufanya mchezo wa hatari kwa taifa la Marekani.
Kauli ya baadaye na iliyosikika ni ile ya Polycap Cardinal Pengo wakati akiongoza misa pale katisa la St. Joseph katika Jimbo Kuu la Dar es salaam akiionya Marekani kwamba kama inadhani ipo salama basi inajidanganya sana. Aliendelea kusema kuwa Marekani ilifainika na mbinu za kanisa katika kuua na kuusambaratisha ukomonisti, Marekani ilidhani kuwa imelitumia kanisa kitu ambacho wanajidanganya, Kanisa lilikua na interest zake ndani ya urusi, na kama kuna kosa Marekani ililifanya ni kushirikiana na kanisa.
Katika vikao vya ndani alikuja kusikika akisema maadam Marekani imeanza harakati ya kulidhoofisha kanisa basi kanisa halina jinsi, na hivyo kusambaratika kwa marekani ni suala la muda tu, na akasema ni taifa kubwa linahitaji muda kidogo ili mambo mengine yawe sawa, dunia iendelee kuwa na amani.
Kwa maelezo hayo huyo Mkuu
MALCOM LUMUMBA, mimi ni miongoni mwa ambao kauli zile bado zinaishi vichwani mwetu na tunajua siku za kuelekea ukingoni mwa taifa hilo zimekaribia sana.