Tukizungumzia kinadharia (au hata kikweli kweli), je hapa JF ni nani ambaye unaona ungeweza kutoka naye kama mtu na rafiki yake wa kimapenzi? Ni mwanachama yupi ambaye unaona au kudhani unaendana naye kiasi cha kama ungeweza au ingewezekana ungependa kutoka naye?
Hii mada ni kwa wote...akina dada pamoja na akina kaka. Haina maana kwamba ukisema ningependa kutoka na fulani basi huyo fulani ndio adhanie kuwa tayari umeshamkubalia
kutoka naye. Si hivyo hata kidogo ingawa kama wenyewe mkija mkielewana kihivyo baadaye basi hiyo itakuwa ni juu yenu.[/
QUOTE]
hahaha! Hii imekaa poa sana ila mimi ni kijana wa kiume mweupe na ni mgeni jf bado sijawajua wengi humu wala kujua kuwatofautisha kujua nani wa kiume au wa kike maana majina tunayotumia humu yote vitendawili na kingine sijajua jinsi ya kuweka picha jamii forum kama profile na jinsi ya ku PM. Thanx