Ungekuwa rais ungefanya nini?

Waheshimiwa sana wanajamvi, tumetumia muda wa kutosha kuilaumu serikali iliyopo madarakani na chama tawala kwa matatizo yanayoikibali nchi hii. Mimi ni mmoja wenu katika hili na naamini CCM na serikali yake inastahili kubeba lawama isipokuwa haiitakuwa kuishia kulaumu tu. Tuna wajibu wa kupendekeza nini kifanyike kujikwamu toka hapa tuliponasa. Hata kama wahusika hawatachukua ushauri wetu tutakuwa tumepanua zaidi fikra zetu kuhusu mwelekeo sahihi tunaostahili kuchukua kama taifa na kipindi kitakapofika tutajua kwa uhakika zaidi nini kifanyike.

Kama wewe ungekuwa raisi wa nchi hii ungefanya nini kukabiliana na haya:

- Mfumuko wa bei
- Ubovu wa elimu
- Huduma mbovu za afya
- Tatizo la jira - Hasa kwa vijana
- Kudorora kwa kilimo (ambacho tunaambiwa ni uti wa mgongo wa taifa letu)
- Rushwa (imekuwa na kuzaa ufisadi)

Naomba maoni yenu wanajamvi na si lazima uzungumzia vyote, unaweza kuchagua baadhi ukatoa maoni yako.

Natanguliza shukrani zangu

Bolivar

Hayo uliyoorodhesha ningeyapiga chini niende zangu Jamaica kupembea!!!!!
icon14.png
 
Usitutafute ushauri kwa njia za kilaghai wakati wapo watu rsmi kunawalipa kw kodi zetu kufanya kazi hiyo hiyo kwa uongozi hapo Magogoni.

Wameshauriwa mara ngapi hadi leo huku wakituona tu kama vile tunacharaza nyuzi za kwenye gitaaa????????????


Waheshimiwa sana wanajamvi, tumetumia muda wa kutosha kuilaumu serikali iliyopo madarakani na chama tawala kwa matatizo yanayoikibali nchi hii.

Mimi ni mmoja wenu katika hili na naamini CCM na serikali yake inastahili kubeba lawama isipokuwa haiitakuwa kuishia kulaumu tu. Tuna wajibu wa kupendekeza nini kifanyike kujikwamu toka hapa tuliponasa. Hata kama wahusika hawatachukua ushauri wetu tutakuwa tumepanua zaidi fikra zetu kuhusu mwelekeo sahihi tunaostahili kuchukua kama taifa na kipindi kitakapofika tutajua kwa uhakika zaidi nini kifanyike.

Kama wewe ungekuwa raisi wa nchi hii ungefanya nini kukabiliana na haya:

- Mfumuko wa bei
- Ubovu wa elimu
- Huduma mbovu za afya
- Tatizo la jira - Hasa kwa vijana
- Kudorora kwa kilimo (ambacho tunaambiwa ni uti wa mgongo wa taifa letu)
- Rushwa (imekuwa na kuzaa ufisadi)

Naomba maoni yenu wanajamvi na si lazima uzungumzia vyote, unaweza kuchagua baadhi ukatoa maoni yako.

Natanguliza shukrani zangu

Bolivar
 
Endelea ku-assume. Kama unataka michango makini, weka hoja makini na sio assumptions. Don't take things for granted and then ask for michango makini.

Lengo hapa ni kuchochea mawazo ya kutafuta ufumbuzi wa baadhi ya matatizo yanayoikabili nchi hii. Inaonekana suala la CCM kung'olewa madarakani limekugusa sana, LET ME TELL ONE THING, TUTAING'OA TU.
 
Haya ni masuala ya sera Bolivar.. Na hayana jibi moja tena la moja kwa moja. Mengine yanahitaji utaalamu wa wachumi,waweze kudadavua. Unajua unapokuwa Rais,unakuwa una ufahamu lakini shallow katika sekta mbalimbali,ndiyo maana unateua PM,na kisha kwa kushirikiana naye mnateua mawaziri. Na Urais unajua ni taasisi,si mtu.. Ndiyo maana hupati majibu ya kueleweka.
Sema hayo yamekaa kama ahadi jinsi ulivyoyaweka. Kwamba ntadhibiti mfumuko wa bei,nitaboresha huduma za afya,wakulima watapata pembejeo na bei nzuri za mazao yao,nitaboreshaa elimu,nitapambana na rushwa hasa kubwakubwa,nitazalisha ajira kwa vijana,wenye vyeti na wasio na vyeti.. Kitu cha namna hiyo B..
 
Wote tunafaham nchi yetu ina hali mbaya kiuchumi na Rais alitamka hivyo.
Madai yote ya madaktari yanahiyaji pesa kasoro la wakuu wizara kujiuzulu
je ungekuwa Rais ungefanya nini?.
Je watumishi wengine wa serikali unawaahidi nini?
nawasilisha
 
Wote tunafaham nchi yetu ina hali mbaya kiuchumi na Rais alitamka hivyo.
Madai yote ya madaktari yanahiyaji pesa kasoro la wakuu wizara kujiuzulu
je ungekuwa Rais ungefanya nini?.
Je watumishi wengine wa serikali unawaahidi nini?
nawasilisha

Kamati zishaundwa ishu inashugulikiwa unataka rais akurupuke wakati taratibu zinafuatwa. angekuwa padre angekurupuka; JK yuko makini kabisa si mkurupukaji
 
Ningekuwa Rais wa JMT ningefanya yafuatayo ili kupunguza matatizo ya migomo yanayoendelea nchini;
  1. Ningewakusanya viongozi wote wa vyama vya wafanyakazi na kuwaeleza hali halisi ya kifedha serikalini, na kujadiliana nao jinsi ya kuboresha maslahi yao kwa kuangalia hali halisi ya pato la taifa na kutoathiri utendaji wa kila siku wa serikali.
  2. Ningezuia kuongezwa kwa posho za wabunge kutoka 70,000 mpaka 200,000 kwa siku (na badala yake ningewaongezea kutoka 70,000 mpaka 100,000) na kuwaongezea madaktari kutoka TZS 10,000 mpaka 50,000.
  3. Ningesitisha uagizaji wa magari ya kifahari serikalini na kupunguza matumizi ya kawaida serikalini ili kupata kiasi cha fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za kijamii kwa kipindi kifupi.
  4. Ningeagiza taasisi mbalimbali za serikali kama vile TANAPA, NSSF na nyingnezo ambazo zina savings kubwa ku-transfer savings zao ili ziweze kusaidia utoaji wa huduma za jamii na baadae ningeshawishi itungwe sheria ya kuzilazimisha taasisi hizo zisijitegemee kifedha bali ziwe chini ya wizara ya fedha na fedha zote za taasisi hizo zisimamiwe na wizara ya fedha.
  5. Ningewawajibisha viongozi wote wanaoshindwa kusimamia wizara zao kama Waziri, N/waziri na katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii.
  6. Ningeitisha mjadala wa kitaifa ambao ungeshirikisha wadau mbalimbali kama viongozi wa vyama vya siasa, NGOs, Tume mbalimbali, mabalozi na wengneo ili kujadili namna ya kutatua matatizo mbali mbali yanayolikumba taifa letu na namna ya kuyatatua bila kuathiri utekelzaji wa ilani ya chama.
  7. e.t.c
 
ningewafuta kazi mara moja waziri .naibu wake .katibu na mganga mkuu,kwa hatua hiyo najua madaktari wangelegea .nawaagiza madaktari waanze kazi .uku tukijadili hatima ya madai yao .,
 
1. Ningewafukuza kazi Dr Hadji, Dr Nkya, Blandina Nyoni na Mtasigwa. Hii ni kwa ajili ya kujenga goodwill na madaktari kabla ya kuketi nao mezani.

2. Ningewaongezea madaktari posho ya night kutoka 10,000 hadhi 50,000. Hili ndiyo dai pekee ambalo wananchi wanalielewa kirahisi. Nikiwakubalia hili kabla hata ya kukaa mezani itawalainisha kabisa madaktari na kuwafanya wabia wazuri tunapoanza mazungumzo. Vile vile, wananchi wataona kuwa naelewa kinachoendelea

3. Ningeomba madaktari warudi kazini mara moja na wateue kamati yao ya watu 5 ambao watakaa na timu ya serikali kupitia madai. Madaktari waachwe huru kuchagua wawakilishi wao - serikali isije na hoja za "oh, Ulimboka siyo daktari"

4. Ningeteua timu ya vichwa vitano kuiwakilisha serikali kwenye mazungumzo. Hii timu itakuwa ya watu waliotulia na wasio na jazba au madharau. Wala wasitokane na vyeo vyao serikalini, bali uwezo wao wakua analytical. Labda wafuatao; Lukuvi, Simbeye, Kimei, Kafumu na Maajar.

5. TOR za negotiation team zitakuwa;

- Kupitia madai ya madaktari kwa nia ya kuainisha ambayo ni ya haki na kutupa yasiyo
- Kukubaliana madai yatayoshughulikiwa short, medium na long term
- Kushauri serikali mfumo ambao utazuia mtafaruku kama huu kutokea tena (k.m. kuundwa tume ya kudumu)

6. Negotiation team itarudisha report baada ya wiki mbili



 
Hebu assume nafasi ya urais kwa muda unadhani nani kati ya waliopo angefiti wizara zifuatazo?
1. Fedha
2. Mambo ya nje
3. Ulinzi
4. Mambo ya ndani
5. Nishati na Madini
6. Viwanda na Biashara
 
Hebu assume nafasi ya urais kwa muda unadhani nani kati ya waliopo angefiti wizara zifuatazo?
1. Fedha
2. Mambo ya nje
3. Ulinzi
4. Mambo ya ndani
5. Nishati na Madini
6. Viwanda na Biashara

Fedha - Professor Anna Tibaijuka
Mambo ya Nje - Vicky Kamata
Ulinzi - Zambi
Mambo ya Ndani - Kange Lugola
Nishati na Madini - Manyanya
Viwanda na Bishara - Likokola
 
1. Fedha - Kabwe Zitto
2. Mambo ya nje - J.Kikwete (Anaweza fanya hiyo pamoja na kuwa Raisi na hataonekana mtoro tena!)
3. Ulinzi - Sugu - Joseph Mbilinyi
4. Mambo ya ndani - Godbles Lema
5. Nishati na Madini - Mnyika
6. Viwanda na Biashara- Mdee Halima
7. Nitaunganisha Ujenzi na Uchukuzi nampa Magufuli
8. Sheria na katiba - Tundu Lisu
9. Mali asili na utalii - Wenje
10.Utawala bora - Msigwa
11. Waziri Mkuu - Freeman Mbowe - Lkini huyu apewe full powers si yule yupo hayupo
 
Hebu assume nafasi ya urais kwa muda unadhani nani kati ya waliopo angefiti wizara zifuatazo?
1. Fedha
2. Mambo ya nje
3. Ulinzi
4. Mambo ya ndani
5. Nishati na Madini
6. Viwanda na Biashara

kuna wizara 3 nyeti umeziacha, TAMISEMI, Ardhi na Menejimenti ya Utumishi wa Umma nazo zina kashfa kami vile mishahara hewa. Binafsi napata kigugumizi kwa sababu simuoni mwenye ahueni zaidi ya Magufuli na Mwanri
 
Back
Top Bottom