In JK's shoes - in perspective, nimejivika uprezdaa......na sasa niko Mtwara.
1. Naitisha Kikao cha Viongozi wa Mkoa, napewa Taarifa na kuhoji hatua zilizochukuliwa kabla na baada ya fujo na uharibifu wa mali na madhara kwa maisha ya watu kadhaa.
2. Naitisha kikao cha viongozi wa makundi yote ikiwemo vyama vya upinzani, wanawake, vijana,wazee, bila kusaha viongozi wa kidini wa Mkoa, na kuwasikiliza kwa kina hoja zao kuhusu Bomba la Gesi kutoka Mtwara kwenda Dsm.
3. Napima hoja za wana-Mtwara na mustakabali wa maendeleo yao kutokana na raslimali zilizoko katika Mkoa wao na maendeleo ya Taifa zima kwa jumla.
4. Nafikia maridhiano na wanchi wa Mtwara juu ya uendelezaji wa miradi ya kuvuna raslimali, faida ya moja kwa moja kwa wananchi wa Mtwara na jinsi watakavyofaidi kutokana na vyanzo hivyo vipya vya mapato katika mkoa wao.
5. Napanga muda wa kufikia malengo yaliyoazimiwa na kuridhiwa na wana-Mtwara, wananchi wanaeleweshwa na hadi hapo hali itakavyoniridhisha kuwa tumekubaliana na tumeelewana, ikibidi kukaa Mtwara majuma mawili hakuna shida, cha msingi ni suluhu ya kweli ipatikane.
6. Hatimaye mambo yanakuwa shwari na tunaelekea kwenye Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
7. Nawasiliana na BAKWATA, Baraza la Idd kitaifa lifanyike Mtwara, nami naenda kushiriki na wana-Mtwara kula Idd-el-Fitri ili kujenga mahusiano mazuri na kuonyesha kuwa nawajali na kuwasilikilza shida zao.
8. Natoa maelekezo kwa viongozi wote wa Mkoa yote nchini Tanzania, kuhakikisha kuwa wanakuwa karibu na wananchi na kuwa na mikutano ya kusikiliza kero zao walau mara moja kila mwezi.
Mengine yanabakia kuwa kazi ya utekelezaji, na gesi ya Mtwara inaendelea kuzalishwa kwa maslahi ya kizazi hiki na kizazi cha baadae.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika!