Ungekuwa rais ungefanya nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ungekuwa rais ungefanya nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtazamaji, Feb 27, 2010.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,971
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 0
  Wana jamvi tupeane changamoto kila mmoja ajiulize angekuwa ni Rais wa Jamuhuru angefanya nin.

  Nimeona hili ni swali na msingi kwa kuwa inawezekana watalawala, washauri, na waaamuzi na sisi wenyewe katika ngazi mbali badala ya kutatua KIINI cha tatizo tuemkuwa tukijaribu na kupapasa kutatua MATOKEO ya MATATIZO HALISI.

  Mfano kwa mtazamo wangu kashfa kama za EPA,RICHMOND,RADAR, BOT TWIN TOWER, JENGO LA UBALOZI ROME na mengine mengi ni matokea ya tatizo fulani.

  Je kama rais zaidi ya kuhakisha matokea ya KASHFA yanatatuiwa ungefanya nini ili chanzo chake kifungwe kabisa?

  Mtazamo wangu matatizo yote haya chanzo halisi ni MFUMO. Na Huu mfumo unasababisha tatizo la UWAJIBIKAJI.

  Kutatua tatizo hili mimi kama rais nitabadilisha MFUMO wa kuwapata wahusika wa baadhi ya vyeo vya juu Vyeo kwenye wizaara ,idara na mikowa kuwa vya kutangazwa ili KUSAILIWA badala ya KUTEULIWA

  Ningefanya mabadiliko haya
  1. Ningeteua Jaji Mkuu kutokana na application walizofanya majaji

  2. Makatibu wakuu wa wazira nao ningewateua kutonana na application walizoomba wale wanajiona wanaweza

  3.Makatibu Tawala wa Mikoa na wakurugenzi pia zingekuwa nafasi za kusailiwa

  Dhana hii hata kama sio kwa kiasi kikubwa naamini ingechochea uwajibikaji na kuwafanya wahuskia waliochaguliwa kutokana na usahili kufanya kazi kwa profesion ethics zaidi na KUJIAMINI.

  Pili kuondoa mlolongo wa nafasi za juu kwenye wizara, idara kushikwa na watu wanaoteuliwa tu. ( Mfano Waziri , Katibu mkuu na wakurugenzi wa wizara wanateuliwa ) Nadhani taasisi yenyeny viongozi watatu ni wa kuteuliwa ni manzo wa UZEMBE na KUTOKUWAJIBIKA.


  Haya virtual president u re in office lets see the vision of of each one of us.
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Jambo kubwa ni kuwakamata wote wenye tuhuma za ufisadi na kuwafunga mara moja na wale wanaibia Taifa letu, na kufanya serikali iwe accountability kwa watu na sio watu kuwa accountability kwa serikali
   
 3. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mh kazi kweli kweli!!
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,227
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Raisi alichegaguliwa toka chama gani Ccm, Cuf ,Chadema, Nccr au mgombea binafsi? Nauliza kwa sababu madaraka ya raisi yako kisheria na kikatiba sidhani kama anaweza kufanya nje ya hivyo
   
 5. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #5
  Feb 27, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  1. Tanzania ingeondoka leo hii toka EAC
  2. Tanzania ingeondoka leo hii toka EAC
  3. Tanzania ingeondoka leo hii toka EAC
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,971
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 0
  kweli kabisa kuwafunga ni sawa lakini unadhani ungefanya nin hasa ili kuziba hiyo mianya ya hao mafisadi kufisadi,
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,971
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 0
  Ni changamoto kama wewe ungekuwa rais unfenya nini.bila kujali itiakadi
   
 8. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kwanza kuunda Katiba upya na watu wote kushiriki na sio sasa hivi ile ile ya mwaka 1977 na kufanyanyiwa marekebisho, mbaya sana,Kuchukua mawazo yote ya Upinzani na kufanyia kazi na kuleta matokeo mazuri katika jamii yetu
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Matatizo yote haya ya mfumo yanatokana na katiba isiyoendana na wakati yaani katiba mbovu. Ili kubadisha mfumo ningefanya utaratibu wa kuindika katiba ya nchi upya ambamo mambo yote ya mgawanyo wa madaraka yangejadiliwa na jamii kwa kina. Wananchi wangehusishwa kikamilifu katika kuiandika katiba hiyo!!.
   
 10. B

  Bolivar JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Waheshimiwa sana wanajamvi, tumetumia muda wa kutosha kuilaumu serikali iliyopo madarakani na chama tawala kwa matatizo yanayoikibali nchi hii. Mimi ni mmoja wenu katika hili na naamini CCM na serikali yake inastahili kubeba lawama isipokuwa haiitakuwa kuishia kulaumu tu. Tuna wajibu wa kupendekeza nini kifanyike kujikwamu toka hapa tuliponasa. Hata kama wahusika hawatachukua ushauri wetu tutakuwa tumepanua zaidi fikra zetu kuhusu mwelekeo sahihi tunaostahili kuchukua kama taifa na kipindi kitakapofika tutajua kwa uhakika zaidi nini kifanyike.

  Kama wewe ungekuwa raisi wa nchi hii ungefanya nini kukabiliana na haya:

  - Mfumuko wa bei
  - Ubovu wa elimu
  - Huduma mbovu za afya
  - Tatizo la jira - Hasa kwa vijana
  - Kudorora kwa kilimo (ambacho tunaambiwa ni uti wa mgongo wa taifa letu)
  - Rushwa (imekuwa na kuzaa ufisadi)

  Naomba maoni yenu wanajamvi na si lazima uzungumzia vyote, unaweza kuchagua baadhi ukatoa maoni yako.

  Natanguliza shukrani zangu

  Bolivar
   
 11. MANI

  MANI Platinum Member

  #11
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,616
  Likes Received: 2,260
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa nimeshindwa kutimiza ndoto za raia wangu ningepisha wengine wenye uwezo!
   
 12. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kuzunguka dunia nzima kwa hela za walipa kodi wangu
   
 13. Mzee Dogo

  Mzee Dogo JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Ningenyonga mafisadi wote!
   
 14. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 885
  Trophy Points: 280
  Ningekuwa Rais wa hii nchi, kitu cha kwanza ambacho ningekifanya ni ku-extinguish nchini watu kama nyie. Tumekuwa watu wa kulalama 24 hours, 7 days a week. The worse thing, watu tunalalamika bila hata kuchukua hatua yoyote. We expect someone to do it for us. Thanks at least kuna mtu ka-note hili: Tanzania has become a nation of complainers *- Magazine*|theeastafrican.co.ke

  Suala sio kama wewe ungekuwa Rais ungefanya nini. Suala ni kama wewe ni Mtanzania unafanya/umefanya nini kuhusiana na hayo matatizo uliyolist hapo. Kama umeshindwa kufanya chochote, then stop complaining.
   
 15. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,937
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 160
  Njngepiga picha na akina 50cent ili nikistaafu albam yangu iwe ya kuvutia.
   
 16. B

  Bolivar JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Sehemu kubwa ya michango indirect inalenga serikali na rais aliyepo, let forget about him and his CCM government, assume tumeiondoa CCM madarakani tunakabiliana na matatizo iliyotuachia!

  Naomba michango makini tuweke mzaha pembeni
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  dawa ni kufufua viwanda vilivyokufa mf nyumbu,tanganyika pakers etc na kurudisha sera ya ujamaa.uchumi umilikiwe na wananchi wenyewe.
   
 18. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 885
  Trophy Points: 280
  Endelea ku-assume. Kama unataka michango makini, weka hoja makini na sio assumptions. Don't take things for granted and then ask for michango makini.
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,503
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Wamtumie lipumba kwenye kuinua uchumi wetu
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,503
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Wamtumie lipumba kwenye kuinua uchumi wetu kwa kuweka siasa pembeni na kuamua kuijenga Tz
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...