Unga Unga wapelekwa kwa mkemia mkuu

Kwa wale wakuu wa JF niliowaudhi hadi nikafungiwa...Naomba niwaeleze kuwa sitoruka tena anga zenu...Ila bosi wenu mi nayeye kule facebook halafu tuone kama facebook nao watanifungia!
Kwa wale wazalendo...Muendeleze mpambano huu hapa jf kwa niaba ya wanyonge hadi kieleweke!
 
Na Joyce Magoti

JESHI la Polisi nchini limewasilisha kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, vumbi na mfagio uliotumika kusafishia ukumbi wa Bunge ili kufanyiwa uchunguzi wa kina kubaini kama kulikuwa na kemikali za sumu.

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini, Bw. Peter Kivuyo, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya mmoja wa wabunge kunaswa na kamera za Bunge akionekana kumimina vitu katika viti vya baadhi ya wabunge vikiwamo vya Spika na Naibu wake, vitu vinavyodaiwa kuwa ni uchawi.

Hali hiyo ilileta hofu kwa wabunge na wananchi kwa ujumla na kulihusisha tukio hilo na la kuugua ghafla kwa Mbunge wa Kyela Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa kikao cha Bunge. Dkt. Mwakyembe tayari amekanusha ugonjwa wake kuhusishwa na tukio hilo.

Bw. Kivuyo alisema Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa taarifa hizo na kwamba tayari takataka walizofagia zimekusanywa na kupelekwa kwa Mkemia Mkuu kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu utakaosaidia kuondoa utata uliopo.

"Bahati nzuri takataka zilizofagiwa siku hiyo hazikumwagwa na hivyo tumezichukua pamoja na ufagio uliotumika kusafishia ukumbi na kupeleka kwa Mkemia Mkuu ili aweze kufanya uchunguzi wa kina ambao utasaidia kuondoa utata," alisema Bw. Kivuyo.

Bw. Kivuyo aliongeza kuwa hadi sasa hana tarifa zozote za mtuhumiwa wa tukio hilo kuhojiwa na Jeshi lake, bali kazi hiyo si yake inapaswa kufanywa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma.

Inadaiwa kuwa wiki iliyopita kamera za Bunge zilimnasa mbunge akiwa na ofisa wa Bunge akimimina vitu vilivyodaiwa kuwa ni uchawi katika viti vya wabunge kikiwamo cha Dkt. Mwakyembe ambae aliugua ghafla wakati wa kikao cha Bunge.
Sorce majira
 
jamani sio unga uliukutwa kwenye viti ndo umepelekwa kwa mkemia bali ni vumbi ambayo ilichukuliwa baada ya kufagia ukumbi!
 
Hii inanikumbusha hadithi niliyowahi kuisoma kwenye mtandao: Kuna jamaa walikuwa wameiba benki Sweden. Wakati wanatoroka mmoja wao akasema, " nina habari mbaya ya kuwaambia, polisi wako nyuma yetu." Akaangalia tena, akasema," nina habari nzuri za kuwaambia, ni polisi wa kiswidi".

Kuna uhakika gani kuwa hilo vumbi, unga havikuweko kabla ya mheshimiwa Chenge kuingia ukumbini? Tuna uhakika gani kuwa hii vumbi haikutokea baada ya mheshimiwa kuingia ukumbini? Kuna uhakika gani kuwa vyombo vilivyotumiwa kukusanyia na kuhifadhi ushahidi vilikuwa sterile? Kwa nini uchunguzi ufanyike Ocean Road na sio kwenye maabara ya polisi? Au hatuna? Mimi hili suala naona ni kupotezeana wakati na lolote litakalopatikana litaonekana na walakin. Mahakama ya wananchi imeishaamua na haya mengine hayatabadilisha kitu.
 
they perfectly know that ile si sumu bali ni uchawi.
kwa sababu unga huo alokuwa akiumwaga chenge yeye mwenyewe hajajikinga kwa gloves wala masks, kweli pana sumu hapo/
sita alijua kuwa pale ni uchawi, na uchawi ukigundulika huwa haufanyi kazi ndio maana akasema bunge liko salama.
polisi kwa vile hawaamini uchawi na wamebanwa kila kona wanasema watafanya uchunguzi sana sana watakachogundua kuwa ni unga wa miti shamba. as simple as that.
 
Press Releases - Embassy of the united states
http://tanzania.usembassy.gov/pr_01262007a.html

24 Tanzania Police Force take forensic course

January 26, 2007


Forensic experts from the U.S. conducted a two-week training course recently on marijuana analysis for 24 Tanzania Police Force (TPF) participants who had a chance to do hands on work with microscopes and chemical testing as well as document examination in the analysis of typewriting and comparison of documents using Typewriters.

According to a statement from the U.S. Embassy the experts who conducted the training are Terry Mills, a Forensic Chemist. Mills is a retired head of Georgia State Crime Laboratory and has written a definitive chemistry handbook and Meredith Dekalb, a Forensic Document Examiner. Dekalb was a former Document Examiner with the FBI.

The U.S. government through Carla Noziglia, Senior Forensic Advisor has been conducting training, installing instruments and equipping the laboratory since 2002. The TPF on the other hand has renovated its forensic laboratory, and with the equipment and training provided by the U.S. a full service, state-of-the-art forensic laboratory is expected. The on-going programme is envisioned to be completed in 2009.

Noziglia said so far 122 police officers have received basic and advanced training on Fingerprint, Latent print, Firearms and Scenes of Crime. "Training on Forensic Chemists started last year with a batch of 14 participants and more training are expected this year," Noziglia said.
She also said 27 districts in the country have been provided with cameras and crime scene kits. Other equipment donated by the U.S government to the laboratory include two gas chromatographs, an FTIR, six microscopes, four balances, two centrifuges, a superglue fuming cabinet, 55 file cabinets for 10 print cards, and fingerprint supplies.

The Forensic Laboratory will have additional sections in Chemistry, Toxicology, Trace and Biology. The laboratory is part of a cooperative agreement on law enforcement signed between the United States and Tanzania, in which the two pledge to raise the standard of law enforcement in Tanzania through training, equipment, and the construction of the laboratory.

kaswali: Hii Lab kwa hiyo ni kiini macho????????????
 
Kama Joti (JK) amewasafisha watuhimiwa wa Richmond na mwizi MKAPA kakusema aache apumzike ataacha mkumsafisha mumwagasumu/muuaji/vijisenti/anapeleka suti dry cleaner Uk zikafuliwe/mwizi/mzee wa majivuno/ mzee mpenda chini/mchawi???????????????????


Duh,ha ha ha! wewe mkuu ukisikika usinitaje (jokes).


Mkuu uliyosema ni kweli kabisa.Kama Mzee wa Kiwira,baba NET GROUP,Mjomba Bank M,na Shemeji ANBEM company na Baba mkubwa Kiwira coal Mining aliweza kulindwa na kusafishwa na Uncle RICHMOND Kikwete,ni kwanini huyo mjomba niliyembold hapo juu asilindwe?
 
Duh,ha ha ha! wewe mkuu ukisikika usinitaje (jokes).


Mkuu uliyosema ni kweli kabisa.Kama Mzee wa Kiwira,baba NET GROUP,Mjomba Bank M,na Shemeji ANBEM company na Baba mkubwa Kiwira coal Mining aliweza kulindwa na kusafishwa na Uncle RICHMOND Kikwete,ni kwanini huyo mjomba niliyembold hapo juu asilindwe?


kaka huu ni mduara tuu watazunguka watasikia kizungu zungu halafu wataanguka wenyewe... tusubiri utayaona tuu....
 
Basic facts so far:

1. Ni kweli kuwa kuna mbunge aliyeingia ndani ya bunge kwa siri na kumwaga "substance"..unga?....Swali siwalikanusha?Hata kama hapatakuwa na tatizo kwa "unga". Hakuna sheria ya adhabu dhidi yake? unga alikuwa ansonaga ugali humo ndani?

2. Ni kweli kuwa Polisi wanaafiki kuwa kuna subsatance...Hiyo inafanya hoja ya wali kuwa Valid. Chiligati aliposema kuna Mbunge alye kuwa waziri..anatafuta kiti...anaonaje polisi wanachosema sasa....alikuwa anatafuta kiti kwa unga? Chiligati Njoo hapa na ujiweke sawa.

3. Ni kweli kuwa siku ya kwanza ya tukio lilipotokea JF iliitaka serekali, mkemia mkuu, Vyuo vikuu na maprofesa wake, toxologist, Chemists na radioactive experties..Waende mara moja kuchukua sample pale bungeni..Swali? Kwa nini wachelewe kiasi hiki? Kwanini Huwa hawafuatia ushauru wa msingi unaotolewa hapa JF? kama vyombo vingine vya habari vinachota habari hapa..kwa nini hawa wataalamu wanafikicha vidole na kujiuliza .... Next time wasirudie Makosa. They should take JF seriously from now onwards!!

4. Ni nani huyo ameona kuwa ni muhimu kuchukua sampuli hizo sasa. tunaomba Jina lake. Na wadhifa wake.WHY?

Ili Tumshauri Raisi AMFUKUZE KAZI NA AFUNGULIWE mashitaka.

4.1 Alikuwa wapi siku ya kwanza tukio lilipotokea asitoe ushauri huo?
4.2 sampuli za kazi gani? je wakikuta zina radioactive materials ..na wabunge wamesha kuwa contaminated? atajiitaje mtaalam.Bado anafikiri abakie kazini?
4.3 Kwa nini asingemshauri spika kuwa hiyo nyumba isitumike mpka sampuli zitoe majibu? Ni upuuzi kiasi gani kuendelea kukaa pale alafu sampuli ziko kwa mkemia..? kama pako contaminated? You see... its all so stupid!!
4.4 sheria za kimataifa za uchukuaji wa sampuli mahali kma pale ..zinasema bado pawe panatumika? Oh My God!!
4.5. Atatoa sababu gani za kitaalam za kuwaacha wabunge mlendani huku akiwa ana proceed na analysis?

5. Mkemea Mkuu anazichukua kwa confidence ya range gani? atapoint hizo error za sampling? Ameshutumu upuuzi uliofanywa kwa host of the building? ameona kuwa mambo yamepelekwa kidini zaidi ya kisanyansi? Asumptions kuwa" unga" hauna active substance..hivyo wakae tu..maana hakuna tatizo...is that science? Its realy folosh. Hata kama unga hautakuwa na madhara na utakuwa ni unga wa dona..Bado Its exrimly folish. Huwezi kufanya science kwa kubunia bunaia kiasi hiki.

Ni upuuzi kufikiri kuwa hilo zoezi lina maana:

kama liko kivipi?
 
wanapotosha ushahidi sasa subirini tutasikia ni mchanga tu au vumbi la kawaida....kama kawaida yao usanii saaaaaaaana nyuma ya pazia.
 
Majibu ya Mkemia yanajulikana haikuwa sumu wala madhara kwa binadamu, changa la macho....

Ushi
 
bwana Peter kivuyo,hufai hata kwa kulumangila,kama ndio ninyi mnao tegemewa na taifa basi ndio maana hakuna tunalofanikiwa.Ni aibu tena kubwa na ya mwaka kusema maneno kama hayo mbele ya waandishi makanjanja ambao nao wamekuwa kama wabunge wa ccm wanaoshindana kugonga meza bungeni.
Hivi hata mtu mmoja hakumuuliza swali la kijinga tu.iweje ukumbi uendele kutumika wakati bado uchunguzi unaendelea.
 
huu unga unga unaosemwa, haujawai kweli kutumika kwenye malaria aliyowahi kuwa nayo mama Anne Malecela mwezi wa february hivi? naye kuna jambo aliliibua bungeni mara kaumwa ghafla.
ni fikra zangu tu
 
jamani watu tunamiss point muhimu hapa!!HIVI kiongozi mkubwa (MBUNGE) kama CHENGE anatembeaje na Vumbi mkononi??haiingii akilini hata kidogo.
Kama CHENGE sie aliekuwa na VUMBI hilo, je hao wanaolipima wamelitoa wapi??
na kama wamelitoa bungeni, na imethibitika alieliweka ni CHENGE, swali kwa chenge:inakuwaje na kwa sababu gani mtu mzima kama yule anaenda mwaga vumbi kwenye viti vya wabunge wenzie??
siamini kama vumbi hilo kaliokota nje ya ukumbi wa bunge,kamasivyo, kokote alikolitoa,kapanda nalo gari,kaingia nalo kwenye bunge letu tukufu-vumbi bado liiko mkononi.duh!
Basi hili vumbi kwa kweli lilikuwa na umuhimu mkuwa sana KWA MHESHIMIWA CHENGE.kwa nini??
 
huu unga unga unaosemwa, haujawai kweli kutumika kwenye malaria aliyowahi kuwa nayo mama Anne Malecela mwezi wa february hivi? naye kuna jambo aliliibua bungeni mara kaumwa ghafla.
ni fikra zangu tu

ehh ? yaani siku hizi watu wanatumia "unga" kama "style" sio ?....eh kweli nakubali nimeachwa njiani na hiyo style.
 
Inaonyesha ukumbi ulifagiliwa na takataka zote zilipelekwa kwa uchunguzi.Sidhani kama kumekusudiwa vumbi ambalo labda lilitokana na hao Vampire waliovamia ukumbi saa sita za usiku.
 
Wakuu,
Chenge ni fisadi lakini kwa hili la UCHAWI mimi nashindwa kumuhukumu kwani inahitaji uwe na imani ya KISHIRIKINA ili uweze kufanya hivo. Nashindwa ku-imagine hata hawa police wamedhamilia kufanya kitu gani cha maana baada ya uchunguzi wa ile sample ya 'VUMBI' lililopelekwa kwa Mkemia Mkuu wa serikali! Wanachokifanya polisi ni usanii tu!

Karibu kila Mtanzania anafahamu kwamba kuna tukio limejitokeza bungeni ambalo linahusishwa na imani za KISHIRIKINA. Kwa kifupi ni kwamba wabunge na baadhi ya watanzania wameamini kweli kwamba mzee wa vijisenti alikusudia ama kuwadhuru wabaya wake bungeni, au kujisafisha madhambi yake kwa njia ya KISHIRIKINA.

Ninachofahamu ni kwamba, Maabara ya Mkemia Mkuu HAINA vipimo vya UCHAWI kwa maana ya UCHAWI. Narudia tena HAINA. Kitu pekee inachoweza kufanya ni kujua kama hilo vumbi ni KEMIKALI au la, na si vinginevo.

Pamoja na kwamba KEMIKALI inaweza ikatumika kwenye tendo la UCHAWI lakini pia nafahamu fika kwamba UCHAWI ni NGUVU ambayo ni MATOKEO au ni ZAO linaloweza kutokea baada ya kuchanganya KEMIKALI na IMANI ya KISHIRIKINA. IMANI YA KISHIRIKINA iliyokomaa ni kiungo muhimu sana hapa, vinginevo utaambulia kupata KEMIKALI tu na si UCHAWI.

Sisemi kwamba kilichotokea bungeni si uchawi, la hasha. Point na swali langu hapa ni kwamba, kama uchunguzi wa Maabara ya Mkemia Mkuu utabaini kweli kwamba lile VUMBI ni KEMIKALI, je, polisi watawezaje kusema waziwazi kwamba TUKIO LA MZEE WA VIJISENT LILIKUWA NI USHIRIKINA??!!

Ikumbukwe kwamba serikali yetu ya ccm kwa muda mrefu sasa imekuwa ikidai kwamba HAIAMINI USHIRIKINA! Pamoja na kutokuamini huko, ni ukweli uliowazi kwamba tumekuwa tukisikia au kushuhudia matukio mbalimbali yanayodhihilisha kwamba viongozi wetu wa SERIKALI WANAAMINI USHIRIKINA tena kwa kiwango cha juu. Mfano mzuri ni hili tukio ililotokea bungeni ambapo tumeshuhudia wengi wao wakiogopa hata kuingia kwenye ukumbi wao wa bunge kwa KUHOFIA USHIRIKINA WA MZEE WA VIJISENT!

Binafisi naishauri serikali na bunge kutunga sheria itakayosimamia kisheria IMANI YA USHIRIKINA ili wahusika wa ushirikina kama mzee wa vijisenti na wengine wote wanaowaua VIKONGWE huko Shinyanga na Mara waweze kushugulikiwa kisheria na HAKI itendeke. Vinginevo imani ya uchawi itazidi kushamiri na wachawi watazidi kutesa kwa kukumbatiwa na serikali ya ccm inayodai kutoutambua ushirikina.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
ndio sasa wananchi tukubali kuwa ule ulikuwa ushirikina habari ishe.
ushirikina nadhani si kosa kisheria. na kuingia bungeni kwa taratibu/ kibali si kosa kisheria.
hapa chenge kama alikuwa na ruhusa ya kuingia bungeni, hata kama kamwaga unga wa kishirikina basi hana kosa kisheria.
 
Back
Top Bottom