Unga mkono JWTZ kulinda mipaka ya Nchi yetu!

Wana uhusiano gani na Jeshi la Israel?

Wanao uhusiana wa kijeshi, kama sisi tulivyo na uhusianoo wa kijeshi na China, USA, na Cuba!

Wao hasa wakiwatumia Israeli kuuziwa vifaa vya Kijeshi

Kati ya ndege 14 walizonazo 8 wameuziwa na Israel, 2 na Uingereza, 2 waririthi baada ya Uhuru!

Wana sub Marine 4 mbili mpya walizonunua toka USA mbili wamerithi tangu uhuru,

Wanalo jeshi hai la watu 25,200. Makomandoo wasiozidi 30,

Kumbuka Tanzania ndio nchi pekee barani Afrika yenye makomandoo wengi zaidi zaidi 3500 idadi ambayo ni sawa na makomandoo wa Ufaransa, ungufu kidogo ya makomandoo wa UK na zaidi ya hayo Tz pekee tuna kiwanda cha kutengeneza silaha zetu za kivita mfano Mabomu, Sub Marine (zipo sasa), Magari nk!
 
Nani mwenye hizo ramani zenye utata tuzione?, maana hapa kuna utata, wengine wanasema kuna ramani zinaonyesha lake hipo Malawi na nyingine zinaonyesha lake lipo Malawi na TZ
Raman zote dunia zimeandika ziwa Malawi, hata kwenye records the genesis wameandika lake Malawi. Hilo jina lake Nyasa linatumika hapa Tanzania tu.
 
Vita sio suluhisho! Ikiwezekana hilo suala lipelekwe kwenye mahakama ya kimataifa inayosuluhisha migogoro.
 
Mahali popote palipo na utajiri wa madini, mafuta au gas, ni lazima wazungu watawapiganisha tu ili wakamue utajiri wenu vizuri! Hebu tazameni Congo! Sasa na Tanzania ndiko tunakoelekea baada ya habari njema ya utajiri wa uraniaum na gas!
 
Ni kweli kabisa, watu wengine wanadhani VITA ni kama bajeti ya sherehe za UBATIZO/KOMUNIO/KIPAIMARA/KITCHEN PARTY/SEND-OFF au HARUSI.

Hii nchi iko HOI, KIUCHUMI.

My take:
VITA SI LELEMAMA,
NA
KWA VIJANA WENGI HAKUNA UZALENDO.

Mkuu usiwe mwoga kiasi hicho mwishowe watakuja kukuchukulia hata mkeo kwa kigezo cha umasikini. Malawi lazima watambue ziwa nyasa ni mali ya Tanzania pia na hatuwezi kuwaacha kwa hili.
 
Siwezi kuunga mkono ili swala, hivi unajua ndani ya tanzania kuna ardhi ambayo siyo mali yetu? Ambayo viongozi wetu wameuza kwa mataifa ya kiarabu toka enzi za Mwinyi?

Ziwa Nyasa ni mali ya Wamalawi,kwa nini unataka tumwage damu kwaajili ya kuwanyanganya wa Malawi ardhi yao? Ingali tunashindwa kusimamia ardhi yetu inayochukuliwa na wageni kila uchao?

dishi lako limeyumba..pumbav.
 
hako kamama kameona kikwete hawezi maamuz magum ndio maana kameamua kutikisa kiberit.
ANGALIZO-
1.Kikwete asitegemee vita kuwa rahisi kutokana na majeshi kutokuwa na umoja. Hii ni kutokana na kutofautisha maslahi ya majeshi hayo. JWTZ posho juu mishahara juu kushinda Majeshi mengine tafauti kabisa na kipindi cha Nyerere.
2. Kitendo cha kusafiri mno nje ya nchi kuomba misaada ni kitendo kinachoonesha kuwa yuko weak kiutawala.
3. Asitegemee uzalendo kutokana na yeye mwenyewe c mzalendo.
 
Dhambi ya kuunga mkono na kuhalalisha ushoga nchini mwake malawi ndiyo inayo mtafuna huyo mama Joyce, Akasome biblia ili ajue nini kiliizipata Sodoma na Gomora. Anawakaanga wananchi wake huyo. JWTZ songa mbele mimi nipo nyuma yenu.
 
Navichukia sana vyombo vya ulinzi vya Tanzania. Rasilimali za nchi zikichukuliwa na nchi jirani wanapandisha mori lakini zikichukuliwa na Mtanzania fisadi zikaenda kufichwa nchi jirani hawana Tatizo nao.
Hiyo sio kazi ya ya vyombo vya ulinzi bali ni ya jeshi la polisi na TISS.
TPDF kazi yao ndio kama hii inayotaka kuanza, yaani kulinda mipaka yetu
 
Iliwahi kusemwa kuwa "Unapokuwa unapigana na Mkeo/Mmeo ndani ya Nyumba ghafla Nyoka/Jambazi akaingia ndani ya nyumba mnayoishi, ni jambo la Kawaida ugomvi wenu kusimama na kuanza kumshughulikia adui/ Nyoka, na baada ya kumwondoa ndipo mnaanza kushughulikia tofauti zenu" nitakuwa wa mwisho kusema et ni sawa Hawa Mabwabwa wa Malawi wamege sehemu ya Nchi yangu kwa kuwa Tunatofauti za kiitikadi ndani ya Nchi yetu. Kama kijana mzalendo nipo tayari kwa vita kwa heshima ya Watanzania wa leo na wajao!
 
Iliwahi kusemwa kuwa "Unapokuwa unapigana na Mkeo/Mmeo ndani ya Nyumba ghafla Nyoka/Jambazi akaingia ndani ya nyumba mnayoishi, ni jambo la Kawaida ugomvi wenu kusimama na kuanza kumshughulikia adui/ Nyoka, na baada ya kumwondoa ndipo mnaanza kushughulikia tofauti zenu" nitakuwa wa mwisho kusema et ni sawa Hawa Mabwabwa wa Malawi wamege sehemu ya Nchi yangu kwa kuwa Tunatofauti za kiitikadi ndani ya Nchi yetu. Kama kijana mzalendo nipo tayari kwa vita kwa heshima ya Watanzania wa leo na wajao!

Safi sana mkuu kwapamoja tutalinda nchi yetu
 
Anyone who has ever
looked into the glazed
eyes of a soldier dying
on the battlefield will
think hard before
starting a war.
 
kuunga mkondo jeshi sio kusema tu bali hata kuingia hapa Jukwaani na mwelekeo ulio mzuri ni supporter pia.
Mimi ni Mtanzania lakini naomba Mh. Waziri Mathias Chikawe afute kwanza kauli yake bungeni kuwa wahusika wa EPA Tanzania hawahusiki lakini asipofanya hiyo, I feel so inferior to support our Jeshi japo inauma!

Pia mkuu Yeriko usijidanganye na 'ukubwa' wa jeshi maana la Ghadafi lilikuwa kubwa zaidi ya letu!


Nchi imejaa akili viazi.
 
Anyone who has ever
looked into the glazed
eyes of a soldier dying
on the battlefield will
think hard before
starting a war.

And so it is to anyone who has seen a fatal road or air accident will think twice before going on board an aircraft or a vehicle!
 
ner01a.jpeg

Map 5. Complete and closed game reserves in colonial Tanganyika, 1930. (Tanganyika Territory Survey Department Map 24/1/30, TNA 11234.)

Hii ramani ilichorwa mwaka 1930 je ni kwamba wachoraji walikosea kuonyesha mpaka wa ziwa nyasa?
 
(Msafiri, 2011) anaandika yafuatayo "Britain could have solved the border dispute between Malawi and Tanzania like it did the dispute between Malawi and Mozambique; however, Britain did not pay suitable attention to the issue on the Tanzanian side. Furthermore the British maps used while ruling both countries were ambiguous. Even today, maps are not reliable; some of them designate the boundary at the Eastern side of Lake Nyasa while others designate it at the lakes' midline as depicted in the 1937 map" (shown in Figure 1.)
AB7HWKgGSyZmAAAAAElFTkSuQmCC
GAAAAAElFTkSuQmCC

Na hii pia ilichorwa na waingereza mwaka 1937,

Hivyo hili suala si la kushabikia vita kichwa kichwa unaweza kuiingiza nchi katika hali ambayo tutaja jutia milele. Kwanini waingereza hawakuipatia Tanganyika sehemu ya Ziwa nyasa ili kuwapatia haki Watanganyika haki yao ya msingi ya kuvua, kusafiri, kujenga bandari kwnye sehemu ya ardhi yao iliyotumbukia ziwani? hapa panahitaji busara zaidi kuliko kutunishiana misuri.
AB7HWKgGSyZmAAAAAElFTkSuQmCC
View attachment Ramani.docx
 
Navichukia sana vyombo vya ulinzi vya Tanzania. Rasilimali za nchi zikichukuliwa na nchi jirani wanapandisha mori lakini zikichukuliwa na Mtanzania fisadi zikaenda kufichwa nchi jirani hawana Tatizo nao.[/QUO

Hiyo si kazi ya jeshi la ulinzi na usalama kimsingi, bali ni kazi ya Takukuru, Polisi na Usalama wa Taifa! Ukiikabidhi hata hiyo kazi kwa JWTZ vyombo hivyo vingine vinapoteza uhalali wa kuwepo!
 
Back
Top Bottom