Unga mkono JWTZ kulinda mipaka ya Nchi yetu!

Mimi ni mtanzania lakini kwa hili jambo niko tayari kuwaunga mkono wamalawi kwa hali na mali.
Ziwa Nyasa lote ni mali ya Malawi siku zote,
serikali yetu ilikuwa inajua siku zote na hata ulimwengu unajua siku zote, ukiondoa propaganda ambazo watanzania tumekuwa tukilishwa toka shule ya msingi kwamba ziwa Nyasa liko Tanzania wakati si kweli.

Vitisho na Nguvu za kijeshi haziwezi kutusaidia hata kidogo, hahitaji kuwa na jeshi kubwa na imara ili uweze kushinda vita siku za leo, kitu pekee ni kuwa na pesa za kuwekeza kwenye vita lakini pia kuungwa mkono na taifa kubwa lolote ambalo litafaidika na vita yenu, kitu ambacho wenzetu wa Malawi wameshafanikiwa kwa sasa.

Ninawashauri watanzania wenzangu tusiunge mkono juhudi zozote za kivita kwani hazina faida yoyote na wala hazina mchango wowote kwetu kwa sasa na hata baadaye.

Ninaishauri serikali yetu kwa sasa ijikite kutatua matatizo ya waalimu,madaktari pension za wastaafu,katiba mpya nk.

Askari waliopelekwa huko mimi siwashangai hata kidogo kwani hiyo ndio kazi yao na pili hao ni Mbwa wa watawala, wanasubiri kutumwa tu, swali kuu la kuwauliza askari wetu ni; walikuwa wapi wakati twiga na tembo wetu wakitoroshwa kwa ndege za kigeni tena za kijeshi au walikuwa wapi wakati Meli za mafuta za Iran zilipokuwa zinatumia pwani yetu huku zinapeperusha bendera ya Tanzania.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Malawi na ziwa lao.
 
uzalendo ndio kila kitu hapa suala la uvyama pembeni nchi ikishachafuka hakuna cha upinzani wala chama tawala watakaoishi kwa amani katika suala hili tusiwe kama..simba na yanga...ambao wako tayari kushangilia timu pinzani ilimradi tu wa nyumbani asishinde......
 
Yericko NI UJINGA SANA KUTAMBA KWA KUCHOKONOA VITA.kWENYE MABANGO YAKO MENGI NIMEKUWA NIKIKUUNGA MKONO LAKINI KWA ILI SIKUUNGI HATA KUCHA.Mimi ni askari by professional ingawa niliacha na kujiunga na kazi za kiraia za serikali, mantiki ya kuunga mkono vita haipo.Utakuwa uwendawazimu leo hii TANZANIA ITAINGIA VITANI NA MALAWI KWA AJILI YA MPAKA.vITA WATU KAMA WEWE WANAFIKIRI NI SHEREHE ZA HARUSI NA KUVISHANA PETE.NO.Kwa nchi kama hii ambayo imekwisha tafunwa na ufisadi wa kutisha ni MAFISADI TU NDIO WANASHANGILIA VITA ILI WAPATE MWANYA WA KUIFISADI NCHI VIZURI.CHAMA CHANGU MAKINI CDM NAOMBA KIWEKEZE KATIKA DIPLOMACY NA KUACHA KAULI ZA KIJINGA ZA AKINA MEMBE KUCHOKONOA VITA. NCHI HII HAINA UWEZO WA KIFEDHA KUWEKA JESHI KATIKA VITA ZAIDI YA WEEK 4 BILA KUFILISIKA RASMI.

Juhudi za kidiplomasia za kitaifa na kimataifa zikishindikana tuwaachie wachukue ardhi yetu kwakuwa hatuna hela kama unavyojenga hoja?

Kwamara yakwanza naisikia kauli ya aina hii ya kukatisha tamaa,

Kwataarifa yako mkuu ndani ya saa 48 kuanzia leo ikiwa Malawi itakaidi majadiliano vita itaanza rasmmi!

UNGA MKONO JWTZ kulinda nchi yetu mkuu, achana na mawazo hayo!
 
Last edited by a moderator:
kama tukichokozwa hatuna budi kupigana wahaya usema kolandibata ninkusindika! Ukinikanyaga lazima nikusukume!
 
haya sasa! mateja,vibaka, wafungwa ajira hiyoooo! mimi naomba RADIO ZOTE ZIPIGWE MARUFUKU KUPIGA NYIMBO ZA KISHAROBARO KWA SASA! BALI ZIANZE KUPIGA NYIMBO ZA KIZALENDO NA TV ZIONYESHE UZALENDO! ILI KUAMSHA STIMU ZA RAIA KILA KONA! AU KAMA VIPI TWENDE TUKAPIGANE KWA MIKONA RAIA WA MALAWI NA TZ
 
Siwezi kuunga mkono ili swala, hivi unajua ndani ya tanzania kuna ardhi ambayo siyo mali yetu? Ambayo viongozi wetu wameuza kwa mataifa ya kiarabu toka enzi za Mwinyi?

Ziwa Nyasa ni mali ya Wamalawi,kwa nini unataka tumwage damu kwaajili ya kuwanyanganya wa Malawi ardhi yao? Ingali tunashindwa kusimamia ardhi yetu inayochukuliwa na wageni kila uchao?

Ninakuunga mkono 100% Ziwa Nyasa ni la Wamalawi uroho wa nini??? Tulivyo navyo tumeshindwa kuvitumia,Bahari ya Hindi Samaki zinavuliwa bure tu! Victoria vile vile. Ninamuunga mkono Joyce Banda.
 
mkuu embu fafanua kidogo,nyasa ni mali ya malawi?? sijakuelewa!!! au unasema part ya nyasa ni mali ya malawi!!!??
 
Ninakuunga mkono 100% Ziwa Nyasa ni la Wamalawi uroho wa nini??? Tulivyo navyo tumeshindwa kuvitumia,Bahari ya Hindi Samaki zinavuliwa bure tu! Victoria vile vile. Ninamuunga mkono Joyce Banda.
ivi wewe kwenu malaw au?? au una mchumba huko??? sijaelewa una maanisha nini!!!
 
mkuu embu fafanua kidogo,nyasa ni mali ya malawi?? sijakuelewa!!! au unasema part ya nyasa ni mali ya malawi!!!??

Mkuu vijana wengi na hata wabunge wetu hawaiji vema mipaka yetu ya nchi,

Huyo ni mmoja wao! Lakini tuhamasishe uzalendo kwa nchi yetu na tulinde uhuru na mipaka yetu!
 
we jidanganye tu, vita ikianza mps wanapita kukamata maofisini kama nyie kuwapeleka mstari wa mbele...
niliwahi kuona hiyo kwa macho yangu kwa vita ya uganda, tofauti ya wakati ni kuwa sasa hivi itakuwa ngumu, kwani naamini uzalendo haupo tukianzia kwa viongozi wenyewe
 
Chini ya sirikali ya mr. dhaifu siko tayari kwenda mstari wa mbele kupigwa risasi
 
Yericko NI UJINGA SANA KUTAMBA KWA KUCHOKONOA VITA.kWENYE MABANGO YAKO MENGI NIMEKUWA NIKIKUUNGA MKONO LAKINI KWA ILI SIKUUNGI HATA KUCHA.Mimi ni askari by professional ingawa niliacha na kujiunga na kazi za kiraia za serikali, mantiki ya kuunga mkono vita haipo.Utakuwa uwendawazimu leo hii TANZANIA ITAINGIA VITANI NA MALAWI KWA AJILI YA MPAKA.vITA WATU KAMA WEWE WANAFIKIRI NI SHEREHE ZA HARUSI NA KUVISHANA PETE.NO.Kwa nchi kama hii ambayo imekwisha tafunwa na ufisadi wa kutisha ni MAFISADI TU NDIO WANASHANGILIA VITA ILI WAPATE MWANYA WA KUIFISADI NCHI VIZURI.CHAMA CHANGU MAKINI CDM NAOMBA KIWEKEZE KATIKA DIPLOMACY NA KUACHA KAULI ZA KIJINGA ZA AKINA MEMBE KUCHOKONOA VITA. NCHI HII HAINA UWEZO WA KIFEDHA KUWEKA JESHI KATIKA VITA ZAIDI YA WEEK 4 BILA KUFILISIKA RASMI.

Ni kweli kabisa, watu wengine wanadhani VITA ni kama bajeti ya sherehe za UBATIZO/KOMUNIO/KIPAIMARA/KITCHEN PARTY/SEND-OFF au HARUSI.

Hii nchi iko HOI, KIUCHUMI.

My take:
VITA SI LELEMAMA,
NA
KWA VIJANA WENGI HAKUNA UZALENDO.
 
Last edited by a moderator:
Niliwahi kuona uzi flani hapa JF kuwa Mwamunyange na JK hawaivi. sijui kama tofauti zao zilimalizika au ndo wanatupeleka mstari wa mbele tulambe risasi huku wao wanabishana wakiwa wamevaa bullet proof.
 
Nani mwenye hizo ramani zenye utata tuzione?, maana hapa kuna utata, wengine wanasema kuna ramani zinaonyesha lake hipo Malawi na nyingine zinaonyesha lake lipo Malawi na TZ
 
Tofauti ni jambo la kawaida hasa wakutanapo binadamu watimilifu,

Katika mgogoro huu UMOJA ndio ngao yetu!
 
Nani mwenye hizo ramani zenye utata tuzione?, maana hapa kuna utata, wengine wanasema kuna ramani zinaonyesha lake hipo Malawi na nyingine zinaonyesha lake lipo Malawi na TZ

Ramani za GOOGLE zote zinamapungufu, wameonyesha ziwa lote lipo Malawi, tafuta hapo hapo google mpaka wa Tanzania na Malawi KABLA ya 1914 uliowekwa na MJERUMANI na ambao ndio unaotambuliwa na serikali ya Tanzania!

Malawi wanatambua mpaka wa BAADA ya 1914 uliowekwa na MUINGEREZA,

Tofauti ni kwamba:

Swala la mpaka baina ya Tanzania na Malawi lina utata sana. Malawi hawana makosa kuhusu kuhama kwa mpaka ule, tatizo lao ni ukichwa ngumu kutotambua makosa kwenye mpaka huo. Mpaka wa awali ulikuwa unachukua ziwa lote na kuliweka chini ya German east Africa pamoja na sehemu kadhaa za malawi magharibi ya ziwa, lakini Rhodes aliyekuwa na maslahi huko Zambia hakufurahishwa na nguvu za wajerumani wakati huo na hivyo akaitaka serikali ya uingereza kuizuia Ujerumani isije ikamuingila katika ardhi yake huko Zambia. Makubalino ya awali yalikuwa ni kuwa ujerumani isiguse ardhi iliyoko magharibi mwa ziwa Nyasa; hata hivyo wakati wa kuandika mkataba wa Heligoland, hawakufikia mpaka solid baina ya nchi hizi mbili ingawa maandiko yalionyesha kuwa Ujerumani itaishia ufukweni, kulikuwa na kipengelea kuwa mpaka halisi utakuja amuliwa baadaye baina ya mamlaka za nchi hizo mbili. Makubaliano ya baadaye kuhusu mpaka huo yalitokea mwanozni mwa miaka 1900 kabla ya vita ya dunia ambapo walikubaliana kukata ziwa lile kati kati. Unfortunately hawakuweza kuenforce makubaliano yale sawasawa kwa kuwa pande zote hazikuwa na interest sana na raslimali za kwenye ziwa like; kwa hiyo ikawa kila upande una uhuru wa kulitumia bila masharti yoyote. Baada ya vita ya dunia ambapo Malawi na Tanganyika zilikuwa chini ya mwingereza ndipo makosa yalipoanza kwa vile mwingereza pamoja na kutambua makubaliano ya zwali kuhusu mpaka kuwa katikati alikuwa akichanganya kwenye documents na ramani mbalimbali za wakati huo: mara mpaka unakuwa katikati ya ziwa, na mara unakuwa pembezoni mwa ziwa. Wakati tunaelekea kupata uhuru kulikuwa na juhudi imara zilizofanywa na Chifu Mhaiki kuhusu kutatua tatizo lla mpaka ule kwa vile alikuwa anajua kuwa uingereza waliuhamisha kwa makosa; hata hivyo juhudi hizo zilizimwa kimakusudi, na kwa makosa sana na Nyerere ambaye alikuwa akiamini kuwa matatizo ya mipaka hayatakuwapo baina ya nchi za kiafrika zikishapata uhuru kutokana na uaminifu wake kwenye Pan-Africanism. Ingawa mwanzonui kulikuwa na uhakika kuwa swala hilo litatatuliwa baina ya Tanganyika na Malawi, lilharibika baadaye kutokana na Banda kutofautiana na Nyerere kwenye siasa za Afrika ya kusini, Ureno na Rhodesia.

Ukweli ni kuwa mpaka halali ni ule unaopita katikakati ya ziwa kwa sababu mpaka unaotumiwa sasa hivi ulichorwa kimakosa na serikali ya uingereza na hivyo hatulazimiki kuufuata chini ya makubalinao ya OAU. Kwa vile sisi ni mataifa yaliyokomaa baada ya kuwa huru kwa zaidi ya miaka hamsini, itakuwa ni aibu iwapo tutashindwa kumalizana locally mpaka tuhusishe mataifa ya nje. Kuna sababu za kimsingi sana kwa nini hakuna mpaka wowote hapa duniani unaofuata ufukwe wa ziwa au ufukwe wa bahari isipokuwa huu wa Malawi. Njia nyingine zinazoweza kutumika nia kama vile kwa Malawi kutambua kuwa madai ya Tanzania yana mantiki yake na kudai settlement fulani kutoka Tanzania ili kumaliza tatizo hilo. Tusipolimaliza sasa hivi, ni wazi kuwa jambo hili litatuletea matatizo makubwa sana huko mbeleni ikionekana kuwa lina raslimali nyingi zaidi ya samaki na maji.

Ni kwa mambo kama haya kuhusu makubaliano ya zamani yasiokuwa na masalahi kwa nchi ndipo ninajiona namkosa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere, au angalau chama cha CHADEMA kilichoonyeshe kujali Watanzania na raslimali za watanzania kwa ujumla, na hata mtu wa aina ya Lowassa

Angalau jamaa huyo Lowasa anajua sana kutetea raslimali za tanzania hasa zile ambazo hazimletei yeye binafsi pesa ya moja kwa moja, tuliona mgogoro wa Mto Nile na Misri.
 
Yericko ,hamasisha vita lakini mimi nitakuwa upande wa Malawi siyo dhambi kuwa mamluki ukizingatia kuwa mashine najua kutumia na utandawazi huu wa mitandao ya cm na internet miye ni kuclikc tu kule Blantare kitu kinamwagika pwaa.Kikosi au platoon inateketea.Nitakuwa mtu wa mwisho kushawishiwa kwa VITA HII YA KIJINGA.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom