Unga mkono JWTZ kulinda mipaka ya Nchi yetu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unga mkono JWTZ kulinda mipaka ya Nchi yetu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, Aug 7, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,240
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Uzalendo kwa nchi yetu ni muhimu kuliko kila kitu, nawaomba ndugu zangu tusiingize siasa juu ya mgogoro wa Malawi na mengine yanayohusu taifa!

  Tangu juzi majira ya saa sita za usiku vikosi vya wapiganaji vya Tanzania vikiwa na silaha nzito vimeanza kuwasili kusini mwa Tanzania kukabiliana na UVAMIZI wa Malawi,

  Ninawashauri wanaolidharau jeshi letu wasafiri mpaka kwenye ufukwe wa Ziwa Nyasa (beach) wakaone wapiganaji wetu walivyo pandisha MORI kwa hamu ya kusubiri amri ya Amiri jeshi Mkuu wa Majeshi yote Tanzania na kuanza mtiti rasmi wa kumuonya Banda!


  Haijalisha juhudi za kidiplomasia zinaendelea lakini kinga na heshima ya taifa letu haitapuuzwa hata chembe,

  Pamoja na tamko la serikali ya Tz kumtaka rais Joyce Banda kusitasha shughuli za utafiti wa mafuta katika ziwa Nyasa mpaka suluhu ya kidiplomasia ipatikane, bado taarifa za kiintelijensia kutoka Ikulu ya Malawi zinasema kuwa Mwanamama Joyce ameshikilia uzi kuwa Ziwa LOTE ni lake!

  Katika hali hii, niwazi kuwa ili kuilinda mipaka ya nchi yetu yatupasa KUUNGA MKONO JWTZ kwa kila hali na mali, na ikilazimu kupatikana wapiganaji wa kujitolea mimi nitakuwa wakwanza kuingia uwanja wa VITA kuitetea nchi yangu dhidi ya UVAMIZI dharimu wa Malawi kwa ardhi yetu!

  Tuache siasa tuungane kuwaunga mkono wanadiplomasia wanaojitahidi kuepusha VITA na ikishindikana TUUNGE MKONO vita kwa moyo mmoja kutetea UHURU wetu!

  Itasikitisha kusikia siasa za Chadema, CUF, UDP, TLP,NCCR Mageuzi au CCM katika mgogoro huu.

  Wote tuongee lugha moja tuhubiri uhuru wa nchi yetu, na hakuna kipande cha ardhi yetu kitakachomegwa na taifa lolote lile kigeni tungali hai watz!

  UNGA MKONO JWTZ kulinda NCHI yetu!
   
 2. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Saafi, hawa wamalawi wanataka kupima nguvu zetu za kijesh ngoja tukawavamie! Mpaka blantaya wasagaji na mashoga hao alaa
   
 3. B

  Babuu Rogger JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 80
  Wanajeshi si ndio kazi yao, waache waende kwani muda wote wameuchuna tuuuuuuuu.
   
 4. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,240
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Ili washinde wanahitaji kuungwa mkono na wananchi, kumbuka vita ya uganda tulishinda kwakuwa tuliungana na kuwa kitu kimoja!

  UNGA MKONO JWTZ kulinda nchi yetu
   
 5. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  kuunga mkondo jeshi sio kusema tu bali hata kuingia hapa Jukwaani na mwelekeo ulio mzuri ni supporter pia.
  Mimi ni Mtanzania lakini naomba Mh. Waziri Mathias Chikawe afute kwanza kauli yake bungeni kuwa wahusika wa EPA Tanzania hawahusiki lakini asipofanya hiyo, I feel so inferior to support our Jeshi japo inauma!

  Pia mkuu Yeriko usijidanganye na 'ukubwa' wa jeshi maana la Ghadafi lilikuwa kubwa zaidi ya letu!

   
 6. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Navichukia sana vyombo vya ulinzi vya Tanzania. Rasilimali za nchi zikichukuliwa na nchi jirani wanapandisha mori lakini zikichukuliwa na Mtanzania fisadi zikaenda kufichwa nchi jirani hawana Tatizo nao.
   
 7. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,240
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Siku zote katika maisha yangu huamini kuwa vita kati ya Haki na Udharimu, Mungu huwa upande wa HAKI na katika hili Tanzania tupo upande wa HAKI
   
 8. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  we jidanganye tu, vita ikianza mps wanapita kukamata maofisini kama nyie kuwapeleka mstari wa mbele...
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Shime watanzania katika hili JWTZ wanaitaji moral and material support izi tofauti zetu za ndani zikae kando kwanza
   
 10. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,240
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Hehee hajajua msamehe, tumuelishi hapahapa ajiweke sawa kwa vita!
   
 11. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #11
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,240
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Hakika mkuu, nimegonga like japo hujaiona!
   
 12. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Haya sasa vita ni vita mura kilimo kwanza mfuko wa mbolea laki moja muraaaaa kusema mbali vitendo mbali tafakari chukua hatua!
   
 13. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Wakianzisha vita wanataka tuwaunge mkono wakati wa amani wanatuibia na kuficha VIJISENTI ulaya wakati sie tunakufa na njaa!!
   
 14. malema 1989

  malema 1989 JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 848
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  hayo maneno tu, mbona huku tumeshaanza kujiandikisha? sipatii picha huyu mama banda tutamfanya nn tutakapoiteka Malawi .Hivi huyu ni mke wa docta kamuzu /litoto lake? maana majina ya mwisho kama yanafanania vile!
   
 15. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,335
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  there won't be no war...
   
 16. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Siwezi kuunga mkono ili swala, hivi unajua ndani ya tanzania kuna ardhi ambayo siyo mali yetu? Ambayo viongozi wetu wameuza kwa mataifa ya kiarabu toka enzi za Mwinyi?

  Ziwa Nyasa ni mali ya Wamalawi,kwa nini unataka tumwage damu kwaajili ya kuwanyanganya wa Malawi ardhi yao? Ingali tunashindwa kusimamia ardhi yetu inayochukuliwa na wageni kila uchao?
   
 17. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  yanaibuka mapya sasa, na mtu asimame hapa na kubisha juu ya haya!!! Yametokea jeshi likiwepo!
   
 18. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #18
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Umegonga ikulu safi sana kiongozi,nilishawahi sema huko nyuma bora tu wamalawi wachukue ziwa lao!!
   
 19. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #19
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,240
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu!
  Hata kama hayo yapo kwa mgongo wa uwekezaji lakini uvamizi wa Malawi tuugatae!

  Tusimamie ukweli wa mpaka kuwa katikati ya ziwa nyasa na si ufukwe wa tz!
   
 20. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #20
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Yericko NI UJINGA SANA KUTAMBA KWA KUCHOKONOA VITA.kWENYE MABANGO YAKO MENGI NIMEKUWA NIKIKUUNGA MKONO LAKINI KWA ILI SIKUUNGI HATA KUCHA.Mimi ni askari by professional ingawa niliacha na kujiunga na kazi za kiraia za serikali, mantiki ya kuunga mkono vita haipo.Utakuwa uwendawazimu leo hii TANZANIA ITAINGIA VITANI NA MALAWI KWA AJILI YA MPAKA.vITA WATU KAMA WEWE WANAFIKIRI NI SHEREHE ZA HARUSI NA KUVISHANA PETE.NO.Kwa nchi kama hii ambayo imekwisha tafunwa na ufisadi wa kutisha ni MAFISADI TU NDIO WANASHANGILIA VITA ILI WAPATE MWANYA WA KUIFISADI NCHI VIZURI.CHAMA CHANGU MAKINI CDM NAOMBA KIWEKEZE KATIKA DIPLOMACY NA KUACHA KAULI ZA KIJINGA ZA AKINA MEMBE KUCHOKONOA VITA. NCHI HII HAINA UWEZO WA KIFEDHA KUWEKA JESHI KATIKA VITA ZAIDI YA WEEK 4 BILA KUFILISIKA RASMI.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...