Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,387
- 10,965
Kwa hiyo alijaribu hata kushauri? Maana hiyo ndiyo hoja ya msingi; kama ana dhamira ya dhati ya ubanaji wa matumizi kwa mambo yasiyo ya msingi. Kwa upande mwingine, je, Rais alikuwa na mamlaka ya kuamua fedha kutoka kwa wafanyabiashara zitumike vipi?Kushawishi na kuwa na Mamlaka ya kuamua ni vitu viwili tofauti.
Sawa. Kulikuwa na ulazima wa Rais kwenda physical pale? Mbona tuna teknolojia ambayo ingemwezesha kushiriki sherehe hizo hata akiwa Ikulu Dar? Angetumia video conferencing kutoa hotuba yake fupi, katika kuepusha gharama ambazo zimetumika kwa yeye na msafara wake kusafiri kwa barabara kutoka Dar hadi Singida.Kumbuka chama kinaundwa na wanachama na hizo sherehe ni njia mojawapo ya kukutanisha wanachama wote ambao hawapati fursa ya kuhudhuria kwenye vikao vya juu chamani. Hapo ni kuonesha uwazi na uwajibikaji mbele ya wanachama wake.
Kwa upande mwingine, sijaelewa hoja yako ya kuhusisha sherehe na uwajibikaji wa viongozi wa chama mbele ya wanachama. Ebu fafanua zaidi: yaani sherehe za birthday ya CCM ni njia mojawapo ya kuonyesha uwajibikaji wa viongozi kwa wanachama? Uwajibikaji katika nini? Kwani sherehe hiyo ni kwa ajili ya kusoma taarifa za mapato na matumizi ya chama? Chama hakina njia zingine za kuwajibika kwa wanachama? Pia hata Mwenyekiti angeweza kuwa Msoga na kisha vyombo vya habari vikawapa pale na yeye akizungumza kile alichozungumza Singida, bado angekuwa amewajibika kwa namna moja au nyingine, kama kuzungumza na hadhira ni njia ya uwajibikaji kama unavyosema.