Unazuia sherehe za Uhuru, unaadhimisha birthday ya CCM

magode

JF-Expert Member
Oct 2, 2014
2,204
3,337
Wanabodi
Salaam;

Serikali ya awamu ya 5 inajinasibu kubana matumizi na kufuta baadhi ya sherehe za kitaifa kwa lengo hilo la kuzuia matumizi yasiyo ya lazima.

Kichekesho kimeonekana leo baada ya serikali nzima kuhamia Singinda kwenye sherehe za birthday ya CCM ya kutimiza miaka 39.

Huko nyuma tulishuhudia sherehe za uhuru zikipigwa kumbo, sherehe za wabunge zikapigwa ban, baadae TBC nayo ikapigwa ban kwa lengo hilo hilo la kubana matumizi. Cha kushangaza Rais na serikali nzima walikuwa kwenye birthday hiyo ya CCM kwa ajili ya kutoa hotuba za mipasho!!

Kweli hii nchi ngumu sana aisee!
 
You mean unasema kuwa chadema, ACT, Nccr, Tadea, Chaumma wakitaka kufanya sherehe zao magufuli aingilie??

Sherehe za CCM sio za kitaifa, sherehe ya uhuru ni ya kitaifa

sherehe ya ccm ni ya kichama, ya uhuru ni ya serikali

acha upuuzi
 
muanzisha uzi, mtendee haki mama yako na baba yako! hawakukuzaa zuzu ila chuki zako ndio zinakupofusha

you mean unasema kuwa chadema, ACT, nccr, tadea, chaumma wakitaka kufanya sherehe zao magufuli aingilie??

sherehe za ccm sio za kitaifa, sherehe ya uhuru ni ya kitaifa

sherehe ya ccm ni ya kichama, ya uhuru ni ya serikali

acha upuuzi
Ungeweza tu kuchangia bila kutukana bado ningekuelewa..! Nisaidie ndugu kunielewesha,Rais,waziri mkuu,makamu wa Rais nk. Magari waliyotumia ni ya ccm?? Unaweza kutuhakikishia vp km matangazo ya moja kwa moja ccm ndo wamelipia?? Ukiweza rudi kwa matusi tena kwa sababu hainipunguzii kilo.
 
Sa kwani hizo si ni pesa za chama chao ama?

Wanabodi
Salaam;

Serikali ya awamu ya 5 inajinasibu kubana matumizi na kufuta baadhi ya sherehe za kitaifa kwa lengo hilo la kuzuia matumizi yasiyo ya lazima.

Kichekesho kimeonekana leo baada ya serikali nzima kuhamia singinda kwenye sherehe za birthday ya ccm ya kutimiza miaka 30.

Huko nyuma tulishuhudia sherehe za uhuru zikipigwa kumbo,sherehe za wabunge zikapigwa ban,baadae tbc nayo ikapigwa ban kwa lengo hilo hilo la kubana matumizi. Cha kushangaza Rais na serikali nzima walikuwa kwenye birthday hiyo ya ccm kwa ajili ya kutoa hotuba za mipasho!!

Kweli hii nchi ngumu sana aisee!
Tatizo kuu la Nchi yetu kwa sasa ni upeo mdogo wa Watu wetu kama huyu mleta mada! Mtu mzima hataki kushughulisha akili (kama anayo)! CHADEMA na hii "Mizwazwa" ni mzigo kwa Taifa! Mtu hajui hata tofauti kati ya shughuli za Chama na Serikali! Mwisho itasema Rais Magufuli kazuia harusi za watu binafsi ili kubana matumizi ya Serikali! Haya ndo huandaa maandamano kwenda Ikulu kwa Rais ili kuona TV live! Michovu kila mahali!
 
Siku hizi ujinga umegeuzwa kuwa hekima na busara!

Kuna baadhi ya watu hawafahamu kama ni wajinga!

He who knows not and knows not that he knows not is a fool!

Hufahamu hata maana/tofauti ya sherehe za chama na taifa.

Kasome kwanza civics!

Mambo kama haya hata mtu mwenye common sense ambaye halifahamu hata darasa atafahamu tofauti ya sherehe za chama na kitaifa,
 
siku hizi ujinga umegeuzwa kuwa hekima na busara!

Kuna baadhi ya watu hawafahamu kama ni wajinga!

He who knows not and knows not that he knows not is a fool!

Hufahamu hata maana/tofauti ya sherehe za chama na taifa.

Kasome kwanza civics!
mkuu matumizi ya viongozi wote wa serikali waliohudhuria yamegharikiwa na ccm au ni kodi zetu?? Tupe pia uhakika wa ccm kulipia matangazo ya moja kwa moja kupitia tbc!
 
Ungeweza tu kuchangia bila kutukana bado ningekuelewa..! Nisaidie ndugu kunielewesha,Rais,waziri mkuu,makamu wa Rais nk. Magari waliyotumia ni ya ccm?? Unaweza kutuhakikishia vp km matangazo ya moja kwa moja ccm ndo wamelipia?? Ukiweza rudi kwa matusi tena kwa sababu hainipunguzii kilo.
Magari Ni ya serkali kwa sababu wao Ni viongozi wakubwa wa serilali, rais akienda kwenye birthday ya mpwa wa shemeji yake bado atatumia gari ya serilali. Ile ilikuwa sherehe ya CCM, mwenye mamlaka hayo Ni mwenyekiti wa CCM, rais alikaribishwa tu.
 
kumbuka sherehe za vyama zinagharamikiwa na vyama vyenyewe na aio serikali inayotoa hela. hamna sababu yakuzizuia hoja hii hujafikiri kabla yakuileta tofautisha fedha za serikali na fedha za vyama tofauti kabisa imebwaya hiii thread
 
Kweli nchi hii ngumu tena xana xaxa sijui matumizi yapi wanayobana wanajitekenya wenyewe na wanacheka wenyewe
 
.....ni ileile eeeh ooh ni ileile eeh
Mshana jr mtendee haki mtoa mada, usiendelee kumjaza ujinga. Ninafahamu wewe una uelewa zaidi kuhusu tofauti ya sherehe za vyama na serikali.
mkuu matumizi ya viongozi wote wa serikali waliohudhuria yamegharikiwa na ccm au ni kodi zetu?? Tupe pia uhakika wa ccm kulipia matangazo ya moja kwa moja kupitia tbc!
Waziri Mkuu alipoenda Arusha kwenye sherehe ya kusimikwa Askofu Mkuu KKKT Frederick Shoo unadhani kanisa la KKKT lilimlipia pesa za mafuta ya magari na walinzi wake?

Nimekuambia nenda shule ukajifunze civics!
 
Mshana jr mtendee haki mtoa, usiendelee kumtia ujinga. Ninafahamu wewe una uelewa zaidi kuhusu tofauti ya sherehe za vyama na serikali.

Waziri Mkuu alipoenda Arusha kwenye sherehe ya kusimikwa Askofu Mkuu KKKT Frederick Shoo unadhani kanisa la KKKT lilimlipia pesa za mafuta ya magari na walinzi wake?

Nimekuambia nenda shule ukajifunze civics!
Ungejipa muda wa kusoma nilichoandika wala usingetetea hii kitu. Me nimezungumzia serikali yote ilikuwa pale,me najua hujasoma lkn hata hili unashindwa kujua kuwa serikali imetumia kodi zetu?? Unalinganisha waziri mkuu aliyeenda peke yake na hawa walionda wote kwa gharama zetu..???
 
Kwa hiyo mleta mada unashauri Sherehe za Uhuru Zingefanyika kwa sababu chama kimefanya Sherehe. Na hata kama zote zingekuwa halali kufanya moja na nyingine ukawasaidia wananchi tatizo ni nini????? Vyovyote iwavyo kuna unafuu kuliko tulipotoka.
 
Back
Top Bottom