Unazuia sherehe za Uhuru, unaadhimisha birthday ya CCM

Unazuia sherehe za Uhuru, unaadhimisha birthday ya CCM

Wanabodi
Salaam;

Serikali ya awamu ya 5 inajinasibu kubana matumizi na kufuta baadhi ya sherehe za kitaifa kwa lengo hilo la kuzuia matumizi yasiyo ya lazima.

Kichekesho kimeonekana leo baada ya serikali nzima kuhamia singinda kwenye sherehe za birthday ya ccm ya kutimiza miaka 30.

Huko nyuma tulishuhudia sherehe za uhuru zikipigwa kumbo,sherehe za wabunge zikapigwa ban,baadae tbc nayo ikapigwa ban kwa lengo hilo hilo la kubana matumizi. Cha kushangaza Rais na serikali nzima walikuwa kwenye birthday hiyo ya ccm kwa ajili ya kutoa hotuba za mipasho!!

Kweli hii nchi ngumu sana aisee!
Mkuu unaposema CCM imetimiza miaka 30 leo ni kwa hesabu za shule gani?
 
Ungejipa muda wa kusoma nilichoandika wala usingetetea hii kitu. Me nimezungumzia serikali yote ilikuwa pale,me najua hujasoma lkn hata hili unashindwa kujua kuwa serikali imetumia kodi zetu?? Unalinganisha waziri mkuu aliyeenda peke yake na hawa walionda wote kwa gharama zetu..???
Kwa msaada mdogo tu ni kwamba; hao viongozi unaowaona waliohudhuria hizo sherehe walienda wakiwa na kofia za uanachama wa CCM na si kwa kofia ya uongozi wa Serikali kama unavyodai. Hebu jiulize mbona hakuna kiongozi yeyote kutoka nchi jirani alikuwepo pale. Kama akialikwa mgeni kutoka nchi jirani basi atakuja Mwenyekiti wa chama au katibu wa chama cha siasa na si kama Rais wa nchi fulani. Umetaka ushahidi kama pesa iliyotumika ni ya chama au ya serikali; sasa rafiki yangu mbona unahoji juu ya matumizi ya chama hicho kabla ya kuuliza mapato yake? Mimi labda nikuulize wewe CCM wanaingiza kiasi gani hadi wewe kuhofia hawawezi kumudu gharama za sherehe yao?
 
Tatizo hizo sherehe zinagaramiwa na pesa za wananchi wote kama ilivyo za siku ya uhuru
Serikali inatoa ruzuku kila mwezikwa kila chama chenye wabunge. Kiasi cha ruzuku hutegemea idadi ya wabunge kama sikosei. Once chama kimepata ruzuku, hiyo pesa si ya wananchi wote bali ni ya wanachama wa chama husika. Wakiamua kujirusha kama ilivyofanya ccm leo hakuna wakuingilia. Halafu hakuna hata senti ya serikali iliyotumika kwani ccm ni chama tajiri sana na ina raslimali zinazoingiza fedha nchi nzima. Kwa hiyo kugharamia kijisherehe kama cha leo si tatizo. Chezea ccm wewe
 
Wanabodi
Salaam;

Serikali ya awamu ya 5 inajinasibu kubana matumizi na kufuta baadhi ya sherehe za kitaifa kwa lengo hilo la kuzuia matumizi yasiyo ya lazima.

Kichekesho kimeonekana leo baada ya serikali nzima kuhamia singinda kwenye sherehe za birthday ya ccm ya kutimiza miaka 30.

Huko nyuma tulishuhudia sherehe za uhuru zikipigwa kumbo,sherehe za wabunge zikapigwa ban,baadae tbc nayo ikapigwa ban kwa lengo hilo hilo la kubana matumizi. Cha kushangaza Rais na serikali nzima walikuwa kwenye birthday hiyo ya ccm kwa ajili ya kutoa hotuba za mipasho!!

Kweli hii nchi ngumu sana aisee!

Tatizo ni nini hasa? Umeshindwa kabisa kutofautisha kati ya shughuli za vikundi vya 'hiari' mfano vyama vya siasa na nchi?
 
kama ametumia gharama za serikali sio vizuri na inastahili kukemewa ila kama ni za chama sawa tu,tutofautishe mambo ya chama na ya serikali hata mimi naweza acha party yoyote ofisini kwangu nikaenda kusheherekea birthday ya mwanangu
Hii haikwepeki.kaenda na magari ya serikali, walinzi wa serikali kwenye sherehe za chama
 
Utaratibu wa kutumia mali za umma kwa shughuli za vyama ni wa ajabu sana. Ndiyo maana sishangai mawaziri na viongozi waandamizi wa serikali kutumia mali za umma kwa shughuli zao binafsi. Hili limehalalishwa na serikali za CCM. Na kufanywa kama jambo lililo sawa kabisa. Ndiyo maana umeweza kuona sawa kwa viongozi lukuki kutumia mali na fedha za umma kuhudhuria sherehe za chama.

Kama sababu ya Rais kutofanya sherehe wakati wa Uhuru ilikuwa na kuepusha matumizi mabovu, basi angeshukuru kwa mualiko na kusema haoni haja ya kwenda, kwani safari ya Rais tena kwa barabara inagharimu fedha nyingi za umma. Alternatively, angeweza kubaki Dar, na kuhutubia hadhara ya kwenye sherehe kwa njia ya video. Angetumia utaratibu wa video conferencing, angeokoa fedha nyingi za umma. Yeye ni Rais, ingawa ni mwana CCM pia, lakini mualiko haumfungi yeye kuhudhuria kwa ulazima, kama kweli ana dhamira ya dhati juu ya uepushaji wa matumizi yasiyo ya lazima.
Huku mnakoelekea mtasema pia Rais aondolewe ulinzi maana ni gharama. Hivi Rais alifuta sherehe za uhuru au alibadilisha namna ya kusherehekea?? Kweli kulalamika ni jadi yetu waTz
 
Siku hizi ujinga umegeuzwa kuwa hekima na busara!

Kuna baadhi ya watu hawafahamu kama ni wajinga!

He who knows not and knows not that he knows not is a fool!

Hufahamu hata maana/tofauti ya sherehe za chama na taifa.

Kasome kwanza civics!

Mambo kama haya hata mtu mwenye common sense ambaye halifahamu hata darasa atafahamu tofauti ya sherehe za chama na kitaifa,
Acha kujifanya mjuaji.rais na wenzake wametumia fedha za umma kwenye sherehe za ccm.full stop
 
Huwezi kubana matumizi kwenye serikali wakati chama chako kinafuja hela. Charity begins at home. Kwani wale maofisa waliokuwa wanazuiliwa airport wasisafiri kwenda holiday waliiuwa wanatumia hela ya serikali? Kuna hela hapo za walipa kodi zimetumika, kama vile matumizi ya magari na madereva ambao wamo kwenye ayroll ya walipa kodi. Ila tu naamini kwamba hizi sherehe zimefanyika kwa vile Dr Magufuli hakuwa na nguvu katika uamuzi wa hili katika chama. Hii ni kuonesha kuwa CCM hawako pamoja na Dr Magufuli katika hili suala la kukata matumizi. Wingi wao wamekosa kupiga hela!
 
You mean unasema kuwa chadema, ACT, Nccr, Tadea, Chaumma wakitaka kufanya sherehe zao magufuli aingilie??

Sherehe za CCM sio za kitaifa, sherehe ya uhuru ni ya kitaifa

sherehe ya ccm ni ya kichama, ya uhuru ni ya serikali

acha upuuzi
Mm nadhani ilitakiwa awe kazini huyo rais wenu na serikali yake. Maana wanawazuia watu wasifanye mikutano na kisiasa kwa kusema muda wa kampeni umeisha. Kwanini wao wasiwe mfano kwa kufanya kazi kwanza alafu maadhimisho baadae
 
Kulikuwa na magari ya serekali pale na mdafara wa Rais,maskari wa kutosha ccm ndo imeweka mafuta ya magari ?
Rais analindwa hata akienda kumsalimia binamu yake kijijini achilia mbali mama yake! mimi nadhani kama kungekuwa na kasoro juu ya sherehe hizo basi viongozi wa vyama vya upinzani ilikuwa ni sehemu muafaka ya kukosoa. Ukiona kimya basi jua mambo yapo sawa.
 
Sisiemu ina hela zake na vyanzo vyake vya pesa na wanazitumia wanavyotaka wao, wakiamua wanarusha bonge la party au wakiamua wananunua madawati.
Magufuli sio wa kuamrisha sisiemu watumie vipi pesa zao.
 
mkuu matumizi ya viongozi wote wa serikali waliohudhuria yamegharikiwa na ccm au ni kodi zetu?? Tupe pia uhakika wa ccm kulipia matangazo ya moja kwa moja kupitia tbc!
Sasa kama hujui aliyegharamia hiyo shughuli unaanzishaje uzi kulalamikia serikali!?

Ndo maana watu wanadoubt uwezo wako wa kufikiri. CCM ni taasisi kama zilivyo CHADEMA, nccr nk! Iliweza kuendesha kampeni leo ishindwe kulipia matangazo ya Luninga!? Ishindwe kugharamia safari za viongozi wake!? You must be kidding man!
 
Back
Top Bottom