Unazuia sherehe za Uhuru, unaadhimisha birthday ya CCM

Unazuia sherehe za Uhuru, unaadhimisha birthday ya CCM

Ungeweza tu kuchangia bila kutukana bado ningekuelewa..! Nisaidie ndugu kunielewesha,Rais,waziri mkuu,makamu wa Rais nk. Magari waliyotumia ni ya ccm?? Unaweza kutuhakikishia vp km matangazo ya moja kwa moja ccm ndo wamelipia?? Ukiweza rudi kwa matusi tena kwa sababu hainipunguzii kilo.
Mkuu kwa hiyo ulitaka Rais , Waziri Mkuu, Makamu wa Rais wasiende kwenye sherehe za chama chao?
 
Kama unadhani gharama zilizotumiwa si za chama ni za serikali, wewe mwenye dhania hiyo ndiye unapaswa kuweka ushahidi huo hapa, usiwe na dhania za kimahaba!!!
Tangu jana kikwete aliposema vijana wa mtandaoni serikali iwafikirie,naona mko busy kutetea kila upuuzi! Me naweza kuwa sina ushahidi wa takwimu lkn ushahidi wa mazingira upo wazi. Rais alienda na msafara na magari ya umma,waziri mkuu,mawaziri,wakuu wa mikoa na wilaya. Hawa wote walitumia kodi zetu. Ambacho niliona kwa macho ni cha ccm,ni mashati tu ya kijani. Acheni kujitoa ufahamu!
 
Ungeweza tu kuchangia bila kutukana bado ningekuelewa..! Nisaidie ndugu kunielewesha,Rais,waziri mkuu,makamu wa Rais nk. Magari waliyotumia ni ya ccm?? Unaweza kutuhakikishia vp km matangazo ya moja kwa moja ccm ndo wamelipia?? Ukiweza rudi kwa matusi tena kwa sababu hainipunguzii kilo.
.......tafakari, bila upendeleo wa kujiliwaza,wala kujichukiza:.......ktk nchi zetu hizi kwenye ukanda wa SADC, nani anaweza kuzuia vyama tawala(CCM,FRELIMO,SWAPO,ZANU-PF,MPLA,ANC),kutumia serikali zake kujiimarisha?....viongozi ktk mageuzi,(sad to say)wako mbali mno kupata mbinu stahiki kivitendo, kukitoa madarakani CCM...zaidi ni uhodari wa kutoa kauli kali,zilizojaa hamasa hewa, na mapungufu ya kiuhalisia..
 
mkuu matumizi ya viongozi wote wa serikali waliohudhuria yamegharikiwa na ccm au ni kodi zetu?? Tupe pia uhakika wa ccm kulipia matangazo ya moja kwa moja kupitia tbc!
Mimi binafsi sina wasiwasi na akili yako sababu hauna.
Hivi mbowe alipoenda Nairobi kwa shughuli binafsi kwa kutumia gari la KUB ilikuwa sahihi?,kama ilikuwa sahihi kwa Mbowe sasa iweje leo iwe wrong kwa viongozi wa CCM kutumia magari ya serikali kutokana na nyadhifa zao?
Think big Nyumbu
 
Kwani kwenye sherehe za chama, serikali si inakuwa imealikwa. Mpaka sasa Magufuli hana uongozi wowote wa juu ndani ya chama chake, ukiachia kuwa mjumbe wa kamati kuu kwa nafasi yake aliyonayo ya rais. Sidhani kama angeweza kuzuia chochote wakati yeye ni mwalikwa.
 
You mean unasema kuwa chadema, ACT, Nccr, Tadea, Chaumma wakitaka kufanya sherehe zao magufuli aingilie??

Sherehe za CCM sio za kitaifa, sherehe ya uhuru ni ya kitaifa

sherehe ya ccm ni ya kichama, ya uhuru ni ya serikali

acha upuuzi
mkuu mimi nilidhani hata sherehe za ccm hutumia kodi zile zile za wanachi...
nilidhani ukitumia fedha za chama unatumia fedha za wanachama..
na ukitumia fedha za nchi,unatumia fedha za wananchi..
wanachama na wananchi ni walewale..
na hizo fedha ziwe kwenye chama,ziwe serikalini ni za watanzania walewale..
na nilidhani fedha hizohizo zilizoko kwenye chama na zilizoko serikalini ndizo za kuwaletea maendeleo wananchi...
au fedha zikiwa chamani si za maendeleo ni za starehe na kufuja ?
lakini pia najiuliza..iweje serikali ya CCM ikiwa na fedha serikalini iseme hizi tunabana,ikiwa na fedha chamani iseme hapa hakuna kubana ni full kujiachia..
which is which ?
 
Mkuu kwa hiyo ulitaka Rais , Waziri Mkuu, Makamu wa Rais wasiende kwenye sherehe za chama chao?
Angalau ww mkuu Ritz umeuliza swali zuri. Kwenda au kutokwenda sioni km ni hoja. Hoja hapa ni kwamba,Rais yupo kwenye mkakati wa kubana matumizi,na ndani ya ccm ni mtu ambae ana ushawishi mkubwa,kwa vile sherehe zilikuwa zinahusu chama kinachotawala ni wazi kingetumia(kimetumia)gharama kubwa sana! Kwa nini asingetumia nguvu yake ya ushawishi kuzuia hizo sherehe ambazo mbali na gharama za ccm,hata serikali imetumia gharama kubwa sana kumhudumia Rais na viongozi wengine. Mbona aliweza kuzuia fedha za wabunge ambako pia alialikwa?? Tuache ushabiki ktk mambo ya kitaifa!
 
Sawa. Lakini yeye ni mwanachama mwenye ushawishi mkubwa kuliko wote, kwa sababu ni mwanachama aliye Rais wa JMT. Je, alitumia ushawishi huo kushauri na kumtaka Mwenyekiti wa CCM atumie fedha za sherehe kwenye shughuli za maendeleo? Kama alivyotumia ushawishi wake kumshauri na kumwagiza Spika wa Bunge juu ya fedha za 'sherehe ya wabunge'.

Pesa za ccm ziende kwenye Maendeleo? Kwa maana hiyo hata pesa za Chadema ziende kwenye Maendeleo.

Je upo tayari Ruzuku ifutwe kwenye vyama vya siasa?
 
You mean unasema kuwa chadema, ACT, Nccr, Tadea, Chaumma wakitaka kufanya sherehe zao magufuli aingilie??

Sherehe za CCM sio za kitaifa, sherehe ya uhuru ni ya kitaifa

sherehe ya ccm ni ya kichama, ya uhuru ni ya serikali

acha upuuzi
Kinachozungumziwa hapo ni utumiaji wa rasilimali za taifa,elewa jambo ndio uchangie huyo rais alivyokwenda singida katumia rasilimali za taifa kuanzia walinzi,magari,mafuta, utakuta hata posho zimetumika sasa wewe badala ya kuyatazama hayo unarusha ngumi hewani.huko ndio kubana matumizi?mapolisi walijazana uwanjani kwa ajili ya hiyo shughuli ya ccm ndio kubana matumizi?masikini mpaka wengine wamepoteza maisha yao.ujinga wenyewe ndio kama huu
1454821919604.jpg
 
Wanabodi
Salaam;

Serikali ya awamu ya 5 inajinasibu kubana matumizi na kufuta baadhi ya sherehe za kitaifa kwa lengo hilo la kuzuia matumizi yasiyo ya lazima.

Kichekesho kimeonekana leo baada ya serikali nzima kuhamia singinda kwenye sherehe za birthday ya ccm ya kutimiza miaka 39.

Huko nyuma tulishuhudia sherehe za uhuru zikipigwa kumbo,sherehe za wabunge zikapigwa ban,baadae tbc nayo ikapigwa ban kwa lengo hilo hilo la kubana matumizi. Cha kushangaza Rais na serikali nzima walikuwa kwenye birthday hiyo ya ccm kwa ajili ya kutoa hotuba za mipasho!!

Kweli hii nchi ngumu sana aisee!


Naona unajaribu kulinganisha vitu viwili tofauti kabisa!!
CCM ni taasisi yenye vyanzo vyake ambavyo havitoki serikalini anayoiingoza Magufuli.
 
Sa kwani hizo si ni pesa za chama chao ama?
Kwahiyo hao mapolisi waliofariki ktk uwajibikaji wa kwenye sherehe hizo unawaweka kundi gani?wangekufa green guard sawa lkn hawa ni watumishi wa umma,tumia busara
 
Hapo hazitumiki pesa za serikali... ni pesa za chama... Alafu ukumbuke hapo ni mwenyekiti ndiyo mwenye maamuzi...
 
Ungeweza tu kuchangia bila kutukana bado ningekuelewa..! Nisaidie ndugu kunielewesha,Rais,waziri mkuu,makamu wa Rais nk. Magari waliyotumia ni ya ccm?? Unaweza kutuhakikishia vp km matangazo ya moja kwa moja ccm ndo wamelipia?? Ukiweza rudi kwa matusi tena kwa sababu hainipunguzii kilo.
Pia muulize wale police waliopoteza maisha ni green guard?wale ni watumishi wa umma wamekufa wakikitumikia ccm hao,kwanini tusilaani hicho kitendo
 
Wanabodi
Salaam;

Serikali ya awamu ya 5 inajinasibu kubana matumizi na kufuta baadhi ya sherehe za kitaifa kwa lengo hilo la kuzuia matumizi yasiyo ya lazima.

Kichekesho kimeonekana leo baada ya serikali nzima kuhamia singinda kwenye sherehe za birthday ya ccm ya kutimiza miaka 39.

Huko nyuma tulishuhudia sherehe za uhuru zikipigwa kumbo,sherehe za wabunge zikapigwa ban,baadae tbc nayo ikapigwa ban kwa lengo hilo hilo la kubana matumizi. Cha kushangaza Rais na serikali nzima walikuwa kwenye birthday hiyo ya ccm kwa ajili ya kutoa hotuba za mipasho!!

Kweli hii nchi ngumu sana aisee!
Kwan sherehe za ccm zinatumia pesa za wananchi?
 
Tatizo kuu la Nchi yetu kwa sasa ni upeo mdogo wa Watu wetu kama huyu mleta mada! Mtu mzima hataki kushughulisha akili (kama anayo)! CHADEMA na hii "Mizwazwa" ni mzigo kwa Taifa! Mtu hajui hata tofauti kati ya shughuli za Chama na Serikali! Mwisho itasema Rais Magufuli kazuia harusi za watu binafsi ili kubana matumizi ya Serikali! Haya ndo huandaa maandamano kwenda Ikulu kwa Rais ili kuona TV live! Michovu kila mahali!
Kafie mbele ya safari wewe panya buku,yaani mtu kutoa mawazo yake ndio unamjibu maneno makali utadhani kakuchukulia mkeo?ukoo wa panya wewe
1454822415958.jpg
 
Siku hizi ujinga umegeuzwa kuwa hekima na busara!

Kuna baadhi ya watu hawafahamu kama ni wajinga!

He who knows not and knows not that he knows not is a fool!

Hufahamu hata maana/tofauti ya sherehe za chama na taifa.

Kasome kwanza civics!

Mambo kama haya hata mtu mwenye common sense ambaye halifahamu hata darasa atafahamu tofauti ya sherehe za chama na kitaifa,
Magu kaenda huko kwenye sherehe za ccm kama nani?
 
Tofautisha mambo ya chama cha Siasa na serikali na pia kumbuka hadi sasa Rais JPM Sio mwenyekiti wa chama kwa hiyo kuingilia maamuzi ya chama ktk kusherekea ni vigumu. Tusubirie wampe uenyekiti then from there we can judge
 
mkuu matumizi ya viongozi wote wa serikali waliohudhuria yamegharikiwa na ccm au ni kodi zetu?? Tupe pia uhakika wa ccm kulipia matangazo ya moja kwa moja kupitia tbc!
Hapo hupati jibu sana sana utaambulia matusi,lkn husikate tamaa tuendelee kusema na kukemea huu ujinga
 
Back
Top Bottom