Unazingatia nini unapotunga neno siri (nywila)--password?

Attelan

JF-Expert Member
Oct 12, 2023
434
700
Habari wanajukwaa!

Niende moja kwa moja kwenye mada. Neno siri (nywila) ni neno ambalo unalitumia wewe pekee unapoingia kwenye services mbalimbali za kimtandao kama mitandao ja kijamii, baruapepe n.k.

Kuna baadhi ya tovuti humtaka (prompt) mtumiaji kutumia maneno ya siri yaliyo magumu kwani wanagoma kutumia mipangilio ya namba kama 1234567890/0987654321 na kuendelea. Tovuti hizo hulazimisha watumiaji wachanganye herufi kubwa, herufi ndogo, alama maalumu (@,#,$,_,&,-,+,* n.k.). Kwa bahati mbaya watu hupotezea na kuona hilo jambo si la muhimu.

Kuna mmoja wa wadau wangu yeye alikuwa akitumia namba yake ya simu ya mkononi kama neno siri lake katika mtandao wa Facebook miaka hiyo ya 2013. Hapo unakuwa na uwezekano wa kupoteza vitu vyako vingi kama mtu ataamua kukudukua (na hii itakuwa rahisi sana kama mtu atakuwa na namba yako au baruapepe yako ambayo anaijua na anajua neno siri lako ambalo kwa bahati mbaya uwenda ulimwambia mwenyewe).

Unaweza kujipa moyo kwamba hakuna taarifa yako ambayo itakuwa na maana kwao ila ninakuhakikishia kwamba taarifa yoyote ina umuhimu na inaweza kukuletea madhara makubwa kuliko unavyofikiri.

Kuna jambo moja lilitokea nilibaki kushangaa sana, ilikuwa hivi:-

Jamaa mmoja wa mtaani hapa ambaye ni muajiriwa wa Serikali alinifuata siku moja majira ya jioni akiwa anataka nimsaidie jambo.
" Facebook yangu ina shida, naomba nisaidie" hiki ndicho alichoongea. Baada ya kumsikiliza aliniambia kwamba kuna mtu anamsumbua huko Facebook.

" Aliniambia nimtumie namba yangu ya simu ili aniunganishe na matumizi ya bure ya Facebook yaani bila kuunga bando", baada ya kusikia maneno yake nilitamani kucheka ila sikuwa na namna ikabidi nivumilie tu nimwache aendelee.

" Baada ya kumtumia namba yangu ya Facebook baada ya muda alinitumia meseji na kusema ilitakiwa nimtumie namba ambayo Facebook wamenitumia ili amalizie kuniunga na Internet ya bure kwa Facebook" aliendelea.

"Ulimtumia?" ndilo swali pekee nililomuuliza na yeye alijibu kwamba alituma na baada ya hapo amekuta Facebook yake imemtoa kilazima na kwamba hana uwezo wa kuingia tena kwenye akaunti yake.

"Oops!" nilijikuta nimechoka kabisa, nilitoa jibu kwamba basi ameshamzawadia akaunti yake yule mhuni aliyetumiwa namba za OTP.

Niliishia kula pozi na kukaa kimya kwa muda na baada ya hapo nikamwambia tutengeneze nyingine (akaunti) na hapo asithubutu kumtumia mtu OTP atazotumiwa na Facebook wenyewe (Hapa nilipata shida kumuelezea maana ya OTP). Nilishindwa kuelewa inawezekanaje kuwa mtumiaji wa mitandao ya kijamii na usijue namna ambavyo mitandao hii inafanya kazi japo kwa juu juu ukijua utunzaji wa taarifa zako za muhimu.
 
Nina password 1 na ndo natumia ktk kila apps niliyopo.
Huwa sibadilishi password, lakini hii password enyewe, hata napoandika huwa nachekaga sanaa.

Sipati picha wakati najoin JF, nilivyoweka password hii walishtukajee. Woiiiiih
 
Kwa hiyo we unachanganya namba, herufi na alama zingine. Angalau wewe kuna wale ambao anaweza akaandika juma123
 
cocastic kwenye teknolojia kuna mengi sana. Taarifa zako hazivuji ukiwa unaona wala unatambua. Unaweza kuivujisha wewe mwenyewe muda wowote. Mimi aliwahi nitafuta mtu nimrekebishie akaunti yake ya Facebook (ni ke 😂😂😂) alinipa namba na password kabisa na alinikabidhi na simu yake
 
Nina password 1 na ndo natumia ktk kila apps niliyopo.
Huwa sibadilishi password, lakini hii password enyewe, hata napoandika huwa nachekaga sanaa.

Sipati picha wakati najoin JF, nilivyoweka password hii walishtukajee. Woiiiiih
Tupe hint basi nasi tucheke
 
Mie naweka password na sizingatii chochote. Kila mwezi lazima nibadili nywila
 
Password weka iwe mchanganyiko wa nambari, maneno na alama na iwe ndefu...

Mfano mimi passwords nazotumia ni kuanzia characters 15 hivi...
 
Back
Top Bottom