Hivi ikitokea una mwanamke ambae anakunywa pombe na wewe haunywi unawezaje kuishi nae?? Unakuta zile harufu za pombe zinakukera na ukimueleza mwenzio angalau aache pombe haachi. Na kingine mwanamke akinywa pombe naona anakua kwenye risk ya kuchepuka kwa sababu anaweza akapata offer ya mwanaume akalewa watu wakajilia vyao. Wadau nyie mnalionaje hili swala na kama ishakutokea uliwezaje kutatua.
Kwanza pole,
1. kama ndo mnaanzana kwenye mahusiano na unaona huwezi kuvumilia kati sha huo uhusiano kabla haujafika mbali maana usitarajie kuwa iko siku ataacha pombe.
2. Kama umeshamuoa au mmefika mbali kwenye mahusiano na huwezi kurudi nyuma basi ni kuvumilia maisha yenu yote na wewe kutafuta hobby itakayokukeep busy wakati mkeo au mpenzio anakunywa pombe.
3. Kama wakati mnaanza mahusiano au wakati mnaoana hakuwa anakunywa pombe ameanza baada ya kuolewa au wakati mahusiano yameshafika mbali basi huyo alificha tabia zake na sasa kayafichua makucha laah amepata kampani ambayo imemfundisha ulevi kwa ajili ya starehe tuu laah amekuwa na stress (zozote zile) na suluhisho lake limeishia kwenye pombe.
4. Hii ni kwa pande zote mbili ke na me, yafaa wote muwe na interest moja, mkijikuta mmesikiliza moyo yenu ilivoshibana na kutamaniana bila kuangaliana tabia basi mkishazoeana ndo unaanza kuona tabia zake kero.
5. Mke mlevi kwa mume asiyekunywa pombe ni kero. Mme mlevi kwa mke asiyekunywa pombe ni kero. Japo kuna wanywaji kwa afya na akinywa hasababishi kero kwa mwezie kama;
a. Ukiwa na partner mlevi anaweza kunywa hadi kuzima wewe ukiwa sober ndo uanze kumzoa zoa hadi kwenye gari kisha hadi umlaze kitandani umvue viatu nguo au umuache alale navyo hivyo hivyo hadi asubuhi.
b. Hapo bado hajakutukana ile ya kilevi kuwa unamharibia starehe yake, bado hajatapika na wengine kujikojolea. Wengine mkiwa njiani unamrudisha home akwambie simama nikojoe mkojo umenibana tena kwa ukali. Utasikia unataka nijikojolee...
c. Wengine akilewa anaanza kutoa siri za ndani au analia au wengine a nacheka cheka hovyo. Wengine akilewa anaanza kushika shika watu bila kujali kuwa huyu ni shemeji au mtu baki tuu hivo kuwa fedheha kwa wenzao wao. Bado kupotea hela, kuwashika shika hovyo mabaa medi mbele yako akiwa amelewa, kila leo kupoteza simu. Kwa mwanamke ni hatari kubakwa au kurubuniwa au kisha washawishika kimapenzi iwapo mpenzi wake hayupo na kwa wanaume hatari kupiga vya fasta na kuleta magonjwa ya zinaa nyumbani. Wanaume wengi walevi wamebambikiwa mimba si zao na ndo maana wengi hukataa hata mimba ambazo wamezitia kweli.. kiufupi ulevi ni kero kwa asiye mlevi.
d. Kwakweli kero za ulevi ni nyingi kwa wasio walevi japo wapo walevi anakunywaaa weeh na ni waoga, akiona amezima basi atalala hata hapo bar asubuhi ndo anarudi home huyu anaogopa kupata ajali. Wengine akiona amekunywa kutoshea basi ananyanyuka anarudi home kimya bila kumbughudi mtu hadi asubuhi maisha yanasonga.
Kero ni nyingi mie naona kwa wanywaji au walevi bora waoane na wanywaji au walevi wenzao ili tabia ziendane na wasikerane. Na wasio kunywa kabisa waoane wenyewe kwa wenyewe wabakishe kero ya uzinzi na kukesha disco. Mwisho wa siku hakuna mkamilifu hata mie Kasie jina mapungufu yangu.
Na enjoy kuwa single, simkeri mtu sikerwi na mtu
Single for life.
Kasie mie.