Unaweza kupata hela kwa kuangalia video online?

Zacht

JF-Expert Member
Jul 17, 2020
1,009
2,197
Wataalamu wa mitandao naomba mnijibu Kama ni kweli inawezekana kupata hela kwa kuangalia video online.

Nimeuliza kwa sababu Kuna dada flani(rafiki yangu) alikuwa anapost picha za screenshots status zikionyesha ameingiza hela kwa kuangalia video online nikamuuliza kweli unapata hela akasema niamini napata hela kweli.

Nikamwambia hebu fanya mpango wa kuniunganisha akanitumia link ,nilivyoifuata ile link kulikuwa na sehemu ya usajiri nakasajiri lakini baada ya kumaliza kusajiri ni kakuta Kuna kulipia kiingilio Kama 15000 hivi hapo nilifunga zote .

nikamuuliza vipi tena mdada mbona sielewi akanimbia ndio hivyo lazima utoe kiingilio ,nikamwambia nitajiunga siku nyingine sijajiunga hadi leo .hela aliyokuwa anapata sio nyingi alikuwa anatuma status amepata 8k,10k,12k per day kutokana na bidii yako ya view kwa maelezo yake, Sasa na Mimi nikashawishika nakaona ngoja na Mimi niwe napata hela za bando.

Naomba wataalamu mnijuze/mtujuze Kama hiki kitu kime-exist duniani kweli na Kama kipo tusaidiane bando zetu zisiende bure.

NB
Mtandao ulikuwa wa wakenya na malipo yake yalitolewa kwa Kenya sh
 



Jaribu kufatilia hapo ,naona thread yako iko na same content

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom