Unatakiwa kupewa nini baada ya kurudisha mkopo wote benki?

maryarca

New Member
Oct 9, 2015
1
1
Habari,

Naomba tuelimishane kuhusu mikopo ya bank kwa wafanyakasi na wafanya biashara.

Pale umefanikisha kurudisha mkopo wao wote, wanatakiwa kukupa nini

Je, utarudisha mkopo uondoke zako bila kupewa chochote, nauliza kwakua unapo chukua mkopo, unasign mikataba, unajaza fomu, unandika barua za ofisini, serikali za mitaa, unalipa riba, hati miliki, salary slips, hata kurudisha mkopo pia, unandika barua mambo ni mengi.

Sasa umefanya vyote ivyo, vizuri kabisa na umerudisha mkopo wao wote vizuri kabisa, kuna cheti chochote unapewa!

Je, wanarudisha riba yako!? Naomba kufahamu wanatakiwa kukupa nini, baada ya kukamilisha kurudisha mkopo wao wote.
 
Sasa umefanya vyote ivyo, vizuri kabisa na umerudisha mkopo wao wote vizuri kabisa, kuna cheti chochote unapewa!

Je, wanarudisha riba yako!?
Naomba kufahamu wanatakiwa kukupa nini, baada ya kukamilisha kurudisha mkopo wao wote.
Habari yako,

Unaongelea jambo muhimu ambalo linahusu haki na stahili ya wakopaji baada ya kukamilisha kulipa mikopo yao kwa ukamilifu.

Kwa kawaida, benki au taasisi nyingine ya kifedha inapaswa kumpa cheti cha kumaliza mkopo kila mkopaji anaporudisha mkopo wake kikamilifu.

Hii ni kama ithibati au uthibitisho kwamba mkopaji amelipa mkopo wake wote na sasa hana deni tena kwa taasisi hiyo ya kifedha.

Cheti hiki huwa na:
  • Jina la mkopaji;
  • Nambari ya mkopo;
  • Tarehe ya kuanza na kumaliza mkopo;
  • Kiasi cha mkopo alichokopeshwa;
  • Idadi ya miezi au miaka aliyolipa mkopo;
  • Kiasi cha jumla alicholipa ikiwa ni pamoja na riba;
  • Sahihi na muhuri wa benki/taasisi iliyotoa mkopo.
Baadhi ya faida za cheti cha kumaliza mkopo:
  • Inathibitisha kuwa mkopaji hana deni tena kwa taasisi hiyo ya kifedha
  • Inamsaidia kupata mikopo mingine kutoka kwa taasisi nyingine za kifedha
  • Inathibitisha uwajibikaji na uaminifu wake katika kulipa madeni
  • Inamjengea historia nzuri ya kifedha kwa baadaye.
Kwa hiyo mkopaji anastahili kupewa cheti hiki cha kumaliza mkopo. Si vizuri akamilishe bila kupata ithibati yoyote.

Kuhusu riba - hii huwa hairejeshwi , Ndio faida yao benki husika, na Ni sehemu ya masharti ya mkopo na ni malipo halali kwa huduma ya mkopo.

Kwa hiyo kwa ufupi, mkopaji anastahili cheti cha kumaliza mkopo lakini hakuna fedha za riba zinazorejeshwa.

Naomba nikutakie siku njema.
 
Kwa mawazo yangu!

Naona wana staili kutoa risiti ya huduma ambayo wamesha toa, ilo la kwanza

Pili wange weka utaratibu wa kupata shahada fulani ili viwe vielelezo/CV kama ukihitaji tena mkopo mahala pengine ili iwe rahisi kupata huduma, means sio lazima upitie mchakato wa documentation nyiiingi kana kwamba ndio unaanza kukopa
 
Habari yako,

Unaongelea jambo muhimu ambalo linahusu haki na stahili ya wakopaji baada ya kukamilisha kulipa mikopo yao kwa ukamilifu.

Kwa kawaida, benki au taasisi nyingine ya kifedha inapaswa kumpa cheti cha kumaliza mkopo kila mkopaji anaporudisha mkopo wake kikamilifu.

Hii ni kama ithibati au uthibitisho kwamba mkopaji amelipa mkopo wake wote na sasa hana deni tena kwa taasisi hiyo ya kifedha.

Cheti hiki huwa na:
  • Jina la mkopaji;
  • Nambari ya mkopo;
  • Tarehe ya kuanza na kumaliza mkopo;
  • Kiasi cha mkopo alichokopeshwa;
  • Idadi ya miezi au miaka aliyolipa mkopo;
  • Kiasi cha jumla alicholipa ikiwa ni pamoja na riba;
  • Sahihi na muhuri wa benki/taasisi iliyotoa mkopo.
Baadhi ya faida za cheti cha kumaliza mkopo:
  • Inathibitisha kuwa mkopaji hana deni tena kwa taasisi hiyo ya kifedha
  • Inamsaidia kupata mikopo mingine kutoka kwa taasisi nyingine za kifedha
  • Inathibitisha uwajibikaji na uaminifu wake katika kulipa madeni
  • Inamjengea historia nzuri ya kifedha kwa baadaye.
Kwa hiyo mkopaji anastahili kupewa cheti hiki cha kumaliza mkopo. Si vizuri akamilishe bila kupata ithibati yoyote.

Kuhusu riba - hii huwa hairejeshwi , Ndio faida yao benki husika, na Ni sehemu ya masharti ya mkopo na ni malipo halali kwa huduma ya mkopo.

Kwa hiyo kwa ufupi, mkopaji anastahili cheti cha kumaliza mkopo lakini hakuna fedha za riba zinazorejeshwa.

Naomba nikutakie siku njema.
Maelezo mazuri mkuu.

Na vipi kuhusu bima ya mkopo, huwa inarudi au ndo imeenda hiyo.
 
Taarifa zote za mkopaji kuhusu marejesho ya mkopo hutunzwa na benki inayokopesha. Kupata mkopo mwingine ndio uthibitisho wako kuwa unalipa mkopo wako kwa wakati. Unapoanza kukwepa kulipa mkopo ulioomba, unabatizwa jina baya na taarifa zake mbaya kuhusu mwenendo usioridhisha hupelekwa kwenye taasisi nyingine iitwayo "Credit bureau".
 
Back
Top Bottom