Waraka wa Mwinjilisti Bujibuji kwa wana JamiiForums wote. Soma ufaidike na hekima ya Simba Nyamaume

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,886
155,868
Dondoo za maisha:

1. Usiwakopeshe ndugu zako. Wasaidie.
¹ Ndugu zangu wapendwa katika jamvi hili adhimu la JamiiForums nawausia, usimkopeshe nduguyo, msaidie.

²Kuna ndugu wazandiki wenye husda, anakuja na gia ya kukopa, kumbe hana nia ya kurudisha, usimkopeshe, mpe aende.
³Leo familia nyingi hazina mahusiano mazuri, tatizo au chanzo, kilianza na mbegu ndogo sana. Hatuwezi kumfurahisha kila mtu, ni vyema kama hutaki kumsaidia, umjulishe wazi kuwa hitaji lake li nje ya uwezo wako.

2. Usisalimiane kwa kupeana mikono hali ukiwa umekaa.
¹Sio kwetu vijijini tu, ila popote uendapo, heshimu kila mtu na mpe heshima yake yeye mwenyewe akiona na kuthibitisha. Kama umekaa jamvini, kigodani, safari au kwenye kiti chochote, akitokea mtu anakusalimia kwa kukupa mkono, hata akiwa ni mtoto au ni mdogo sana kwako, inuka, mpe mkono, rudi ukae. Je utapata hasara gani kwa tendo lisilogharimu dakika zako tatu?

3. Kuwa na mipaka na maneno yako, usiwaambie watu ambacho hawapaswi kukisikia wala kukijua.
¹Comrade, jiepushe na kuongea sana. Jiepushe kuelezea matatizo yako kwa kila mtu. Chagall na bagua watu wa kukujua. Acha watu wakuone upande wako mmoja tu, wa mazuri na wa mafanikio. Ruhusu wachache sana kujua madhaifu, mapungufu, matatizo, magumu na machungu unayoyapitia.

²Mapito yako magumu ni furaha kwa adui wako, na tena ni silaha mbaya ya maangamizi ya kukuangamizA.

³JIFUNZE kukidhibiti kinywa chako. Wacha kinywa chako ukitumie kwa kula na kunywa, usikitumie kinywa chako kutangaza mafanikio yako, yaache yajitangaze.

4. Usile Tonge la kwanza wala la mwisho mwisho la chakula ambacho hujakinunua.
¹Wana Nzengo wangu wa JF, chalula ni ibada. Chakula ni lango lako la mafanikio, au ni lango la anguko lako.
² Chakula usicho kilipia jua kwamba kimegharamiwa. Kuna gharama mbili kubwa, gharama za kimwili na gharama za kiroho.
³ Gharama za kimwili ni zile gharama za kukinunua na kukiandaa chakula hicho.
⁴ Gharama za rohoni ni ibada, dua, sala na manuizo yanayofanyika wakati wa maandalizi ya chakula hicho na athari zitokanazo au zitakazopatikana baada ya wewe kula chakula hicho.
⁵ Mpe heshima aliyegharamia afungue Tonge la kwanza baada ya kunawa, pia afunge kwa Tonge la mwisho.

5. Usishiriki upumbavu wowote hata kama unakupa hela leo.

6. Usimkosoe mpisha ukiwa ugenini.
Mpendwa ndugu mwana JF, ukienda ugenini vumilia yote, hata wali ukiwa haujaiva, au ugali una mabunye, usimseme vibaya mpishì. Chakula ni uzima tena ni mauti.

7. Muda wote, tumia akili mapenzini na kamwe usitumie hisia.
¹ Ewe binti yangu na kijana wangu, nawaonyeni, kwenye mapenzi haswa haya mapenzi yenu ya mtandaoni, blind dating etc, usiwekeze moyo, moyo unao mmoja tu, na hauna spare part.
² Ili ufaidi mapenzi vizuri na yasikuumize, usitumie mapenzi au moyo au hisia kupenda, tumia akili. Fanya reasoning kwenye kila ufanyalo, jiepushe na assumptions.
³ Kwenye mapenzi usiwekeze ndoto zako, wala pesa zako, wala destiny yako. Kwenye mapenzi wekeza kucha na nywele, hata ukivikata vitaota tena.
⁴ Muda wote kumbuka usalama wa afya yako ya moyo na akili ni namba moja. Mapenzi ya kijinga ya kutumia hisia no hatari kwa afya yako ya akili, moyo ,tumbo na uchumi wako. Think big, think brave , Think smart.
⁵ Jua na tambua kwamba mapenzi ni mchezo wa watu wasio na akili wala watu serious. Be funny, puuza mambo ya uzushi, furahi, tabasamu, mchekeshe mwenzako, yaani tu kuwa popoma au poyoyo la mwenzako nanyi mtaishi kwa salama na amani.
8. Usipokee simu yako katikati ya maongezi.
Ndugu yangu, katikati ya maongezi yenu, nakusihi, usiyakatishe kwa kupokea simu na kuongea kirefu. Bora upokee na kusema nitakupigia baadae, kisha uzime. Kabla hujaanza mazungumzo, ni bora uzime simu au uiweke kwenye hali ya mtetemo.

9. Usile hela ya kazi ambayo hujaifanya.
Huu ni wito kwenu vijana na wazee wenzangu, uaminifu ni mtaji namba moja.
¹ Leo fundi mwaminifu anaonekana ni kinyozi peke yake, wengine wote matapeli na magirini, unajua kwa nini? Kwasababu walikula advanced payments. Kinyozi halazi kazi.
² Uaimifu ni mtaji, jijengee hali ya kuaminika na utaaminiwa.
³ Ukiwa peke yako, hamna anayekuona, hakikisha huvunji sheria, hicho ñdio kipimo cha awali cha uaminifu.

10. Sikiliza, itikia kwa kichwa na tumia lugha za mwili ukiwa unapokea taarifa za watu wengine.
¹ Unaletewa umbea, ubuyu, au taarifa za mbaya za mtu yeyote yule, eidha unamjuà au humjui, ni boss wako au mdogo kwako, au mko ĺevel moja.
² Sikiliza tu, uwe msikilizaji mkubwa, jiepushe na ku comment, utanaswa na vinasa sauti uaibike.
³ Kama kuna jambo la wewe kulikubali, ama kulikataa, usitoe neno, tumia bichwa lako, peleka kulia na kushoto kuonyesha umekataa, au tingisha kichwa chako juu na chini kukubali. Usitumie sauti.
⁴ Tabasamu sehemu zenye kufurahisha, khuzunika sehemu zisizo furahisha. Tumia alama za mwili kuonesha hisia zako, shika tama unapopigwa na butwaa.
⁵ Usimkatishe tamaa mleta umbea na ubuyu, jifunze kutoka kwake, jihadhari naye, kuna sehemu pia anapeleka taarifa zako.

11. Usimkwaze kwa kumvunjia heshima nduguyo, rafikiyo au yeyote yule mbele ya watu wake waheshima, iwe wakwe au watoto ama wafanyakazi wenzie
Ndugu, usije ukamfanyia masikhara ya kudhalilisha au kuvunjia heshima mtu yeyote mbele ya wale wanaomheshimu.
Kila jambo lifanye kwa kiasi bila kumvunjia mtu yeyote heshima.

12. Usiruhusu hisia zako zizidi akili zako.
Waswahili tunasema sikio halizidi kichwa. Maumivu ya siku moja ya njaa ya yasikufanye uuze utu wako. Esau kwa njaa ya siku moja aliuza haki yake ya uzaliwa wa kwanza. Kwa njaa na tamaa ya matumbo ya viongozi wetu, tumeuza rasilimali za nchi yetu. Hela tutaenda kuficha ughaibuni, nchi zao zitaifanyia biashara hiyo hela yako haramu na zitafaidika zaidi. Hapa nimeongea kwa level ya juu kidogo. Jiulize wewe, je hisia zako zinakuharibia vipi hitma ya maisha yako? (Your Life destiny ?)

13. Usijipindekeze, Jiepushe na Uchawa.
Ndugu yangu mpendwa, tuliye zaliwa wote na huyu baba yetu mpendwa wa pekee Mzee JamiiForums, ninakusihi sana, jiepushe na kujipndekeza, jiepushe na uchawa.
Kujipendekeza hakukujengei heshima kwa unaye jipendekeza kwake, ila kunakudhalilisha na kuutweza utu wako. Hamna boss anayemwamini mtu anayejipendekeza, anamtumia tu kupata taarifa za watu mbalimbali, ila moyo wake uko mbali sana na wewe.
Uchawa una kilio kikubwa kuliko kicheko.

14. Kuwa nadhifu mudà wote, usingoje sikukuu na matukio maalum.
Ndugu kama ambavyo upendo husitiri wingi wa dhambi, hali kadhalika unadhifu na utanashati husitiri ufukara wetu. Sio tu ufukara wetu, ila pia utanashati unafanya tukubalike, tuheshimike, tuaminike na pia utanashati ni mlango wa kibali au Favour

15. Usimpige ngwara, teke wala mtama mtu ambaye tayari yuko chini kwa mweleka.
¹Maisha yana milima na mabonde, huenda unamdai jamaa, au ndugu yako, au rafiki yako, lakini yu mahututi kitandani. Usimbughudhi. Tena huenda ana madeni mengine makubwa

²Tafadhali na wewe ongeza maarifa yako tuikuze hii injili ya Bujibuji kwa Wana JamiiForums imguse kila mmoja.

³Injili hii inaletwa kwenu kwa hisani ya Nakubusu, Gwappo Mwakatobe, Mshana Jr, Elly, Watu8, Bill Lugano na Pearl a.k.a LULU. ⁶⁶⁶
 
Masomo mazuri sana Tena Bure ni Bando tuu,Ahsante
 
Usimsahau mzazi/mlezi alokulea wakati hujielewi,kumbuka alijitoa sadaka sana wewe kuwa ulivyo.Wasaidie wawapo wahitaji maana na wewe ulikuwa muhitaji kwao zaidi sana wakizeeka wakumbuke maana hawana nguvu kumbuka na wewe ukipata neema utazeeka.

Usilipe baya kwa baya,maana hutakuwa na tofauti na alokutendea ubaya.Wewe lipa jema kwa baya ulotendewa ili umfundishe mjinga kwa vitendo.
 
Saidia ndugu ila wekeza sana kwa mkeo na watoto wako kwani ukifa leo au kesho familiar yako watabaki peke yao bila msaada wa ndugu zako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom