Unataka Utajiri? Njoo Tunduma haraka!


Hii kitu ni kweli iko Tunduma na hata Mbeya mjini. Wenyewe ambao wanafurahia huo utajiri wanasema kila kitu kinawezekana 'ujasiri wako tu'. Sasa kuhusu hizo sentensi nilizoweka red, mimi nilipata maelezo tofauti kidogo;
1. Jogoo akichagua mahindi kadhaa, ina maana sawa kuwa utakuwa tajiri wa kufa mtu kwa kipindi hicho. Tofauti inayobaki ni kuwa unafanywa msukule. Muda wa kutumika msukule ukiisha, then unauawa moja kwa moja
2. Kipindi kile ukiwa msukule, wanasema unapewa 'rejesho' unalotakiwa kurudisha kila siku. Hii inatokana na 'matajiri wapya' waliopo kwenye mng'aro ambao wewe unakuwa unawatumikia. Ni kwamba wakati wewe ulipokuwa ukifaidi utajiri ni kuwa kuna watu waliofanywa misukule ndio walikuwa wanakuletea mali, hivyo sasa inakuwa zamu yako kuwatumikia wengine
3. Huo msukule kazi unazofanya ni kuiba kimazingara fedha na vitu vya thamani toka nyumbani kwake i.e. kuchota ule utajiri wake alioucha na kuupeleka kwa mganga ili awagawie 'matajiri wapya'. Na kama haujitoshelezi basi unahamia kuiba kwa ndugu na jamaa zako.
4. Inasemekana pia ukishindwa kufikisha 'rejesho' la muda uliopewa basi unapata viboko vya haja. Kwa hivyo salama yako iwe kuwa 'rejesho' ni dogo kuliko uwezo wa wewe kurejesha, la sivyo kila siku unalalia fimbo
 
Matthew 16:26 KJV

For what is a man profited, if he shall gain the whole world, and lose his own soul? or what shall a man give in exchange for his soul?

ndo ushangae sasa,hata mtu awe na mabilioni atakufa atayaacha,ni upuuzi mtupu.
 
Tajirika mwenyewe umalize ndugu zako wote,wenzio tuna chapa kazi ili tupate kihalali
 
dalili za kukata tamaa na athari za kunywa VIROBA kwa wingi,.......wenye hela ni washirikina!
umenifurahisha sana mkuu,Tanzania ukiwa na hela kama sio fisadi basi watakuita mchawi.hawaamini katika kufanya kazi kwa bidii. Ndio maana hata maofisini anaejituma kazini lazima aundiwe zengwe kwamba anamajungu au anajipendekeza kwa bosi...wabongo tufanye kazi kwa bidii fursa zipo nyingi tutatajirika tu.!
Kama
 

Unasahau kuwa watanzania tunaishi kama kuku wa kienyeji, kila mtu anajihangaikia mwenyewe. Ndio maana maskini wanakua na hela sababu wanajua hayupo wa kumsaidia zaidi ya nguvu zake.
 
...Huu upo nje nje tu, wala sio hadithi...
Kuna utajiri gani huko si tungewasikia au kuwaona km huko Mirerani, Geita au wangetoa matajiri wanaohesabika km kina Rostam, EL, MENGI, Bakhresa lakini wapi wote huko unaambiwa wamewaweka watoto au wazazi wao Misukule
Utajiri wa Tunduma ni wa Mipakani km Tarakea, Namanga nk kuwa na makaratasi mengi (Noti) mifukoni
 
watanzania bwana! hebu badilikeni jamani, unatumia muda mwingi kujadili mambo ya kusadikika, and then, mwisho wa siku unatoa povu kwa kulalamikia serikali? badilikeni jamani, maji hufuata mkondo, na kizazi chenu kitafuata nyayo zenu hizo hizo.
 
Nilidhani jogoo anawekewa punje za mahindi kwenye kinyeo cha kijana kisha anadonoa ili kumfanya kijana awe lijali
 
habari nzurii.huo utafiti ulimshirikusha pia huyo mganga au ni vipi?
 

.
Halafu kibaya zaidi asilimia kama 99 ya maduka ya Tunduma yanapiga nyimbo za injili(kwaya).
.
 
Tunduma bana kwa mambo ya ushirikina sikatai maana kuna siku (wiki tatu zimelizopita) nilikuwa hapo mchana kulitanda bonge la wingu radi zinapiga hatari mwenyej wetu akasema hii mvua hainyeshi cz wafanyabiashara wameanika mazao yao na kweli haikunyesha ila mm binafsi nilishannua mpk mwamvuli

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Utajiri wa punje,mambo ya wakinga hayo, watoto wa mwakipande hao.
 
Hivi ni ukweli haya Mambo? Na kwa mfano huyo mganga anaekupa masharti akifa inakuaje? Na ukifa utajiri unabaki ili familia iuendeleze?
 
mkuu jogoo akidonoa mahindi mawili inakuaje sasa?..si unaruhusiwa ku appeal..bt ntakuja mda ambao jogoo najua ana njaa
Hahaha Aisee hizi Mambo nadhani ni watu wanahadithia baada ya kuangalia Nigeria film
 
Mkuu haya Mambo umejuaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…