Unamkumbuka Multaza Lakha?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unamkumbuka Multaza Lakha?!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Sajenti, Jul 9, 2010.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kuna advocate mmoja kwa jina la Multaza Lakha kwa wale waliokuwa wakifuatilia ile kesi ya uhaini miaka ya 80. Huyu bwana kwa kumbukumbu zangu ni miongoni mwa mawakili waliokuwa mahili sana nyakati zile. Kwenye ile kesi ya uhaini iliyowahusisha akina Zacharia Hans Pope, Mr & Mrs Banyikwa, Capt. Eugene Maganga na wengine, Multaza Lakha aliwahi kumhoji aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma wakati huo Mzee Ndejembi na mtoto wake kama mashahidi wa upande wa mashitaka. Mapaka leo bado nakumbuka jambo moja ambalo Lakha alimwambia mtoto wa Ndejembi alipokuwa akitoa ushahidi wake.....hapo ni baada ya Ndejembi kuchemsha katika kujibu maswali ya Lakha..nanukuuu " yaani wewe na baba yako mmetoka Dodoma kuja hapa kutoa ushahidi wa uongo??"... Ni kesi ya miaka mingi sana lakini nilikuwa nikiifatilia ingawa bado nilikuwa mwanafunzi. Kuna yeyote anayejua liko huyu Multaza Lakha???:A S 39::A S 39:
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Advocate Lakha alienda Uingereza kwenye miaka ya katikati ya 1980s... ni kama alikimbia nchi kiaina inavyosemekana.
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  Murtaza Lakha, nakumbuka kusoma exchanges za mahakamani za kesi ya uhaini katika Mfanyakazi kila Jumamosi. Enzi hizo za kina Jame Nhende, kabla hata ya Stan Katabalo (RIP) na Loliondogate.

  Eighties babies hawawezi kuelewa, y'all make me feel old already.

  Hivi Mfanyakazi bado lipo ?
   
 4. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ya, Alikuwa ni advocate maarufu sana na machachari katika enzi zake, baada ya ile kesi ya uhaini hakusikika tena, sijui nini kilimpata
   
 5. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
   
 6. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Ni MuRtaza Lakha. Hivvi wako wapi James Nhende na lile 'trupu' lao la Mfanyakazi ya wakati ule ambao kuna wakati ilikuwa inaongoza kwa mauzo katika magazeti yote nchini?
   
 7. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Pia niliwahi kusoma series ya story za Capt. Eugene Maganga kwenye gazeti la Rai mwaka 2007. Kwa kweli jamaa alivyokuwa anaelezea ile habari na anataja maeneo mengi ambayo harakati zao zilikuwa zikifanyika nadhani kama angeandika kitabu nina imani kingepata soko sana...
   
 8. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..James Nhende yuko Mwanza ameanzisha magazeti kama sio gazeti lake moja linaitwa kasi mpya lingine nimesahau jina.
   
 9. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Asante Mkuu. Kulikuwa na wale waandishi waliojipa jina la sijui 'Maluteni wa burudani' Charles Charles, Rashid Zahor na Hemed Kimwaga waliishia wapi??
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huyu charles Charles amekuwa mwandishi mamluki; unamkodisha anakuandika kunyoosha mambo a' la wakina Ra na EL!1
   
 11. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Kwakweli Mfanyakazi la enzi zile ndo angalau lilikuwa wazi maana enzi zile UHURU,MZALENDO na DAILY/SUNDAY NOISE tuu... Mpiga picha Senga sijui yuu wapi... Nadhani Hemed Kimwaga ameshatangulia mbele ya haki... Mwaweza nisahihisha!
   
 12. N

  Ngala Senior Member

  #12
  Jul 9, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  namkumbuka pia wakili muccadam. kimsingi kesi ile ilitikisa njiiiii hiii mpaka ikaondolewa mahakamani njii ilikuwa na wanasheria makini
   
 13. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  mmmh......?
   
 14. R

  Rwegoshora Member

  #14
  Jul 10, 2010
  Joined: Jul 23, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu kama sikosei ni huyu jamaa na website yake hii hapa.

  Murtaza Lakha
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Jul 10, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  He is the one..mhhh..hapa umri umesonga kweli...

  Katika uhai wake alikuwa mtu mwema sana, mcheshi na mkarimu!
   
 16. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #16
  Jul 10, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mola ampumzishe kwa amani
   
 17. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 772
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 180
  Aliwahi kusaidia kushinda kesi gani?
   
 18. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #18
  Jul 10, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Mkuu, sina hakika sana na hili. nadhani Kimwaga bado yupo hai ingawa sina hakika kwa asilimia mia%. tafadhali hebu cheki tena source zako...
   
 19. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #19
  Jul 10, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Preta, what with the mmmm...?

   
 20. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
   
Loading...