The Voices From Within: "Mahakamani Watashindwa Tena!" Sababu ni Mawakili! Jee Tanzania Tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?Jitokezeni Kusaidia!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,582
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa huja na makala za "Kwa Maslahi ya Taifa" Makala ya leo ni The Voices From Within kuwa "Japo Hawakutendewa Haki Ndani ya Chama Chao Chadema Kwa kufukuzwa Kwa kuvuliwa uanachama Kikangroo na CC ya Chadema iliyokaa as a kangaroo court, ikawavua uanachama na baadae kikao cha Baraza Kuu kuyabariki maamuzi yale batili ya Kikangroo ya CC yao. Wakakimbilia mahakamani ili kutafuta haki, na huko Mahakamani kwa mara ya kwanza waligonga mwamba na sasa wamefile kesi nyingine.

Sauti hii "The Voices From Within" imeniambia " Safari hii huko Mahakamani pia Watashindwa Tena!" Sababu ni Kuwatumia Mawakili ambao ni mawakili tuu. Kuna mawakili na mawakili bora. Hii kesi ilihitaji Mawakili Bora wa calbre ya Murtaza Lakha. Jee kwenye safu ya mawakili wetu Tanzania, Jee tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?. Kama wapo, please Jitokezeni Kusaidia ili kuepusha hukumu ya karma kuwashukia wahusika wa kadhia hii.

Mtu ukikosa haki kwenye Taasisi yako, ukakimbilia mahakamani, ili upate haki, ukakosa haki mahakamani, jee uende wapi baada ya hapo?.

Kitachobaki ni kitu kimoja tuu kumuachia Mungu ambaye ndiye pekee hutoa hukumu za haki kupitia kitu kinachoitwa karma "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

Leo mchana huu, nilikuwa napitia bandiko fulani, mara nikaisikia sauti, "the voices from within" ikinieleza kuwa japo wamefile upya kesi, lakini Watashindwa tena and this time it will be fatal, hivyo uamuzi hautakuwa struck out kama mwanzo, this time the case will be dismissed entirely on its totality and kila mmoja will bear his own costs!.

The voices from within, huwa haitoi sababu, lakini kwenye suala hili mimi nazijua sababu ambazo ni just some simple logic, wanawatumia mawakili wenye uwezo duni!. Sasa kabla hata hiyo kesi mpya haijapangiwa siku ya kusikilizwa, natoa wito kwa manguli wa sheria, hata kama hawajawa contracted, wajitokeze wajitolee kuwasaidia hawa wadada, ili watendewe haki.

Kwa jinsi nilivyoisoma ile hukumu, kusema ukweli wanawatumia mawakili wenye uwezo mdogo au wa wastani sana kiasi kwamba kuna baadhi ya makosa ni silly mistakes, hivyo mtu aliyefanya silly mistakes kama zile, hata akirejebisha makosa na ku file tena, I doubt kama atakuwa na uwezo wa kuargue kesi writs kama za habeas corpus, mandamus, prohibition, quo warranto and certiorari, sio kesi za kumpa tuu wakili yoyote ili mradi ni wakili, hizi zinahitaji kuwa handled na mawakili mawakili kweli ambao ni mawakili bora na sio hawa ma bora wakili wanaofile kesi kwa makosa ya kijinga kabisa na kupeleka mahakama ku struck out!. Leo mpaka nimemkumbuka Wakili Murtaza Lakha.

Kwa vile mimi ni mtu wa mastori hivyo naomba kuikatiza kwanza hii mada, nianze na mastory mastory ya Pasco Mayalla, halafu nije kumrudia Wakili Murtaza Lakha kisha ndio ni drive home hoja yangu. Hivyo kama wewe sio mtu wa mastori mastori, ishia hapa halafu rukia kule chini
Kati ya fani zote kabisa duniani, fani ambayo ni rahisi sana kusomea ni sheria, sifa pekee ya kusomea sheria ni kujua kusoma na kuandika, hivyo toka nikiwa mdogo nikajipanga nitakuwa Mwanasheria.

Tangu nikiwa mdogo nakuwa nikawakuta wazazi wangu wote wawili ni wafanyakazi wa serikali wakifanya kazi bomani.

Mwaka 1976 tulikuwa tukiishi Mwanza eneo la Isamilo ya chini nyumba yetu ndio nyumba ya pili Isamilo ya chini, nyumba ya Kwanza ni nyumba ya RC, pale kilimani, nyumba yetu ni ya pili, next ni RPC, next ni DSO, next ni OCD.

Wakati huo nikiwa darasa la pili, sikujua hata kumetokea nini lakini siku moja nimerudi kutoka shule pale Nyakahoja, just a working distance from home, nakuta mizigo imefungashwa imetolewa nje, kuangalia next house, kwa RPC, the same, kwa DSO the same, kwa OCD the same unajiuliza kumetokea nini?, just puzzled, no one tells you kumetokea nini wewe si mtoto utajua nini?.

Nikaambiwa tunahama, nikauliza mbona tunahama na masanduku tuu na vyombo vya jikoni, vipi makochi yetu vitanda etc?. Kumbe fenicha zote kwenye nyumba za serikali, ni mali ya serikali, wewe unakuja na nguo zako tuu kama kwenye apartments!.

Kumbe mambo yalianzia juu serikalini kwa Makamu wa Pili wa Rais enzi hizo, Rashid Kawawa, Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi, Waziri wa Usalama , Peter Siovelwa, IGP Pundugu, DGIS, Emelio Mzena, wote walistaafishwa kwa manufaa ya umma, na huko Mwanza kuanzia RC, RPC, RSO, DSO na OCD, wote wamemwaga Unga na kurudishwa kijijini at the place of domicile!.

Naomba niikatishe hii story to make this long story short, Ila kwa kifupi ni Baba alifutwa kazi tulirudishwa kijijini!. Nimejikuta mimi ni like father like son, kuna type fulani ya watu wanapenda sana starehe, hivyo wanaishi as if hakuna kesho, ni kula, kunywa na starehe zote kwa kwenda mbele, kumbe hata gari na pesa za starehe ni pesa za serikali, halafu mara ghafla unatupwa kijijini, hakuna umeme, maji, ... naomba nisimalizie...

Niliokolewa kutoka kijijini na Baba Mdogo, ndio nikaingia jijini Dar es Salaam tukikaa Drive in nikisoma Oysterbay.

Mwaka 1978 nikiwa darasa la 4, ndipo Kesi ya Mauaji Mwanza Ikaanza kuunguruma na kuripotiwa RTD na magazetini. Ni kupitia media ndio nikajua dingi alikuwa nani na washitakiwa ni wale majirani 4, RPC, RSO, DSO na OCD wa Mwanza.

Mzee alikuwa akitetewa na wakili Murtaza Lakha. Ni Mzee wangu tuu pekee ndiye aliyechomoka the rest walikula mvua za kutosha!.

Baada ya kusoma maendeleo ya kesi hiyo nika develop interest ya kuwa wakili kuwa nikiwa mkubwa nitakuwa kama Lakha.

Nikamaliza Oyster bay nikaenda Tambaza, then Ilboru. Kipindi cha ujana maji ya moto kimenikutia Ilboru, ni Boys only tumezungukwa na vibinti vyeupe vya kabila la Waarusha, ukigusa tuu...!, kuna kusoma?.

Ni kipindi hicho ndio tukakutana na kina Tundu Lissu, Ayub Rioba huku kina Mwingulu Mchemba na Lazaro Nyalandu ni madogo wa nyuma yetu.

Kama nilivyosema kule juu, sheria ndio fani rahisi kusomea kuliko fani zote, ili mtu kusomea sheria, enzi hizo ulihitaji kujua tuu kusoma na kuandika.

Enzi hizo kwa Tanzania LL.B ilitolewa UDSM pekee, na chuo kilikuwa kinachukua wanafunzi 60 only, hivyo kusoma LL.B, lazima upate Division One Kali!.

Kama nilivyoeleza maisha ya Ilboru, hali niliyokutana nayo kule, matokeo yangu ya form 6, nilikosa Div 1 kwa point 1!. Ukikosa Div 1, you have to forget sheria ndoto ya kuwa Murtaza Lakha, ikafia hapo!.

Nikaenda kusomea uandishi wa habari, nikaajiriwa RTD miaka 5, TV zilipoanza nikaenda DTV 5 years na TVT ilipoanzishwa nikawa ndio waanzilishi.

Mwaka 2003 nikiwa TVT, nikapigwa zegwe nikapigwa chini!. By then tayari niliishakuwa Mtangazaji maarufu, na tujisenti ninavyo, huku nchini mwetu Tanzania milango ya mtu yoyote mwenye pesa za kulipia unaweza kusoma chochote, hivyo nika ji enrolled FoL, UDSM, kusoma LL.B na kuhitimu 2007.

Ni baada ya kuhitimu LL.B ndio nika realize Niko more comfortable as a journalist than as a lawyer, hivyo nikaamua kuendelea na maisha as a freelance journalist.

Uandishi wa habari sio fani ngumu, kila mtu anaweza kuwa mwandishi wa habari, lakini ili kuwa mwandishi mzuri habari unahitajika kuwa na kipawa fulani au kipaji fulani.

Ujio wa social media umerahisisha sana upashanaji wa habari sasa every Tom, Dick and Harry can be a journalist na fani imevamiwa, kila mtu ni mwandishi wa habari, kama sio wa main stream media, then ni mwandishi wa social media, Facebook, Twitter Instagram YouTube Pinterest TikTok, Whatsapp na SMS.
Sasa ndio narejea baada ya mastory mastory ya Pasco Mayalla.

As days go by nikiangalia mienendo ya baadhi ya kesi, nimemkumbuka sana wakili Murtaza Lakha, nimejiridhisha hata fani ya sheria nayo imevamiwa, kila mtu mwenye LL.B, anaweza kuwa wakili.

Japo kila mtu mwenye LL.B anaweza kuwa wakili, na fani ya uwakili imevamiwa, ili kuwa wakili mzuri, zaidi ya kuwa admitted kwenye Bar, lazima pia uwe na uwezo fulani na kipawa fulani.

Kwa haya yanayoendekea mahakamani sasa, nimemkumbuka sana wakili Murtaza Lakha alikuwa ni wakili mzuri, kama sio Murtaza Lakha, Mzee wangu asingetoka!.

Ile sauti ilioniambia Watashindwa tena kesi sababu ya kuwatumia mawakili ili mradi ni mawakili tuu, badala ya kuwatumia mawakili bora, wao wanawatumia na bora wakili!.

Kwa vile mhusika mkuu wa kesi hiyo na yeye pia ni mwasheria, nilitaraji kwa vile Zitto Kabwe na yeye pia aliwahi kutimuliwa na chama kile kile kwa mtindo ule ule wa a Kangaroo Court, Zitto alifungua kesi hivyo hivyo na kesi yake ilitupwa katika hatua za awali, hivyo Bi dada alipoamua kufungua kesi hii ilipofunguliwa tulitaraji wangewatumia mawakili manguli wa sheria na sio wakili tuu alimradi ni wakili.

Hata kwa majaji wetu, niliwahi kusema kitu kuhusu utoaji haki na uwezo wa baadhi ya majaji Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Kitendo tuu cha shauri kuwa struck of fatal procedural improperity ni uthibitisho tosha wa mawakili wenye uwezo wa wastani?.

Natoa wito kwa manguli wa sheria wajitokeze wajitolee kuwasaidia hawa wadada ili watendewe haki, lengo la kuwasaidia watendewe haki sio tuu ili kuwatendea haki hawa Wabunge 19 bali kuiepuka adhabu ya karma itakayo itandika chama chao na viongozi wake, kufuatia the consequences of karma ya Zitto kwa chama hicho na viongozi wake, wasipotendewa haki, the karma consequences will be bad, big and devastating!.

Paskali
 
Watashindwa sio kwasababu ya mawakili, bali watashindwa kwasababu haki haipo upande wao.

Kama walishindwa wote waliokuwa na kesi kama yao, kwanini nao wasishindwe?

Wacha kupeleka lawama zako pasipostahili ili kuficha madhaifu ya chama chako, na spika wenu, nyie ni wavunjifu wa sheria.
 
Swali la msingi ni je, walipata baraka za chama chao wakati wakienda mjengoni? Ikiwa ndio basi wameonewa, ila kama sio basi acha wapate stahiki yao.

Kuna mmoja nilimuona akibusu picha na kwa kusoma mazingira chama chao hakikuwa kwenye good terms na aliyekuwa pichani sasa hapa panaleta maswali zaidi? Anyways watajijua wenyewe, mie acha niangalie ya CCM.
 
Hawa wabunge wa Covid 19 wataishia kuingiziwa madolido na akina Halima ila kwa sasa thamani yao ni karibu na zero

Thamani yao ni kuwatoa Chadema kwenye harakati za katiba mpya na kuwapeleka kwenye harakati za kuwafukuza wabunge 19. Angalia nyuzi za hapa Jamii Forums, nyingi zinahusu sakata la hao wabunge. Nyuzi za katiba mpya ni chache sana.
 
Swali la msingi ni je, walipata baraka za chama chao wakati wakienda mjengoni? Ikiwa ndio basi wameonewa, ila kama sio basi acha wapate stahiki yao.

Kuna mmoja nilimuona akibusu picha na kwa kusoma mazingira chama chao hakikuwa kwenye good terms na aliyekuwa pichani sasa hapa panaleta maswali zaidi? Anyways watajijua wenyewe, mie acha niangalie ya CCM.

..barua ya chama huandikwa baada ya kikao cha kamati kuu kufanya uteuzi.

..sasa inafahamika kwamba kama kamati kuu haikuketi kufanya uteuzi.

..Kwa msingi huo inawezekana kina Halima walikwenda moja kwa moja kuapa kwa Spika kwa MAAGIZO tu bila kuwahusisha Nec.
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa huja na makala za "Kwa Maslahi ya Taifa" Makala ya leo ni The Voices From Within kuwa "Japo Hawakutendewa Haki Ndani ya Chama Chao Chadema Kwa kufukuzwa Kwa kuvuliwa uanachama Kikangroo na CC ya Chadema iliyokaa as a kangaroo court, ikawavua uanachama na baadae kikao cha Baraza Kuu kuyabariki maamuzi yale batili ya Kikangroo ya CC yao. Wakakimbilia mahakamani ili kutafuta haki, na huko Mahakamani kwa mara ya kwanza waligonga mwamba na sasa wamefile kesi nyingine.

Sauti hii "The Voices From Within" imeniambia " Safari hii huko Mahakamani pia Watashindwa Tena!" Sababu ni Kuwatumia Mawakili ambao ni mawakili tuu. Kuna mawakili na mawakili bora. Hii kesi ilihitaji Mawakili Bora wa calbre ya Murtaza Lakha. Jee kwenye safu ya mawakili wetu Tanzania, Jee tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?. Kama wapo, please Jitokezeni Kusaidia ili kuepusha hukumu ya karma kuwashukia wahusika wa kadhia hii.

Mtu ukikosa haki kwenye Taasisi yako, ukakimbilia mahakamani, ili upate haki, ukakosa haki mahakamani, jee uende wapi baada ya hapo?.

Kitachobaki ni kitu kimoja tuu kumuachia Mungu ambaye ndiye pekee hutoa hukumu za haki kupitia kitu kinachoitwa karma "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

Leo mchana huu, nilikuwa napitia bandiko fulani, mara nikaisikia sauti, "the voices from within" ikinieleza kuwa japo wamefile upya kesi, lakini Watashindwa tena and this time it will be fatal, hivyo uamuzi hautakuwa struck out kama mwanzo, this time the case will be dismissed entirely on its totality and kila mmoja will bear his own costs!.

The voices from within, huwa haitoi sababu, lakini kwenye suala hili mimi nazijua sababu ambazo ni just some simple logic, wanawatumia mawakili wenye uwezo duni!. Sasa kabla hata hiyo kesi mpya haijapangiwa siku ya kusikilizwa, natoa wito kwa manguli wa sheria, hata kama hawajawa contracted, wajitokeze wajitolee kuwasaidia hawa wadada, ili watendewe haki.

Kwa jinsi nilivyoisoma ile hukumu, kusema ukweli wanawatumia mawakili wenye uwezo mdogo au wa wastani sana kiasi kwamba kuna baadhi ya makosa ni silly mistakes, hivyo mtu aliyefanya silly mistakes kama zile, hata akirejebisha makosa na ku file tena, I doubt kama atakuwa na uwezo wa kuargue kesi writs kama za habeas corpus, mandamus, prohibition, quo warranto and certiorari, sio kesi za kumpa tuu wakili yoyote ili mradi ni wakili, hizi zinahitaji kuwa handled na mawakili mawakili kweli ambao ni mawakili bora na sio hawa ma bora wakili wanaofile kesi kwa makosa ya kijinga kabisa na kupeleka mahakama ku struck out!. Leo mpaka nimemkumbuka Wakili Murtaza Lakha.

Kwa vile mimi ni mtu wa mastori hivyo naomba kuikatiza kwanza hii mada, nianze na mastory mastory ya Pasco Mayalla, halafu nije kumrudia Wakili Murtaza Lakha kisha ndio ni drive home hoja yangu. Hivyo kama wewe sio mtu wa mastori mastori, ishia hapa halafu rukia kule chini

Sasa ndio narejea baada ya mastory mastory ya Pasco Mayalla.

As days go by nikiangalia mienendo ya baadhi ya kesi, nimemkumbuka sana wakili Murtaza Lakha, nimejiridhisha hata fani ya sheria nayo imevamiwa, kila mtu mwenye LL.B, anaweza kuwa wakili.

Japo kila mtu mwenye LL.B anaweza kuwa wakili, na fani ya uwakili imevamiwa, ili kuwa wakili mzuri, zaidi ya kuwa admitted kwenye Bar, lazima pia uwe na uwezo fulani na kipawa fulani.

Kwa haya yanayoendekea mahakamani sasa, nimemkumbuka sana wakili Murtaza Lakha alikuwa ni wakili mzuri, kama sio Murtaza Lakha, Mzee wangu asingetoka!.

Ile sauti ilioniambia Watashindwa tena kesi sababu ya kuwatumia mawakili ili mradi ni mawakili tuu, badala ya kuwatumia mawakili bora, wao wanawatumia na bora wakili!.

Kwa vile mhusika mkuu wa kesi hiyo na yeye pia ni mwasheria, nilitaraji kwa vile Zitto Kabwe na yeye pia aliwahi kutimuliwa na chama kile kile kwa mtindo ule ule wa a Kangaroo Court, Zitto alifungua kesi hivyo hivyo na kesi yake ilitupwa katika hatua za awali, hivyo Bi dada alipoamua kufungua kesi hii ilipofunguliwa tulitaraji wangewatumia mawakili manguli wa sheria na sio wakili tuu alimradi ni wakili.

Hata kwa majaji wetu, niliwahi kusema kitu kuhusu utoaji haki na uwezo wa baadhi ya majaji Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Kitendo tuu cha shauri kuwa struck of fatal procedural improperity ni uthibitisho tosha wa mawakili wenye uwezo wa wastani?.

Natoa wito kwa manguli wa sheria wajitokeze wajitolee kuwasaidia hawa wadada ili watendewe haki, lengo la kuwasaidia watendewe haki sio tuu ili kuwatendea haki hawa Wabunge 19 bali kuiepuka adhabu ya karma itakayo itandika chama chao na viongozi wake, kufuatia the consequences of karma ya Zitto kwa chama hicho na viongozi wake, wasipotendewa haki, the karma consequences will be bad, big and devastating!.

Paskali

Ww na Halima Mdee ni wanasheria, kwenye kesi hii ndio mlipaswa mdhibitishe hiyo elimu yenu ya sheria. Unamlaumu Halima na genge lake kumpa wakili dhaifu, lakini hata ww huthubutu kutuonyesha kile unachojisifu nacho kila siku hapa jukwaani! Nilikuambia ww ni mjanja wa mjini, lakini huna uwezo wowote kwenye hicho unachojisifia. Badala ya ya kuleta mabandiko ya nongwa huku jukwaani, nenda mahakamani ukatuzibe midomo kwa kuwatetea kina Halima.
 
..barua ya chama huandikwa baada ya kikao cha kamati kuu kufanya uteuzi.

..sasa inafahamika kwamba kama kamati kuu haikuketi kufanya uteuzi.

..Kwa msingi huo inawezekana kina Halima walikwenda moja kwa moja kuapa kwa Spika kwa MAAGIZO tu bila kuwahusisha Nec.
Hilo liko wazi, sijui kwanini watu wanajizima data!
 
Ulisoma kipande kindogo tu. Soma ukurasa wa nne utaona. (Angalia na.6)
Screenshot_20220625-224156.png
 
Ww na Halima Mdee ni wanasheria, kwenye kesi hii ndio mlipaswa mdhibitishe hiyo elimu yenu ya sheria
Mkuu Tindo, kwanza niendelee kutoa appreciation kwako kwa kuchangia nyuzi zangu mbalimbali kwa michango very objective. Kwenye uzi huu nimesema kuna kesi na kesi na kuna mawakili na mawakili, sio kila wakili anaweza kila kesi, hizi kesi za kesi writs kama za habeas corpus, mandamus, prohibition, quo warranto and certiorari, sio kesi za kumpa tuu wakili yoyote ili mradi ni wakili, hizi zinahitaji kuwa handled na mawakili, ambao ni mawakili kweli ambao ni mawakili bora wa calibre ya Murtaza Lakha na sio hawa ma bora-wakili, na hili la Watanzania wanapokuwa na kesi fulani, hawajui waende kwa wakili gani ni tatizo!, hata ile kesi ya ugaidi ya Mbowe, tungekuwa na mawakili wa calibre ya Murtaza Lakha, ile kesi inaanza tuu, ilikuwa iishe next hearing kwa DPP kuleta nolle!, haikupaswa hata kufikia stage ya guilty verdict na Mbowe kuonekana has a case to answer ila DPP ndio kaokoa jahazi kwa nolle.

Elimu ya sheria, a possession of an LL.B is one thing, practicing sheria is another thing, and being good is quite another.

Kuna watu kibao they possess excellent LL.B and they don't practice mimi being one of them, LL.B yangu ni Hons!. Kuna wengi wana practice and they are not good at all!. Huyu nguli Murtaza Lakha, ninayemtaja hapa, he doesn't even possess a law degree!. Hivyo kusoma sheria, kupata LL.B, na kuwa wakili, does not guarantee you can be the best, hivyo naomba usitutake mimi na Halima tuthibitishe hizi elimu zetu za sheria, possession is one thing, practicing is another and being good quite another.
. Unamlaumu Halima na genge lake kumpa wakili dhaifu, lakini hata ww huthubutu kutuonyesha kile unachojisifu nacho kila siku hapa jukwaani!
Sijamlaumu Halima kumpa wakili dhaifu, nimesema kwa vile kesi kama hii kuna precedent ya Zitto, Halima should have known better!. Kwenye kesi kama hii, Zitto alijikwaa, akaanguka, Halima kabla hajafungua kesi kama hii, alipaswa aangalie Zitto alijikwaa wapi na sio kuangalia alipoangukia, sasa Halima ameanzia hapo hapo Zitto alipoangukia, badala pale alipojikwaa, hivyo Halima alifika pale Ziito alipojikwa, na yeye akajikwaa pale pale na akaanguka vile vile!.

Mimi sijisisifu bali hutoa tuu facts kuwa mimi ni Mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea ambaye pia ni holder wa an LL.B (Hons) mwenye Msonge wa LW. 100 Constitutional law ambayo haya mambo writs kama za habeas corpus, mandamus, prohibition, quo warranto and certiorari, ndimo mwake mwake.
Nilikuambia ww ni mjanja wa mjini, lakini huna uwezo wowote kwenye hicho unachojisifia.
Kama kusema kuwa una LL.B (Hons) na A ya constitutional law ni kujisifu, nimesema kule juu na hapa nasema tena na tena, possession of an LL.B is one thing, lakini uwezo ni something else.

Uwezo ni ability, namna ya means za kuutumia huo uwezo ni capacity, na namna ya kuutumia huo uwezo ni capability. Mimi ndio ninajijua nina uwezo gani yaani the ability, the capacity and the capabilities, akiibuka mtu akakubeza kwa sababu hujaonyesha, kitu cha kufanya ni sio kuendelea kusema au kuonyeshea ili watu waone bali ni kumwambia tuu "thank you".
Thank you Mkuu Tindo
Badala ya ya kuleta mabandiko ya nongwa huku jukwaani, nenda mahakamani ukatuzibe midomo kwa kuwatetea kina Halima.
Mimi sio wakili, mimi ni Mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, na amini usiamini hivi ninavyo wasaidia humu jf ni msaada mkubwa sana!.
P
 
Back
Top Bottom